May 10, 2016

NJIA MBILI PEKEE UTAKAZOTUMIA KUKATA TIKETI ZA MABASI YAENDAYO KASI

Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wanaonekana kurejesha matumaini yao kuhusu kumalizika kwa adha ya usafiri jijini humo, hii ni kutokana na kukamilika kwa mradi wa mabasi yaendayo haraka ambapo jana zilitangazwa nauli za mabasi hayo, na hii leo mabasi hayo yameanza majaribio kwa kubeba abiria kwa muda wa siku mbili bure wakati akisubiriwa Rais Magufuli kuuzindua mradi huo rasmi Alhamisi wiki hii.

JINSI YA KUKATA TIKETI ZA MABASI HAYO

Kutakuwa na mifumo miwili ya ukataji tiketi, mfumo wa kwanza ni ule uliozoeleka wa tiketi za karatasi ambazo unakata ukiwa katika kituo cha mabasi hayo, na wapili ni ule wa kutumia KADI MAALUMU, Huu ni mfumo ambao abiria atapatiwa kadi na kujaza salio kwenye kadi hiyo kupitia mawakala watakaotangazwa kwa kuweka kiwango cha nauli ambayo ataweza kuitumia ndani ya wiki au mwezi mzima.

Baada ya hapo abiria atakapofika kituoni atalizimika kuipitisha juu ya mashine maalumu zilizopo kituoni hapo, kwa ajili ya makato ya nauli na ndipo mlango utajifungua kumruhusu abiria kuingia kwenye sehemu ya kusubiria usafiri huo.

No comments: