MKAZI wa kitongoji cha Chelsea, jijini London,Mare Simone(54) amefanya ngono na wanaume 1,500 katika kipindi cha miaka 23 ili kuwatibu matatizo yanayohusiana na mapenzi.
Wateja ni miongoni mwa wanaume 10,000 waliokwenda ofisini kwake kupata tiba ya matatizo hayo.
Mjasiriamali huyo anatoa ushauri wa mambo ya kimapenzi kwa wanawake na wanaume na ametamba kuwa yeye ni mtaalamu wa masuala ya kitandani.
Baada ya kuachana na mumewe, Mare aliamua kuisomea rasmi taaluma hiyo ya mapenzi na kisha kufungua ofisi na hadi sasa ametoa somo la mapenzi kwa zaidi ya wateja 10,000 waliofika kwenye ofisi yake katika kipindi cha miaka 23.
Mare amebainisha kwamba, kati ya wateja hao,hadi sasa amefanya ngono na wanaume zaidi ya 1,500 wakiwemo waume au wapenzi wa wanawake wengine.
Amesema,hadhani kuwa anafanya kosa lolote kinyume cha sheria kutembea na waume za watu kwa sababu anaboresha maisha ya mapenzi ya watu wengine,anapata riziki yake kwa kutoa tiba hiyo, na kwamba, yeye si kahaba.
"Watu wananilipa kwa ushauri ninaowalipa na kwa kutibu matatizo yao hawanilipi kwasababu ya ngono".
"Najipatia kipato changu kwa kulala na waume au wapenzi wa wanawake wengine.
Lakini mimi sifanyi ukahaba kwa kuwa taaluma ya mapenzi inaruhusiwa kisheria na mapenzi yanafanyika katika mazingira ya tiba" alisema Mare.
"Nasaidia kuimarisha na kubadilisha maisha ya kimapenzi ya maelfu ya wanaume na hivyo nakuwa nimesaidia kuimarisha maisha ya kimapenzi ya wake zao au wapenzi wao"
"Wanawake wengine wanabeba mimba za wanawake wengine kwa sababu wanataka kuwasaidia wanawake wasio na uwezo wa kupata mimba.
Hali hiyo ni sawa na mimi kwani nawasaidia watu kuwa na maisha mazuri ya kimapenzi".
Mare anaifurahia kazi yake na huwa na furaha zaidi wateja wake wanapoondoka kurudi majumbani mwao wakiwa na matumaini mapya kwenye maisha yao ya kimapenzi.
Kwa siku anatoa vipindi vitano vya masuala ya mapenzi,wateja wake ni watu wa rika mbali mbali, jinsia zote, maumbile tofauti na wafanyakazi wa vitengo tofauti tofauti.
"Wanaume mara nyingi hunifuata kwa sababu ya matatizo ya kutosimama vyema kwa uume na kufika kileleni mapema kabla ya wapenzi wao wakati wengine huambiwa waje wanione na wake zao kwakuwa hawawaridhishi kitandani".
"Kabla hawajaniona huwa wote wanapimwa magonjwa ya zinaa na lazima watumie kondomu iwapo nitalala nao" alisema Mare.
"Kwa wanawake mara nyingi hunifuata wakiwa na matatizo ya kutofika kileleni au wanapoona wapenzi wao hawajui jinsi ya kuwaridhisha kitandani".
"Huwa nawafundisha jinsi ya kujipa raha wao wenyewe na kuipenda miili yao" amesema na kusisitiza kwamba hatarajii kuacha kutoa huduma hiyo katika miaka 10 ijayo.
hapo chini ni picha ya mwanamke huyo