Yanga yatolewa nje na Al Ahly, yakubali kichapo cha goli 2-1
Wawakilishi pekee wa Tanzania katika mashindano makubwa ya vilabu barani
Afrika (CAF Champions League), Yanga wametolewa katika mashindano hayo
baada ya kupokea kichapo cha goli 2-1 kutoka kwa Al Ahly ya Misri.
Katika
mchezo huo ambao ulionekana timu zote kukamiana ulianza kwa kasi huku
timu zote zikishambuliana kwa zamu na hadi mapumziko hakuna timu
iliyokuwa imefanikiwa kuona lango la mwenzake.
Kipindi cha pili Al
Ahly ilifanikiwa kupata goli kupitia mchezaji wake Hossam Ghaly katika
dakika ya 51 ya mchezo huo na dakika 15 mbele yaani dakika ya 66 Yanga
ilisawazisha goli hilo kupitia Donald Ngoma.
Mchezo huo uliendelea
kwa timu zote kushambuliana kwa zamu na katika dakika ya 90+5 ya mchezo
huo, Al Ahly kupitia Abdallah El-Said ilipata goli la pili nala ushindi
ambalo limewawezesha kuingia nafasi inayofuatia.
Baada ya matokeo
hayo, Yanga imetolewa katika mashindano hayo na kuungana na wenzao Azam
ambao nao walitolewa jana ambao wote walikuwa wakishiriki mashindano ya
vilabu Afrika ambayo yanaandaliwa na Chama cha Soka Afrika (CAF).
No comments:
Post a Comment