Sep 7, 2016

UDICTETA UCHWARA NDIO HUU

TUNAJIFUNZA NINI KUTOKA IVORY COAST??

By bukuku tz,

Huyu anayevutwa na Askari sio kibaka, sio mwizi, sio mfuasi wa chama cha upinzani ambao wengi wamezoea kuonewa bila sababu. Huyo ni Rais wa nchi. Ni Rais wa zamani wa Ivory Coast Ndg.Laurent Gbagbo.

Kwa taaluma ni Gbagbo Mkemia, lakini kabla ya kusomea masuala ya kemia alikua mwalimu wa shule ya sekondari. Alipata PhD yake ya Kemia mwaka 1979 kutoka chuo kikuu cha Paris Diderot University (Ufaransa).

Hakuwahi kufikiria kuwa Rais wa nchi hiyo licha ya kujaribu kugombea mara kadhaa. Alipata nafasi ya urais kibahati bahati baada ya kiongozi wa mapinduzi wa nchi hiyo Jenerali Robert Guéï kukata jina la mtangulizi wake Henri Konan Bédié, pamoja na jina la Waziri Mkuu wa zamani aliyekua anapewa nafasi kubwa ya kushinda Ndugu Alassane Ouattara.

Wakati Gbagbo akigombea Urais wa nchi hiyo alijipambanua kama mtetezi wa wanyonge, mpenda demokrasia, mtu anayeumizwa na matatizo ya watu maskini, na mpenda haki. Alijipambua kama mtu wa "KAZI" kwa ajili ya kuinua maisha ya watu maskini. Akajinasibu kujenga viwanda hasa vya Cocoa, kahawa na mafuta yanayochimbwa nchini humo.

Lakini alipoingia madarakani akaanza kukandamiza demokrasia, kubana vyama vya upinzani, kubana vyombo vya habari, kupandisha kodi hadi kwenye bidhaa zinazotegemewa na watu maskini. Akaanza kutoa upendeleo kwa watu wa familia yake na kuteua ndugu zake kushika nafasi za juu katika wizara na idara za serikali.

Akamkamata na kumuweka kizuizini Waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Ndugu Alassane Ouattara kwa sababu aliamua kujiunga na chama cha upinzani cha Republican. Akasahau kwamba wakati Ouattara akiwa Waziri mkuu yeye alikua Mbunge tu ktk serikali Félix Houphouët-Boigny. Licha ya wafuasi wa chama chake kukamatwa bila sababu, Oattara hakuweka kinyongo. Bado alisalimiana na Gbagbo na kumheshimu kama Mkuu wa nchi.

Lakini Gbagbo akalewa madaraka. Akafikia hatua ya kuona kwamba yeye ndiye mtu pekee aliye sahihi katika nchi hiyo na maneno yake ni sheria. Akapuuza katiba ya nchi. Akaagiza kukamatwa kwa vijana wengi waliokua wafuasi wa vyama vya upinzani wanaomkosoa. Akapiga marufuku maandamano ya kisiasa.

Baadhi ya raia wa Ivory Coast wakalalamika kuwa Rais wao ameanza kuwa "Dikteta". Lakini kila aliyesikika akimuita Gbagbo dikteta aliishia korokoroni. Hatimaye Gbagbo akawa ndiye msemaji wa mwisho, mwenye nguvu na mamlaka juu ya mambo yote na kauli yake haitakiwi kupingwa wala kusahihishwa.

Ziara yake ya kwanza nje ya nchi alimtembelea Rais wa Burkina Fasso, swahiba wake Blaise Compaoré ambaye alikua na elements za udikteta. Compaore ndiye aliyemuua Thomas Sankara (the true son of Africa) na kujitangaza Rais mwaka 1987.

Kwahiyo Gbagbo aliporudi na kuanza kuongoza nchi yake kibabe, kukamata wanaomkosoa na kufungia vyombo vya habari, wananchi wakajua ni matokeo ya urafiki wake na dikteta Compaore.

Hali ya uchumi ya Ivory Coast ikazidi kudorora siku hadi siku. Watumishi wengi wa umma hawakulipwa mishahara yao kwa wakati, wawekezaji wengi wa kigeni wakafunga biashara, hakukua na nyongeza ya mishahara kwa watumishi lakini nyongeza ya kodi ilikua kwenye kila bidhaa na huduma.

Rais Gbagbo akapandisha ushuru/kodi katika Bandari ya Abidjan. Wafanyabiashara wengi wa nchi za Burkina Fasso na Mali wakaanza kupitisha mizigo yao kwenye bandari za Togo, Benin, na Liberia. Rais Gbagbo aliposhauriwa na wachumi juu ya athari ya maamuzi yake alikua mkali na kutishia kuwafukuza kazi waliomshauri. Alisema ni heri zije meli chache zenye kulipa kodi kubwa kuliko meli nyingi zenye kulipa kodi ndogo.

Hatimaye idadi ya meli zinazotua katika bandari ya Abidjan zikaanza kupungua kutoka meli zaidi ya 35 kwa mwezi hadi wastani wa meli 8 hadi 12 kwa mwezi (ingia hapa  http://www.marinetraffic.com/en/ais/index/eta/all/port:1150/portname:ABIDJAN). Pia mapato ya bandari yakaanza kupungua. Kilimo cha Cocoa ambalo ni zao kuu la biashara nchini humo kikaanza kuporomoka na uzalishaji wa mafuta ukaanza kupungua.

Uchumi ukazorota na hali ya maisha ikazidi kuwa ngumu. Rais Gbagbo akadhani watu wameficha pesa majumbani kwao, kumbe ni matokeo ya mfumo wa uchumi alioutengeneza mwenyewe.

Lakini wakati hayo yote yakiendelea, mamlaka ya mapato ya Ivory Coast (Cote' d’Ivoire General Direction of Taxes) ikawa inatangaza kukusanya mapato makubwa na kuvuka lengo kila mwezi. Wananchi wakajiuliza hayo mapato yanaenda wapi kama watumishi hawalipwi mishahara, huduma muhimu za jamii zimeongezwa kodi, madai ya watumishi hayafanyiwi kazi, miundombinu haijengwi, hospitalini hakuna madawa, benki zimesitisha mikopo, na Rais mwenyewe analalamika pesa haipo katika mzunguko. Je hayo makusanyo makubwa ya kodi yanatoka kwenye vyanzo vipi, na yanatumikaje mbona maisha yanazidi kuwa magumu?

Hatimaye mwaka 2010 wananchi wa Ivory Coast wakashindwa kuendelea kuvumilia shida, manyanyaso, ubabe, hali ngumu ya maisha, ukandamizaji wa demokrasia, na udikteta uchwara wa Rais Laurent Gbagbo. Kwenye uchaguzi mkuu wa November 28 mwaka 2010 wakamchagua Waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo (kipenzi cha watu, mtu asiye na visasi) Alassane Ouattara kwa asilimia 54.1% ya kura zote halali.

Tume HURU ya uchaguzi ya nchi hiyo, Ivorian Election Commission (CEI) ikamtangaza mgombea wa upinzani ndugu Ouattara kuwa mshindi wa kiti hicho cha Urais. Lakini Rais Gbagbo akakataa kuachia madaraka. Akajitangaza kuwa yeye ndiye mshindi na akadai kuwa amepata asilimia 51% ya kura zote halali.

Baada ya kujitangaza mshindi akatangaza pia kuivunja tume ya uchaguzi (CEI) na akatangaza kutotambua matokeo ya Tume hiyo. Pia akatoa amri kwa jeshi la nchi hiyo kufunga mipaka yote ya nchi (ya kuingia na kutoka) na akafukuza waandishi wote wa habari kutoka vyombo vya habari vya kimataifa waliokua wakiripoti uchaguzi huo. Akazifungia Radio na magazeti yote ya nchi hiyo yaliyotangaza kuwa ameshindwa uchaguzi.

Lakini wananchi wakaungana kupinga hatua hizo za kidikteta za Rais Gbagbo. Wakaaondoa tofauti zao za kidini, kikabila na kikanda kama ambavyo wamekuwa wakigawanywa na wanasiasa kwa muda mrefu. Wakaamua kuungana kwa pamoja kupinga maamuzi hayo. Wakristo ambao wengi wapo kusini mwa nchi hiyo na waislamu ambao wapo kaskazini wakaweka tofauti zao chini na kuungana kwa pamoja kupinga udikteta uchwara wa Rais Gbagbo.

Maandamano makubwa ya kumshinikiza Gbagbo kuachia ngazi yakafanyika katika mji mkuu wa Abidjan na kuzingira Ikulu yake. Japo mwanzoni Polisi waliuwa raia walioandamana lakini haiwakukatisha tamaa wengine kuingia barabarani. Hatimaye kufikia Aprili 10 mwaka 2011 Rais Gbagbo akawa amezingirwa na maelfu ya watu katika Ikulu yake. Watu wenye hasira ya uonevu aliowafanyia, watu wenye uchungu wa kuumizwa na kunyanyaswa, watu wenye kiu ya demokrasia.

Gbagbo akajua siku yake ya kiyama imefika, hofu ya mauti ikamvaa. Ikulu aliyoiona kama "paradiso" yake, ikageuka kuwa "bonde la uvuli wa la mauti". Akaomba msaada kwa walinzi wake wamtoroshe. Lakini walinzi wakashindwa kumtorosha kutokana na msongamano mkubwa wa wananchi waliozingira Ikulu.

Wananchi waliokua wamezingira Ikuku hiyo wakadai kuwa wanamtaka Gbagbo atolewe nje wamuadhibu kwa mikono yao wenyewe vinginevyo watachoma Ikulu hiyo afie ndani. Hatimaye serikali ya Ufaransa (mkoloni wa zamani wa Ivory Cost) ikatoa helcopter maalumu na makomandoo kadhaa kwenda kuepusha maafa ambayo yangeweza kutokea.

Makomandoo hao wakafika Ikulu ya Gbagbo na kumkuta amejificha uvunguni mwa kitanda kwenye handaki la chini kwenye ikulu hiyo akiwa na mkewe Simone Gbagbo. Wakamtoa na kuondoka nae. Wakamuepusha na "mauti" kutoka kwa raia wake.

Hatimaye Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo (kipenzi cha watu) Alassane Ouattara akatangazwa na kuapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo. Na Gbagbo akapandishwa kizimbani ICC ambako anakabiliwa na makosa ya uhalifu dhidi ya binadanu (crimes against humanity), ikiwa ni pamoja na mauaji ya wapinzani wake, ubakaji, vitisho/ubabe na ukiukwaji wa utawala wa sheria (murder, rape and persecution).

#Umejifunza_nini?

Aug 9, 2016

MWANAUME ALIYEPORWA MWANAMKE NA NUHU MZIWANDA AJITOKEZA HADHARANI

Ubuyu wa mjini unanyetisha kuwa, mkali wa Bongo Fleva anayetamba nawimbo wake wa Jike Shupa aliomshirikisha Ali Kiba, Natfal Mlawa‘Nuh Mziwanda’, anadaiwa kupora demu wa jamaa ambaye naye ni msanii wa wa Bongo Fleva, Valentino Michael ‘Vale wel’.Mrembo anayedaiwa kuporwa kwa Vale ni yule Nawali ambaye kwa sasa Nuh anamnadi kuwa ni mpenzi wake wa kiyama.Ubuyu ulionaswa na Wikienda ulidadavua kuwa mwenye demu wakealipigwa na butwaa alipomuona Nuh akimnadi Nawali kwenye mitandao yakijamii ndipo akang’atwa sikio kuwa kwa sasa hana chake kwani ‘mtoto’ yupo mikononi mwa Nuh.Akimwaga chozi mbele ya Wikienda, Vale alisema kuwa mpaka sasa hajaelewa ni kwa nini Nuh ameamua kumtangaza Nawali kuwa ni mpenzi wake wakati akijua wazi kwamba ni shemeji yake na ni mwanamke wake wa siku nyingi kwani wanafahamiana.“Kiukweli nilikuwa sijui hili wala lile. Nilipoingia mitandaoni nilipigwa na butwaa kumuona Nuh akijitangazia ufalme kuwa mpenzi wake kwa sasa ni Nawali.“Mwanzoni nilijua labda ni mambo ya kiki kwa sababu nijuavyo Nuh hana malengo mazuri na Nawali.“Baadaye ndipo nikawa nahakikishiwa na watu wangu wa karibu kuwa ni wapenzi na hawafanyi kificho.“Kinachoniumiza nilikuwa sina tatizo wala ugomvi wowote na Nawali na bado naamini ni mpenzi wangu kwa sababu hatujaachana na tukikutana huwa tuko kama kawaida,” alisema Vale.
MWENYE KISU KIKALI?
Vale alizidi kutokwa povu kuwa kwa sasa hasemi sana kwa sababu hana mkwanja wa kumpa Nawali hivyo ule usemi wa mwenye kisu kikali unamtafuna kwani inawezekana Nuh anatumia vijisenti alivyonavyo kumnyang’anya tonge mdomoni.“Lakini ukweli ni kwamba ‘nafaiti’ na mambo yatakaponinyookea nitahakikisha nafanya kila njia kumrudisha Nawali kwenye himaya yangu kwani ndiye mwanamke wa maisha yangu.“Najua nilipomtoa, ni mwanamke ambaye ninampenda sana na nimetumia muda mwingi kumbadilisha kimuonekano kwani mwanzoni hakuwa alivyo sasa, alikuwa mgumu hivyo nimefanya jitihada za hali ya juu kumfanya aonekane ‘soft’,” alimalizia Vale.Mwanaume anayedai kuibiwa akiwa na niwale enzi zaoHUYU HAPA MTUHUMIWA NUHBaada ya ubuyu huo ulionyooka kutua kwenye Wikienda, waandishi wetu walimweka ‘mtukati’ Nuh aliyedai kuwa hapendi kumuongelea mpenzi wake huyo kwa sababu kama ni maneno yameshasemwa mengi.“Unajua kuhusu huyu demu wangu, maneno mengi sana yamesemwa hadi nimechoka. Kama huyo mwanaume yupo na anaamini ni mwanamke wake basi amchukue akakae naye,” alisema Nuh akiomba kuachwa atulize mawazo.
NAWALI ANASEMAJE?Kwa upande wake Nawali, alipotafutwa kwa njia ya simu alisema kuwa hamjui Vale na wala hajawahi kupiga naye picha za kimahaba ambazo gazeti hili lina nakalazake.Habari kutoka kwa Wana-Ubuyu wanaolinyaka vilivyo sakata hilo wanadai kwamba Vale ana uhakika kuwa huyo ni mpenzi wake na picha ametoa wakiwa wawili tena kimahaba hivyo inakuwaje Nawali anabisha?
HUYU NDIYE NUHMbali na Nawali, baada ya kufungishiwa virago na Zuwena Mohammed ‘Shilole’, Nuh alitua kwa mrembo mwingine shombeshombe ambaye hata hivyo hawakudumu

Jul 21, 2016

Video:MWANAMKE ALIYE LETEWA PICHA ZA UTUPU KWENYE BOX LA ZAWADI SIKU YAKE YA HARUSI.

ANGALIA VIDEO YA MWANAMKE ALIYELETEWA PICHA ZAKE ZA UTUPU SIKU YA HARUSI YAKE,PICHA ALIZOPIGA NA BWANA WAKE WA ZAMANI