May 12, 2016

MZIWANDA:NILIWAFUMANIA MADEE NA SHILOLE LIVE..


Aisee hii hata mimi nilipitwa nayo ama kweli mimi mapenzi basi nimeyavulia Shati.

akuu mapenzi sio ubondia bora nijitoeLeo akihojiwa na Diva clouds Fm Mziwanda amekiri kuwa Madee alitembea na Shilole kipindi wapo wote na Aliwafumania na kumkuta mmoja wao akiwa hana nguo,Diva anakiri kusikia hizo habari ila alitaka Nuh athibitishe Nuh anasema inauma sana ila ana muheshimu sana Madee ana Muheshimu pia Shilole japo Inauma sasa wali kwichi kwichi na kuwafumaniaOyo nitakupigia nitakupia baadae noma noma noma sanaaaaaHapa Miguu pande hapa Say my name Shishi hapa Jike shupa oyooooo

YANGA YAPEWA PONGEZI

Uongozi wa Klabu ya Soka Yanga umetoa pongezi kwa wachezaji wake kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacon Tanzania kwa mara ya pili mfululizo.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Habari wa Yanga Jerry Muro, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya Klabu hiyo na kusema uongozi wa klabu hiyo unawashukuru wachezaji hao kwa kujituma pamoja na mashabiki wa soka wa klabu hiyo kuwaunga mkono kwa kuwashangilia kila michezo.

Amesema Jumamosi ya wiki hii timu ya Yanga itakabidhiwa Kombe lake katika Uwanja wa Taifa mara baada ya kumalizika kwa mchezo wake wa Ligi Kuu dhidi ya Ndanda FC.

Katika hatua nyingine Muro amesema maandalizi ya kuelekea Angola kwa ajili ya mchezo wa marudiano na timu ya Esperanca utakaofanyika Jumatano majira ya saa nane mchana kwa saa za Afrika Mashariki yanaendelea.

UVCCM WAGOMBANIA NYUMBA YA NYERERE MWANZA

Eneo la mapumziko ya Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, limegubikwa na mgogoro kati ya wakazi wa Kata ya Igoma dhidi ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza kuhusu uhalali wa umiliki wa eneo hilo.

Ni mvutano wa miaka kadhaa sasa tangu mgogoro huo ulipoanza kurindima ambapo wakazi wa eneo hilo linalofahamika kama Mtaa wa Nyerere, wamedai kuwa mtaa huo upo chini ya umiliki wao tangu miaka ya 70, wakati wa harakati za Azimio la Arusha ingawa wakazi hao wamethibitisha kuwa wanao uhalali wa kuendelea kuishi katika eneo hilo, lakini Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Nyamagana mkoa wa Mwanza umeyapinga madai hayo.

Wakati mvutano huo ukiendelea, Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyerere Kata ya Igoma John Manoni, akatolea ufafanuzi juu ya mgogoro huo.

Tangu mgogoro huo ulipoanza kurindima miaka ya 70 hadi sasa, umesababisha wakazi wa mtaa huo kushindwa kuliendeleza eneo hilo, huku wakiiomba serikali kuingilia kati ili kutatua mgogoro huo.

SAKATA LA SUKARI:MAKONDA AAGIZA UPEKUZI WA MAKONTENA YA BILIONEA DEWJI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza kuchunguzwa kwa sukari kontena 115 ambayo ni zaidi ya tani 3,000 iliyokutwa katika Bandari Kavu ya PMM iliyopo eneo la Vingunguti.

Makonda alitoa agizo hilo alipofanya ziara ya kushtukiza katika bandari hiyo na kubaini uwepo wa sukari hiyo ambayo ni mali ya Mohamed Enterprises, ambayo kwa taarifa zake aliambiwa zilikuwa kontena 165.

Makonda ameziagiza Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Shirika la Viwango (TBS) kuichunguza sukari hiyo kutokana na sababu mbalimbali zilizojitokeza katika uwepo wa sukari hiyo kama sukari kuagizwa kutoka Dubai lakini imetoka Brazil na imepakiwa Dubai na upangwaji wa kontena hizo katika bandari hiyo.

“Nashindwa kuelewa kwa nini sukari iagizwe kutoka Dubai lakini itoke Brazil na kufungashwa Dubai, inaonesha inaweza kuwa imeshawahi kuisha muda wake hivyo nataka ichunguzwe na tunataka tujue kama Mohamed Enterprises anaficha sukari ili ipelekwe kwa wananchi kwa matumizi,” alisema Makonda.

Mbali na kutoa maagizo hayo, Makonda pia amezuia kutumika kwa sukari mifuko 22,000 iliyokutwa katika ghala la Mohamed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) lililopo Barabara ya Nyerere na kutaka wapeleke vielelezo kuhusu sukari hiyo kwa mamlaka zinazohusika kama ya matumizi yoyote.

WATU 35 KUTOA USHAHIDI KESI YA KUPINGA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI

KISUTU: Baada ya Kesi namba 3/2015 ya kupinga Matokeo ya Uchaguzi ya Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Jijini Dar es Salaam Maulidi

iliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Iddi Azan (CCM) kuahirishwa kusikilizwa mara 3 mfululizo ndani ya wiki hii kwa sababu mbalimbali, Jaji Chocha kutoka Mahakama ya Mbeya ameahirisha tena kusikilizwa kwa shauri la kesi hiyo leo na kuipangia Mei 19 ya mwezi huu.

msingi

ya

Madai

kutoka nane, hivyo

kuahirishwa kwa kesi

baada ya Abubakari Salim Wakili wa upande wa Iddy

mahakama impe muda wa wiki moja wa kuandaa mashahidi

viapo, ambapo Jaji Choche alikubali.

Abubakari Salim

Upande wa Mshitakiwa

(Maulidi Mtulia Mb) umethibitisha kuwa na wenyewe watapeleka mashahidi 10, wakati upande wa mshitakiwa namba 2 na 3 (Mwanasheria Mkuu na Tume ya Taifa ya Uchaguzi), na wao watapeleka mashahidi 15.

Jimbo la Kinondoni waliojitokeza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

manne

Msingi

ya

Madai

katika kesi hiyo ni

Mbunge Mtulia haukuwa halali 2. Katika moja ya Kituo cha Uchaguzi, Mwangalizi wa CUF alipiga kura nyingi kwa ajili ya mbunge huyo, 3. Mawakala

Azani (CCM) walitolewa nje, 4. Unafuu kwa pande zote mbili.

DR.LIPUMBA:AWATETEA WAFANYABIASHARA

Rais Dk. Magufuli alipiga marufuku uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi bila ya kuwa na kibali cha serikali mapema mwaka huu ili kuondoa ushindani usio rafiki kwa viwanda vya ndani vya bidhaa hiyo, Prof. Ibrahim Lipumba, Mtaalam aliyebobea kwenye masuala ya Uchumi,amenukuliwa hivi karibuni akisema Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli anatumia cheo kuwanyanyasa wafanyabiashara.

Lipumba ameyasema hayo katika mahojiano ya moja kwa moja na Kituo kimoja cha Runinga hapa nchini wakati akichambua sakata la ufichwaji wa sukari nchini.

Amesema kuwa endapo angekua anakaa na Rais Magufuli angehakikisha kunakuwepo na utaratibu wa uagizaji wa sukari kwa watu ambao ni waaminifu ambao hawatakwepa kodi zilizowekwa na kuagiza sukari ili pamoja na gharama na faida iweze kuuzwa kwa bei ya Tsh 1,800 ili viwanda vya ndani vinavyozalisha sukari viweze kulindwa.

“Tuepukane na kufanya mambo mazito ya sera kwenye majukwaa ya siasa na kuwatisha wafanyabiashara katika hali ambayo haiendani na hali halisi iliyopo” amesema Prof. Lipumba.

Hayo yanakuja siku chache baada ya Rais Dk. John Magufuli kutangaza kutaifisha tani za sukari zitakazokamatwa zikiwa zimefichwa na wafanyabishara kwenye maghala na kisha kuzigawa kwa wananchi bure.

Hata hivyo imeripotiwa hivi karibuni kuwepo kwa malalamiko ya kupanda bei ya sukari kutoka kikomo cha bei elekezi ya shilingi 1800 kwa kilo hadi kati ya 2,500 na 2,800.

INSTAGRAM YAZINDUA NEMBO MPYAA

Instagram imezindua nembo mpya katika hatua ya kutaka kujiboresha na kutoonekana kuwa programu ya picha pekee.Nembo hiyo imetengezwa kuimarisha ujumbe unaotumwa.Nembo hiyo inaonyesha kamera ya kawaida na rangi za upinde wa mvua.Zaidi ya picha milioni 80 na video husambazwa kila siku katika Instagram.Mtandao huo una takriban wateja milioni400 na uliipiku Twitter mwaka 2014.Wakati Instagram ilipoanza ,ilikuwa eneola kukarabati na kusambaza picha,kampuni hiyo ilieleza.Miaka mitano baadaye,ni eneo linalopendwa na jamii kubwa ulimwenguni ambapo watu husambaza picha na video.Watumiaji pia watagundua kwamba eneo la bluu katika nembo ya mtandao huo limeanza kubadilika na kuwa jeupe.Mtindo huo mpya una lengo la kuimarisha picha na video zinazotumwa bila kubadilisha unavyoingia katika mtandao huo.Ubunifu wa nembo hiyo mpya ulianza mwaka mmoja uliopita ,instagram iliambia Newbeat.Tulitaka kutengeza nembo ambayo ingewakilisha mahitaji ya awali ya sasa na ya siku za baadaye.