May 12, 2016

YANGA YAPEWA PONGEZI

Uongozi wa Klabu ya Soka Yanga umetoa pongezi kwa wachezaji wake kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacon Tanzania kwa mara ya pili mfululizo.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Habari wa Yanga Jerry Muro, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya Klabu hiyo na kusema uongozi wa klabu hiyo unawashukuru wachezaji hao kwa kujituma pamoja na mashabiki wa soka wa klabu hiyo kuwaunga mkono kwa kuwashangilia kila michezo.

Amesema Jumamosi ya wiki hii timu ya Yanga itakabidhiwa Kombe lake katika Uwanja wa Taifa mara baada ya kumalizika kwa mchezo wake wa Ligi Kuu dhidi ya Ndanda FC.

Katika hatua nyingine Muro amesema maandalizi ya kuelekea Angola kwa ajili ya mchezo wa marudiano na timu ya Esperanca utakaofanyika Jumatano majira ya saa nane mchana kwa saa za Afrika Mashariki yanaendelea.

No comments: