Hatimaye mgogoro uliokuwepo katika ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Isaya Mnguruni na Baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo, kufuatia taarifa aliyoitoa Mkurugenzi huyo juu ya kuwataka Machinga wanaofanya biashara zao katika Soko la Kariakoo kwenda maeneo rasmi waliyopangiwa ikiwemo Ukonga, Kivule, Tabata Muslim na Kigogo Fresh umepatiwa ufumbuzi.
Hivyo mgogoro huo umefikia tamati baada ya madai waliyokuwa wanadai Baraza la Madiwani kuwa maeneo hayo yalikuwa hayana miundombinu stahiki hivyo Manispaa kupitia Mkurugenzi Mnguruni imeahidi kuyatafutia ufumbuzi na inaendelea na jitihada hizo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini hapa, Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko amesema madiwani kwa kauli moja wameridhia hatua ya Mkurugenzi huyo mara baada ya kuhaidi kutatua changamoto ambazo zilizowapelekea kupinga tamko la Mkurugugenzi, ikiwemo huduma ya choo na maji.
Pia ameongeza Machinga wanatakiwa kuondoka kwenye maeneo hayo haraka mpaka kufikia siku ya Jumamosi ili kupisha mradi wa Mabasi yaendayo Kasi (DART) ambao unatarijia kuanza hivi karibuni.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mnguruni amewapongeza madiwani hao kuungana kwa pamoja katika masuala ya maendeleo huku akiwahadi kutatua changomoto zilizobakia ambao zilikuwa tatizo kwa madiwani hao.
No comments:
Post a Comment