Huduma ya ujasusi ya Marekani imeanzisha uchunguzi baada ya aliyekuwa muhudumu mkuu wa nyumbani kwa Donald Trump kutaka raisBarrack Obama auawe.Anthony Senecal aliandika katika mtandao wake wa Facebook kwamba Obama angechukuliwa na jeshi na kupigwa risasi kwa kuwa adui katika muhula wake wa kwanza.Bwana Senecal alimfanyia kazi bwana Trump,mgombea wa urais kupitia chama cha Republican kwa takriban miaka 30.Kampeni ya Trump hatahivyo ilijiepusha na matamshi ya Senecal.''Hakuajiriwa na Trump na hajaajiriwa tangu mwezi Juni 2009'', alisema msemaji wa kampeni ya Trump Hope Hicks katika taarifa.''Tunashtumu matamshi haya machafu kutoka kwa Senecal.Chapisho hilo la Bwana Senecal halikuwa hadharani.Na baadaye siku ya Alhamisi, bwana Senecal mwenye umri wa miaka 84 alikiambia chombo cha habari cha CNN kwamba Obama anafaa kunyongwa nje ya Ikulu ya White House.Pia aliitaja Ikulu ya White House kuwa ''msikiti mweupe''.
May 13, 2016
BOKO HARAM LINKS TO (IS) ALARM (UN)
The UN Security Council has said it is alarmed by ties between Nigeria's Boko Haram Islamist militants and the Islamic State (IS) group.
In a statement, it said Boko Haram - which pledged allegiance to IS in 2015 - continued to "undermine the peace and stability" in West and Central Africa.
Meanwhile, a senior US official said there were reports of Boko Haram fighters joining IS in Libya.
Nigeria is to host a summit on Saturday on fighting Boko Haram.
President Muhammadu Buhari will welcome counterparts from Benin, Cameroon, Chad and Niger for the gathering in Abuja, along with French President Francois Hollande, UK Foreign Secretary Philip Hammond and US Deputy Secretary of State Antony Blinken.
'More contacts'
In the statement, the 15-member UN Security Council expressed "alarm at Boko Haram's linkages with the Islamic State".
It also voiced its support for Nigerian President Muhammadu Buhari's "crucial initiative" to hold the security summit in Abuja.
Meanwhile, Mr Blinken - who is already in Nigeria - said he was concerned by reports that Boko Haram militants were going to Libya, where IS influence has grown in recent months.
"We've seen that Boko Haram's ability to communicate has become more effective," he said.
"They seem to have benefited from assistance from Daesh [IS]."
Mr Blinken added: "So these are all elements that suggests that there are more contacts and more co-operation, and this is again something that we are looking at very carefully because we want to cut it off."
At the same time, he declined to comment on whether the US would agree to a Nigerian request to sell it American war planes to fight Boko Haram.
WATOTO WALIWA NA FUNZA BABA YAO ADAI NI DHAMBI KUUA KIUMBE CHOCHOTE
WAUMINI wa Kanisa la Holy Ghost Tebernacle katika Kaunti ya Murang’aAlhamisi walimvamia mshirika mwenzao waliyemshitumu kwa kuwatesa watoto wake na uvamizi wafunza kwa 'kukataa' kuwatafutia huduma za kimatibabu.Washirika hao kutoka eneo la Kiamaihwa katika Kaunti ndogo ya Kigumo walidai kuwa muumini huyo wa kiume alikuwa akitii itikadi kali ambazo hupinga mauaji ya kiumbe chochote kilicho hai, wakiitaja kama “iliyopitwa na wakati”.Pasta Joseph Mwaura wa Kanisa hiloaliambia Swahilihub kwa njia ya simu kuwa “watoto wawili wa muumini huyo wake walikuwa wamevamiwa nafunza kila sehemu ya mwili na wakitembea ungedhani walikuwa wakicheza mchezo wa kuigiza uliohitaji wahusika kutembea kana kwamba wanacheza densi na kujikunakuna!”“Baada ya kupata habari hizo, waumini wenzangu wakiwa zaidi ya 100 walimvamia muumini huyo alipowakataza kutekeleza uokoaji huo wa watoto wake na kisha wakamwamurisha awatoe watoto hao nje watolewe funza,” akasema.Alisema kuwa watoto hao wote wakiwa ni wa kiume wa kati ya miaka 10 na 13 walikuwa wamevamiwa na wadudu hao na ikabainika kuwa hata hawakuwa wakienda shule.“Waumini hao walikataa katakata kumsikiza baba watoto hao akisema kuwa walikuwa wakimtakia laana kutoka kwa Maulana ikiwa angewakubalia waue funza hao!"Aliongeza kuwa aliteta vikali kuwa imani yake haingemruhusu kuua kiumbe yeyote aliyeumbwa na Mungu, akiongeza kuwa funza hao walikuwa wametumwa kukaa katika 'hekalu' - yaani miili ya wanawe.Funza kutumwa“Alituambia kuwa wadudu hao wametumwa ndani ya miili ya watoto wake na hakuna vile angeweza kupingana na tukio la kiroho. Alishikilia kuwa Mungu angewaamrisha watoke kutoka miili ya wanake atakapoamua kufanya hivyo,” akasema Pasta Mwaura.Baba huyo alidaiwa kubishana kuwa imani ya waumini hao waliomvamia kwake ilifaa kuwa ya kulisha watu kiroho wala sio kutibu magonjwa au kutekeleza uokoaji wa watu kutoka naukarimu wao kwa viumbe wa Mungu.“Alitulaumu kwa kupotosha waumini kuwa madawa ya kizungu ni suluhu kwa magonjwa, akiyataja kama uchawi wa Kizungu!,” akateta Pasta Mwaura.Aidha, bwana huyo alisisitiza kuwa hakuna mahali ndani ya Biblia ambapo Yesu alionekana akitafuta matibabu hospitalini.Hata hivyo, ubishi wake haukumfaa kwa lolote kwa kuwa waumini hao walifanikiwa kuwaokoa watoto hao ambapo waliwatoa funza hao na hatimaye wakapakwa dawa ya kutibu vidonda.“Aidha, waokoaji hao waliwapeleka watoto hao hadi hospitalini kwa matibabu zaidi ambapo walipewa dawa zaidi ya kupulizia nyumba yaoili kuuwa wadudu wanaosababisha uvamizi wa funza,” akasema pasta Mwaura.Alisema kuwa kuanzia Jumatatu ijayowatoto hao watasajiliwa shuleni na ambapo wamemuomba chifu wa eneo hilo kumwandama baba huyo ili atimize hilo.“Wakati umefika kwa waumini wa Kikristo kutupilia mbali itikadi ambazo zimewasababishia ujinga, magonjwa na umasikini,” akasema.ULIMWENGU WA PILI BADO UNASUMBULIWA NA FUNZA KWELI!!!ONLY IN KENYA