Mvua zinazo endelea kunyesha jijini dar es salaam zimesababisha madhara makubwa kwa wananchi waishio na wafanyao biashara maeneo ya kariakoo Baada ya mvua hiyo kusababisha hasara kwa wafanya biashara ambao walibaki kushuhudia mali zao zikisombwa na maji yaliyo sababishwa na mvua hizo zinazo endelea kunyesha kwa kasi.
Pia katika maeneo ya barabarani kulikua na msongamano mkubwa wa magari yaliyo zimika kutokana na maji yaliyo sababishwa na mvua hizo kubwa.
Kwa upande mwingine wafanya biashara walilazimika kufunga maduka ili kuepukana na janga hilo,
tatizo kubwa linalo onekana ni swala la miundo mbinu,Wananchi wameiomba Serikali kutenga fedha ili kurekebisha miundo mbinu hiyo ambayo inaonekana kuto kaa katika hali ambayo haijitoshelezi..
Apr 21, 2016
MAFURIKO YATIKISA DAR
Subscribe to:
Posts (Atom)