May 10, 2016

TRA YAFAFANUA JUU YA SAKATA LA UGAWAJI SUKARI

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetolea ufafanuzi wa sukari tani 6757 mali ya Kampuni ya El-Naeem Enterprises iliyokamatwa hivi karibuni katika Bohari ya Forodha ambapo imesema ilikuwa chini ya uangalizi ikisubiri vibali husika ili iweze kuruhusiwa kusambazwa nchini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania, Richard Kayombo, amesema sukari hiyo ilikuwa katika Bohari ya Forodha ya uangalizi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania ikiwa imehifadhiwa kusubiri kukamilishwa kwa utaratibu wa kodi, vibali vya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na vibali vya Bodi ya Sukari na hatimaye kuweza kuruhusiwa kutoka.

Sukari hiyo kwa sasa imeruhusiwa kutolewa ambapo mtembezi.com imefika katika bohari hiyo na kushuhudia ikipakuliwa tayari kusambazwa nchini.

RAIS MAGUFULI AGOMEA MUALIKO NCHINI UINGEREZA

Rais John Magufuli amepata heshima ya pekee kualikwa na waziri mkuu wa Uingereza katika mkutano utakaofanyika kuzungumzia mikakati ya mapambano ya rushwa ikiwa ni nchi mbili tu zimepata fursa hiyo kwa bara la Africa ikiwemo pia Nigeria.

Lakini Rais wetu amedai sasahivi amebanwa na majukumu kwahiyo atawakilishwa na Waziri mkuu mh. Kassim Majaliwa

RAIS MAGUFULI AWARUKA FUTI 100 MATAJIRI

Baada ya

sarakasi zilizokuwa zikipigwa na watia nia wa urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka jana na hatimaye kubaki na tano bora iliyopitishwa na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CC) na Mkutano

Mgombea Urais aliyepeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu Dk. John Pombe Magufuli lilipatikana.

kuzisaka

ya

Vita

katika uchaguzi

mbwembwe

kampeni kati ya aliyekuwa Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) chini ya mwavuli wa Ukawa,

aliyekuwa Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Magufuli

kupelekea

na

Uchaguzi

Magufuli kuwa mshindi Oktoba 29 na kuapishwa

kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hivi karibuni

amenukuliwa

vya Habari

itaendelea kutetea na kusimamia haki za wanyonge kwani anaamini wao ndio waliomchagua kwa kura nyingi kuliko matajiri katika kinyang’anyiro cha urais Oktoba mwaka jana

Mkuu.

Akasema

ilichaguliwa na masikini; kama matajiri walifikiri nitakuwa

wamenoa.

masikini na nitawatumikia masikini na si matajiri”.

JINAMIZI LA SELFIE NA MADHARA YAKE KWENYE MAISHA

Mwanamziki kutoka nchini DRC Congo “Koffie Olomide” hivi kaaribuni alirudi kwenye muziki baada ya kimya kikubwa na ujio wake ulikubalika kutokana na Nyimbo aliyorudi nayo kukubalika na mashabiki zake, wimbo huo unaojulikana kwa jina la “selfie” umekuwa gumzo karibu dunia nzima. Lakini tofauti na hiyo nyimbo neno hilo la selfie linamaana nyingine katika matumizi ya simu ambayo kwa sasa kwa asilimia kubwa yamekuwa yakisababisha ajali na kupoteza maisha.

Baadhi ya watu ambao asilimia kubwa ni vijana wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na matumizi maabaya ya simu wakati wakiwa wanatumia njia za uchukuzi na hii kupelekea vijana wengi kufariki kwasababu asilimia kubwa ya watumiaji wa simu ni vijana.

Nchini India mjini Pathakot imekuwa tofauti baada ya kijana wa miaka kumi na tano (15) kufariki dunia baada ya kujipiga risasi baada ya kutaka kupiga picha “selfie” akiwa amejielekezea bastora ambayo kwa Bahati mbaya alijifyatulia risasi, jitihada za kuokoa maisha yake ziligonga kwamba baada kufariki akiwa njiani akipelekwa hospitali.

Nchini India imewahi kutokea tena ajali ambayo kijana mmoja aligongwa na treni wakati alipokuwa anatumia simu akiwa kati kati ya reli na hali hiyo kupelekea kifo chake, kumekuwa na matokeo haya mara nyingi hapa nchini Tanzania iliwahi kutokea msichana kugongwa na treni kwa kutokuweza kusikia honi ya Treni alipokuwa akivuka kwenye reli huku ameweka hear phone zenye sauti ya juu

Tunashauriwa kuwa makini na matumizi ya simu zetu na haswa tukiwa sehemu za barabarani haswa watembea kwa miguu sio vizuri kusikiliza mziki wa sauti kubwa hiyo itatusaidia kusikia tahadhari yoyote tukiwa barabarani na sehemu yoyote inayotumiwa na vyombo vya moto.

NJIA MBILI PEKEE UTAKAZOTUMIA KUKATA TIKETI ZA MABASI YAENDAYO KASI

Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wanaonekana kurejesha matumaini yao kuhusu kumalizika kwa adha ya usafiri jijini humo, hii ni kutokana na kukamilika kwa mradi wa mabasi yaendayo haraka ambapo jana zilitangazwa nauli za mabasi hayo, na hii leo mabasi hayo yameanza majaribio kwa kubeba abiria kwa muda wa siku mbili bure wakati akisubiriwa Rais Magufuli kuuzindua mradi huo rasmi Alhamisi wiki hii.

JINSI YA KUKATA TIKETI ZA MABASI HAYO

Kutakuwa na mifumo miwili ya ukataji tiketi, mfumo wa kwanza ni ule uliozoeleka wa tiketi za karatasi ambazo unakata ukiwa katika kituo cha mabasi hayo, na wapili ni ule wa kutumia KADI MAALUMU, Huu ni mfumo ambao abiria atapatiwa kadi na kujaza salio kwenye kadi hiyo kupitia mawakala watakaotangazwa kwa kuweka kiwango cha nauli ambayo ataweza kuitumia ndani ya wiki au mwezi mzima.

Baada ya hapo abiria atakapofika kituoni atalizimika kuipitisha juu ya mashine maalumu zilizopo kituoni hapo, kwa ajili ya makato ya nauli na ndipo mlango utajifungua kumruhusu abiria kuingia kwenye sehemu ya kusubiria usafiri huo.

KINACHOENDELEA SAKATA LA KUONDOLEWA WAMACHINGA

Hatimaye mgogoro uliokuwepo katika ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Isaya Mnguruni na Baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo, kufuatia taarifa aliyoitoa Mkurugenzi huyo juu ya kuwataka Machinga wanaofanya biashara zao katika Soko la Kariakoo kwenda maeneo rasmi waliyopangiwa ikiwemo Ukonga, Kivule, Tabata Muslim na Kigogo Fresh umepatiwa ufumbuzi.

Hivyo mgogoro huo umefikia tamati baada ya madai waliyokuwa wanadai Baraza la Madiwani kuwa maeneo hayo yalikuwa hayana miundombinu stahiki hivyo Manispaa kupitia Mkurugenzi Mnguruni imeahidi kuyatafutia ufumbuzi na inaendelea na jitihada hizo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini hapa, Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko amesema madiwani kwa kauli moja wameridhia hatua ya Mkurugenzi huyo mara baada ya kuhaidi kutatua changamoto ambazo zilizowapelekea kupinga tamko la Mkurugugenzi, ikiwemo huduma ya choo na maji.

Pia ameongeza Machinga wanatakiwa kuondoka kwenye maeneo hayo haraka mpaka kufikia siku ya Jumamosi ili kupisha mradi wa Mabasi yaendayo Kasi (DART) ambao unatarijia kuanza hivi karibuni.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mnguruni amewapongeza madiwani hao kuungana kwa pamoja katika masuala ya maendeleo huku akiwahadi kutatua changomoto zilizobakia ambao zilikuwa tatizo kwa madiwani hao.

OMMY DIMPOZ ATOA YA MOYONI KUHUSU MAHUSIANO YAKE

Wakati mwingine unaweza kufunguka juu ya hisia zako kwa mtu fulani ingawa wakati mwingine zinaweza kuathiri jamii; pamoja na kwamba mtu hakatazwi kueleza juu ya hisia zake hata kama jamii itatafsiri kwa upande hasi ama chanya. Unataka kujua Star wa Achia Body Ommy Dimpozy amesemaje?

DIMPOZY AELEZA HISIA ZAKE

Ommy Dimpoz amesema kuwa hapendi ku “date” na wanawake maarufu kwa kuwa hakuna siri baina yenu hivyo anaepuka kuwa katika uhusiano na mtu maarufu, amesema kuwa kama asingekuwa maarufu angependa ‘ku-date’ na Star wa Bongo Movie Wema Sepetu.

“Ukidate na mtu maarufu there is no privacy maana unaishi kwa filling za kuridhisha marafiki wa girl friend wako, kama asingekuwa star ningetamani kudate na Wema” ameongeza Ommy Dimpozy

Ommy Dimpozy hivi karibuni amemtambulisha msanii kutoka katika Label ya PKP anayefahamika kwa jina la Nedy Music

SABABU ILIYO MFANYA DIAMOND PLUTNUMZ KUFANYA NGOMA YA MAKE ME SING

Kwa sasa ukitaja Bongo Fleva hutoacha kutaja jina la nyota wa muziki huo Diamond Platnumz kisha wengine wakafuata, hii ni kutokana na juhudi pamoja na kazi nzuri alizofanya Chibu Dangote kama anavyopenda kujiita Simbaaa. Platnumz ni Mtanzania wa kwanza kuwa na followers milioni moja pia Mwafrika wa kwanza kwa upande wa wasanii kuwa na followers wengi kwa sasa ana watu wanaomfuata katika mtandao wa Instagram milioni mbili na laki moja amemshinda hadi Ne – Yo mwenye “followers” milion 1.7; hili pia ni kipimo tosha cha kuangaliwa nani anafuatiliwa zaidi hapa Afrika.

KUHUSU NGOMA YA “MAKE ME SING”

Star huyo ambaye amedumu katika gemu ya muziki kwa miaka 7 hivi sasa amesema nyimbo yake ya Make Me Sing aliyoimba na msanii A.K.A kutoa Afrika Kusini ilifanyika pindi msanii huyo alipokuja katika “Zari White Party” iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City mwaka jana.

“Sababu ya kufanya nyimbo hii hatukuwahi kufanya nyimbo kali kati yangu na A.K.A, pia kipenzi changu Zari alipoisikia aliipenda sana na shemeji zangu kutoka Uganda wanapenda nyimbo zile ndio maana nimekaza sana katika nyimbo ile” amesema Diamond.

Diamond amezishukuru ‘media’ zote kwa kutoa ushirikiano katika ngoma hiyo kwani hakuisambaza lakini imefanya vizuri katika game ya Bongo Fleva na duniani kote