Apr 29, 2016

JINSI YA KUTOKA KIMAISHA UKIWA NA MSHAHARA MDOGO

Karibu Mpenzi msomaji wa BUKUKU TZ nakukaribisha tena kwenye blog hii yenye mbinu na ushauri wa changamoto zinazotuzuia kufikia mafanikio katika maisha yetu.

Maisha yetu yamejaa changamoto nyingi na unapokuwa kati kati ya changamoto ni vigumu sana kuona njia sahihi.
Hii ni kwa sababu matatizo yanakuwa yamekusonga sana na huwezi kufikiria kwa makini huku ukiwa umeyaweka matatizo hayo pembeni kwa muda.

Ndio maana niliona umuhimu huu wa kuwa na blog hii yenye mbinu na ushauri kwaajili ya kutusaidia kujikwamua katika changamoto zinazotuzuia kufikia mafanikio.

Leo tutajadili changamoto ya kipato. Hii ni changamoto inayowakabili watu wengi sana, hasa katika zama hizi ambazo ajira zimekuwa na matatizo mengi.
Kipato cha mshahara kimekuwa ni tatizo sana, karibu kila mfanyakazi mshahara anaopata haumtoshi, hii inatokana na gharama za maisha kwenda juu kwa kasi huku mshahara kuenda juu taratibu sana.

Pia watu wengi sana wanaanza kazi kwa mshahara ambao ni kidogo sana.
Leo hii kuna wahitimu wa vyuo vikuu wengi ambao wanalipwa mshahara mdogo sana ukilinganisha na viwango vyao vya elimu.

Swali ni je unawezaje kutoka kimaisha kwa kuanza kazi ambayo ina mashahara kidogo?

Kabla ya yote kuna mtu aliwahi kuniuliza swali hili kwa njia ya sms

nimepata kazi lakini mshahara naotakiwa kulipwa ni 250000 kwa mwezi je mshahara huu unaweza kunipa maendeleo ikiwemo kujenga nyumba na hata kununua gari?.naomba mchango wako wa mawazo tafadhali.

Najua hali hii inawatokea wengi, sasa swali la msingi kabisa kabla hatujaangalia ni nini cha kufanya ni je inawezekana kutoka kimaisah kwa kuanzia na mshahara kidogo? Jibu ni ndio inawezekana.

Baada ya kukubali kwamba inawezekana, (yaani kubali wewe kwamba inawezekana ili haya yanayofuata hapa chini yawe na maana kwako) sasa tuangalie ni jinsi gani ambavyo unaweza kutoka kimaisha kwa mshahara kidogo.

1.Weka malengo ya maisha yako.

Hatua ya kwanza na ya muhimu kabisa ni kuweka malengo na mipango ya maisha yako.
Kumbuka kwamba kazi hii yenye mshahara kidogo sio mwisho wa maisha yako, bali ni hatua tu unayopitia kufikia ndoto zako kwenye maisha.
Hivyo weka malengo ya kazi au biashara gani utataka kufanya baadae, malengo ya maisha yako na kila eneo muhimu kwenye maisha yako. Kujua jinsi unavyoweza kuweka malengo ambayo utayafikia bonyeza maandishi haya na usome makala za malengo. 

2.Kubali kwamba kipato chako ni kidogo na anza kwakuishi maisha hayo.

Hatua ya pili na muhimu sana kwako ni kukubali kwamba kwa sasa unapata kipato kidogo na ukishakubali kipato hiko kubali kuishi maisha yanayoendana na kipato hiko kwa siku hizi za mwanzoni.
Usitake kuanz akujionesha na wewe upo, uanze kumiliki siku za bei kali, kuhudhuria sehemu za gharama na vitu kama hivyo. Haya yote yatakuja baadae ukishaweka sawa kipato chako, ila mwanzo huu unahitaji kujibana ili kujenga msingi wako wa kipato.
Ishi kwa kwa kupata huduma zile za msingi kabisa, kitu chochote ambacho usipokuwa nacho hutakufa, au maisha yako hayatakuwa hovyo sana, basi kwa sasa usiwe nacho.
Dhibiti matumizi yako kwa kiasi kikubwa sana ili uweze kujipanga vizuri kwa ajili ya baadae.

3.Anza kuweka akiba kwenye mshahara wako wa kwanza.

Baada ya kudhibiti matumizi yako kwa kiasi kikubwa sana anza kuweka akiba haraka sana, usisubiri chochote, hakuna mabadiliko makubwa yatakayotokea hapo ulipo. Anza kwa kuweka akiba asilimia 20 ya kipato chako, ila nakusisitiza weka zaidi ya hapo.
Na katika hatua hii ya kuweka akiba, weka akiba kwanz andio ufanye matumizi, na sio kufanya matumizi halafu ndio uweke akiba. Weka akiba huku ukiangalia malengo uliyojiwekea ili ujue kama utawez akuyafikia.

4.Angalia fursa nyingine zinazopatikana kwenye kazi yako na hata kwenye maisha yako.

Kazi yoyote, namaanisha kazi yoyote ile ina fursa nyingi ambazo huwa hazionekani kwa wote.
Bali wale wenye kiu kali ya mafanikio ndio huona fursa hizi na kuzitumia vizuri. Angalia ni jinsi gani unaweza kutumia nafasi zinazopatikana kwenye kazi yako kuongez akipato zaidi. Angalia ni changamoto gani ambazo watu wanapitia kwenye kazi hiyo na jinsi gani unaweza kusaidia kuzitatua na kujiongezea kipato. Usikae tu kwenye kazi hiyo na kuidharau kwa sababu inakulipa kidogo. Ifuatilie vizuri kazi hiyo, angalia kila fursa unayoweza kuiibua na kuitumia vizuri.
Pia kuwa na moyo wa kufanya majukumu ya ziada, maliza kazi zako mapema na chukua majukumu mengine yatakayokuwa yanapatikana, hii itakufanya uongeze thamani yako na hata kuongez akipato chako.

Pia angalia fursa nyingine za kazi au biashara nje ya kazi yako hiyo. Kwa kazi yenye mshahara kidogo mara nyingi huwa haikubani sana hivyo hata kama unafanya kazi masaa kumi kwa siku bado una masaa mengine kumi na nne, ukitoa hapo masaa sita ya kulala unaweza kupata muda wa kujishughulisha na biashara nyingine.
Kumbuka wewe sasa hivi upo kwenye wakati mgumu kutokana na kipato chako, sasa kama unataka utoke kazini uende ukapige story au kuangalia tv au kufanya chochote kwa madai kwamba unajipumzisha utaendelea kubaki hapo ulipo.
Jitoe kwa muda huu kufanya kazi sana na kuangalia kila fursa itakayojitokeza mbele yako.

5.Jifunze kila siku.

Moja ya sababu zinazowafanya watu kufia kwenye kazi zenye mishahara midogo ni kuridhika na mishahara hiyo kiakili na uvivu wa kujifunza. Sasa ndigu yangu wewe huna anasa hiyo.
Tumia kila muda ulionao kujifunza, jifunze ujuzi wa ziada, jifunze kuhusu biashara, jifunze kuhusu maendeleao binafsi.
Katika kazi yako angalia ni eneo gani ambalo lina mahitaji ya wafanyakazi ila bado halijapata wafanyakazi wa zuri. Anza kujifunza kitu hiko, soma vitabu vinavyohusiana na eneo hili, angalia video kwenye mtandao zinazoelekeza kuhusiana na kazi hiyo.
Tembelea mitandao mbali mbali na pia ongea na watu waliobobea kwenye eneo hilo. Ukishaanza kupata mwanga omba kujitolea kusaidia kazi kwenye eneo hilo, hata ukinyimwa endelea kuomba na shawishi kwamba una kitu unaweza kuchangia.
Ukipewa nafasi onesha sasa uwezo wako mkubwa, fanya ka viwango vizuri sana. Kama ukiwez akufanya hivi nakuhakikishia kwamba hakuna mtu atakayekubali kukupoteza na thamani yako itakua kwa kasi sana.

Hizi ndio hatua tano ninazokushauri uanze kuzifuata leo ili kuweza kutoka kimaisha kwa kuanzia na mshahara kidogo. Kumbuka kila mtu analipwa kulingana na thamani anayopeleka sokoni.
Hivyo kama ukiweza kumpatia mwajiri wako thamani kubwa hatakuwa na budi bali kuhakikisha hakupoteze na hapo thamani yako itakuw akubwa sana.
Mambo yote haya yatachukua muda kidogo, ila usikate tamaa na endeleza juhudi.

Pia nikupe angalizo kwamba wale utakaowakuta kazini ambao wanajiita waozefu watakukatisha sana tamaa utakapoanza kufuata ushauri huu.
Watakuambia sisi tumefanya kazi hii miaka kumi, unajisumbua tu bwana mdogo/bibi mdogo. Ushauri kwa watu hao, wapuuze haraka sana, sio mfano mzuri kwako kuwaiga kwa sababu kama wamefanya kazi miaka kumi na bado mshahara wao ni wa chini sana ni kipi unaweza kujifunza kwao, usiwasikilize.

MBINU ZA KUKUZA NYWELE KWA MUDA MFUPI BILA GHARAMA.

Je?
  Ndo umeanza safari yako ya kukuza nywele na nywele zako hazikui haraka kama ulivyotegemea?

  Basi inawezekana hautunzi nywele zako vizuri. Nitakuelezea njia unazoweza kutumia kukuza nywele zako haraka na kukujulisha makosa gani unayafanya yanyositisha ukuaji wa nywele zako.

MAKOSA YA SABABISHAYO NYWELE ZAKO KUTOKUKUA HARAKA;

Kosa la kwanza, watu wengi wana blow dry au wananyoosha nywele zao mara kwa mara. Mtu akifanya hivi basi, ataziua nywele zake na zitaanza kukatika wakati wa kuchana au mda wowote.

  Basi inabidi upunguze kutumia vifaa kama hivi ili nywele zako zikue ( Hata kama umepaka dawa).

Pili, tunavyoziachia nywele na kuzistyle kusuka rasta, nywele za kawaida au kushonea weaving zinakubalika, ila ukizichana na kuzisbana nywele basi hapo inaweza kuziharibu au kuzikata nywele.

Pia, kutokukata ncha baada ya mda, ncha zinaweza kuanza kuchanika na inabidi uzikate ili nywele zikue vizuri kwasababu ncha huchangia kwenye kusitisha ukuaji wa nywele na kukata nywele. Unaweza kukata incha1-2 au cm 2-2.5 baada ya miezi mitatu au minne.

MBINU ZA KUKUZA NYWELE HARAKA;

Kwanza, inabidi uzisuke nywele zako mara kwa mara ilizisiharibike au zisikatike. Hivi utaweza hata kuzuia ncha zilizoharibika.
 
Kama hujisikii kusuka nywele au kushonea weaving basi unaweza kuzibana kwa juu au kuzifunga na kitambaa ila ni lazima kitambaa kiwe cha silk ili nywele zako zisiharibike ( unaweza kukitumia hata wakati wa kulala).

Pili, inabidi upake mafuta kwenye kichwa chako mara kwa mara, sana sana unapojisikia kama kichwa kimekauka au kama kinawasha. Mafuta mazuri kutumia kwaaji ya ukuaji wa nywele ni mafuta ya nazi, castor, Moroccan, Jamaican au lavender. Ila hata mafuta mengine yeyote unayotumia ilayasiwe ya mgando.

Pia, usizioshe nywele na shampu mara kwa mara kwasababu shampoo inaondoa mafuta kwenye kichwa na nywele zako.

Basi, inabidi uoshe nywele na conditioner kama unaona nywele zako sio chafu sana, ila kama unaonanywele zako ni chafu basi osha na shampuu.

Itakuwa bora ukipaka mafuta kabla ujaosha nywele na shampu na uoshe nywele zako kila baada ya wiki moja na kama zinakatika basi, osha baada ya wiki mbili au tatu.

Kula vyakula vingi vyenye protini kama kuku, mtindi, maharagwe au nyama yoyote.

Apr 26, 2016

KUJUA KAMA SIMU YAKO NI ORIGINAL AU FEKI

Kabla hujanununa simu mpya hakikisha unaandikanamba hii *#06# , itaonyesha namba ya pekee (serialnumber ) au IMEI (International Mobile EquipmentIdentity) namba ambayo ni lazima ziwe namba 15 au zaidi, na nilazima ianze na namba 35.

1. Sasa angalia kwa makini kama namba unazoziona zinafanana moja kwa moja na namba zilizoandikwa katika simu sehemu ambayo betri inakaa (battery base). Namba hizi zinapaswa kufanana kwa simu ambayo ni origino.

2. Simu yaweza kuwa origino lakini katika viwango nya ubora(qualities) tofauti . Sasa tunaanza kuchambua IMEI ili kujua ubora. Katika namba hizo namba ya saba(7) nay a name(8) ndizo zinazohakikishaubora wa simu yako.

• Kama namba ya saba nay a nane ni 00 inamaana kuwa simu yako imetengenizwa kwa ubora wa juu kabisa katika viwanda vya kuaminika.

• Kama namba ya saba na y a nane ni 01 au 10 inamaana sumu yako imetengeneza Finland na inaubora wa juu pia.

• Kama namba ya saba na y a nane ni 13 inamaanasimu yako imeunganishwa katika nchi ya Azerbaijan na ni hatari sana kwa matumizi na afya yako.

• kama namba ya saba na ya nane ni 02 au 20 inamaana simu yako imeunganishwa katika nchi ya Emirates hivyo ina kiwango cha chini sana.

• Kama namba ya saba nay a nane ni kati ya 03 au 30 au 04 au 40 inamaana simu yako imetengenezwa China lakini ina ubora mzuri ila haijafikia zile zenye 00 , 01 au 10.

• Kama namba ya saba nay a nane ni 05 au 50 inamaana simu yako imatengenezwa labda Brazil ama USA ama Finland.

• Kama namba ya saba na ya nane ni 06 au 60 simu yako imetengenezwa Hong Hong, China au Mexico.

• Kama namba ya saba nay a nane ni 08 au 80 simu yako imetengenezwa Germany na ina ubora wa kawaida.Unaweza pia kuangalia simu uliyonayo sasa kujua kama unatumia simu origino au feki na yenye kiwango gani.Utafiti huu unatoka katika nyanzo nya kuaminika na kama una swali au maoni tafadhali andika comment hapa chini tutakujibu haraka iwezekanavyo

JINSI YA KUPATA MTAJI NA NAMNA YA KUTUMIA MTAJI KATIKA BIASHARA MTAJI


Mtaji ni kitu chochote ambacho unaweza kutumia katika kuzalisha kitu kingine kwa lengo la kupata faida.Biashara oyote iwayo lazima ianze na mtaji. Kuna aina tano za mitaji kama ifuatavyo:-

1. Mtaji wa fedha( financial capital)

2. binadamu mwenyewe( human capital) vitu kama ujuzi, elimu na kufanya kazi kwa bidii.

3. Jamii ( social network capital) ushirikiano na watu wengine katika biashara

4. utamaduni halisi wa mjasiliamali- utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii,historia ya familia

5. fani au utaalamu  katika jambo flani

JINSI YA KUPATA MTAJI.
hapa tunaangalia vyanzo vya mtaji kwa mjasiliamali. Wajasiliamali wengi wanapata changamoto kubwa katika kupata mitaji ya kuanzishia biashara. nivigumu kuanzisha biashara bila kuwa na mtaji wa kutosha,hivyo basi mtaji ni muhimu sana lakini mtaji pekeyake hautoshi kuanzisha biashara ni lazima uwe na elimu ya ujasiliamali ili uweze kufanikiwa katika biashara. kuna njia mbalimbali za kupata mtaji na njia hizo zimegawanyika katika mafungu mawili ambayo ni chanzo cha ndani na chanzo cha nje.
Chanzo cha ndani ( internal sources of capital)
1. Mtaji   toka kwa mjasiliamali mwenyewe. huu ni mtaji ambao mjasiliamali anakuwanao kabla hajaanza biashara. huu ni mtaji bora sana kwani humilikiwa na mjasiliamali mwenyewe na hatakiwi kurudisha rejesho hata baada ya kupata faida.

2. Mtaji ambao unapatikana wakati biashara injiendesha. faida inayopatikana katika biashara inaweza kutumika kama mtaji. njia hii ndio huchangia kukua kwa biashara.

3. hisa. baadhi yawajasiliamali wanaweza kuamua kuwekeza katika hisa za makampuni. uwekezaji katika hisa husaidia kupata mtaji pale ambapo kampuni litagawa faida kwa wanachama waliowekeza katika hisa. pia mjasiliamali anaweza kupata mtaji kwa kuuza hisa kwa mtu mwingine au muwekezaji wa nje.

chanzo cha nje ( external sources of capital)
hapa tunaangalia mtajia ambao mjasiliamali anaweza kuupata toka nje ya yeye mwenyewe. baadhi ya vyanzo    hivyo ni kama ifuatavyo.

1. mkopo toka benki
huu ni mkopo ambao ulipaji wake ni wa muda mrefu.viwango vyariba si vikubwa sana ambavyo mjasiliamali anaweza kumudu kulipa endapo biashara itafanikiwa. mikopo ya benki inahitaji dhamana ya vitu visivyo hamishika mfano nyumba, shamba nk. 

Apr 23, 2016

JINSI YA KUIFANYA SIMU YAKO IWEZE KUKAA NA CHAJI KWA MUDA MREFU.

Namna ya kuifanya simu yako idumu na chaji muda mrefu.
Ujio wa matumizi ya simu za kisasa maarufu kwa jina la Smartphone umewafanya Watanzania wengi kuzinunua,kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa mawasiliano.Simu hizi ni sawa na kuwa na kompyuta ya kawaida iliyounganishwa na mtandao wa intaneti. Kwa mfano, simu hizi zinakupa nafasi kubwa ya mawasiliano kupitia mitandao ya kijamii ya WhatsApp, Facebook, Skype, Viber, Kik Messenger, Twetter, WeChat, LinkedIn, Badoo, Instagram na Twoo.Pia simu za kisasa zina huduma mbalimbali zikiwamo za kujua jiografia ya maeneo, vipimo vya joto, mapigo ya moyo,upigaji wa picha na huduma nyinginezo. Kwa kutumia mitandao ya kijamii watu sasa hawana sababu ya kujisika wapweke, kwani hata ukiwa chumbani peke yako unaweza kuungana na watu duniani kwa kujadili na kupokea taarifa mbalimbali.Hivyo simu hizi zimeweza kuwakusanya watu waliotawanyika sehemu mbalimbali na kujadili mambo kama vile wamekusanyika eneo moja. Mbali na hilo, simu nyingi zina uwezo mkubwa wa kasi yamawasiliano ya intaneti, hivyo kuwa rahisi kutuma na kupokea barua pepe na kupata taarifa kutoka tovuti mbalimbali duniani. Ni kutokana na mambo hayo, simu hizi zimeonekana ndizo za kisasa na watu wengi wameamua hata kujinyima ili kuzinunua. Kasoro ya simu hizi Pamoja na watu wengi kuzipenda, simu hizi zimekuwani kero kutokana na uwezo mdogo wa betrizake kudumu na chaji au nguvu za kuziendesha. Awali watu wengi walipenda simu zinazodumu na chaji muda mrefu. Simu za kisasa zina udhaifu wa kushindwa kudumu na chaji. Nyingi zinatumika kwa saa sita hadi 12. Kwa sababu hii watumiaji wengi wameamua kununua vifaa vya kuhifadhia umeme kwa ajili ya kuzichaji. Vifaa hivi vinajulikana kwa jina la’ power banking’ Kinachokuonyesha kuwa uwezo unapungua ni pale unapojikuta siku za mwanzo unachaji kwa siku moja baadae mara mbili kwa siku, mara tatu na hatimaye unajikuta unachaji mara kwa mara. Kwanini simu hizi hazidumu na chaji kwa muda mrefu kama zilivyo simu nyingine? Nini kifanyike ili kutatua tatizo hili? Wataalamu wana majibu. Sababu za kuisha chaji mapema.Mmoja wa waanzilishi wa Kampuni ya Farbe Tecnik inayojihusisha na utengenezaji wa vifaa vya kuchaji simu, Shane Broesky anasema kupungua kwa uwezo wa kuhifadhi chaji kwa simu hizi ni uzembe wa watumiaji. Anasema watu wengi hudhani kuziacha simu zao zikiwa zinachajiwa usiku mzima au kwa muda mrefu ni kupunguza uwezo wa betri kuhifadhi umeme. Broesky, katika maelezoyake aliyoyatoa kupitia mtandao wa Digital Trends, anawatoa hofu wamiliki wa simu kuwa kuziacha kwenye chaji kwa muda mrefu hakuharibu simu zao. Anafafanua kuwa hii ni kwa sababu simu hizo zina mfumo mzuri wa kuzuia umeme usiendelee kuichaji betri baada ya kufikia kiwango cha juu cha asilimia 100. Broesky anasema hii inasaidia kuepusha betri kuchajiwa kupita kiasi. Lakini akasema kitendo cha kuicha kwenye mfumo wa kuchaji, kinasababisha kila betri ikipungua kidogo kutoka kiwango cha juu, ianze kuchajiwa tena. Kitendo hicho kinapojirudiarudia, anasema ndiko kunakoua uwezo wa betri hasa zile za aina ya ‘Lithium-ion’ katika kuhifadhi umeme. Anasema betri hizi zinapokuwa na kiwangocha juu cha umeme, ikichajiwa joto lake linapanda. “Kitendo cha betri kuwa kwenyehali ya joto kwa muda, ndiko kunakoharibuuwezo wake wa kudumu na umeme kwa muda mrefu,’’ anasema. Namna ya kuwezesha chaji kudumu Ili betri ya simu yako iendelee kuwa na uwezo, Broesky anasema unapaswa uichaji kwa kiwango cha kati ya asilimia 50 na 80. Ukitumia mfumo huo, utaifanya betri ya simu yako iendelee kuwa na uwezo wa juu wa kudumu na umeme kwa muda mrefu. Jambo lingine la kuifanya betri yako idumu na umeme ni kuepuka betri yako kupungua umeme hadi simu kuzima. Kampuni ya Simu ya Tecno nayo ilitoa taarifa kwenye mtandao wake kuwa mtumiaji wa simu za kisasa anapaswa kuepuka simu yake kupata moto wakati wamatumizi.Taarifa ya kampuni hiyo ambayo simu zakezinaonekana kutamba katika soko hapa nchini, inaelezea kuwa iwapo unatumia intaneti katika mazingira ya mawasiliano hafifu, simu hupata moto. Inawashauri watumiaji wa simu hizo pia wasiziache zikiwa zimefunguliwa ukurasa wa mawasiliano ya intaneti kwa sababu wakatimawasiliano yanakuwa madogo, hupata moto.

MBINU 5 ZA KUKUZA BIASHARA KWA MTAJI MDOGO

1. Jipe muda, biashara haitaweza kukua haraka kama unavyofikiri

Uzuri wa kuanza biashara na mtaji kidogo ni kwamba kila mtu anaweza kufanya hivyo. Lakini pia urahisi huu wa kuanza biashara kwa mtaji kidogo unafanya ukuaji wa biashara kuwa wa taratibu sana. Hivyo unapofanya biashara yoyote ambayo unaanza na mtaji kidogo ni muhimu ukajipa muda ili kuweza kukuza mtaji wako. Usiwe na tamaa ya kutaka kukuza biashara hii haraka, unaweza kuingia kwenye maamuzi ambayo yatakugharimu zaidi. Endelea kufanya biashara yako huku ukijifunza zaidi na kuangalia kila fursa ambayo unaweza kuitumia kukuza biashara yako.

2. Kuza mtaji wako taratibu

Kwa mtaji huo mdogo ambao umeanza nao biashara, endelea kuukuza kila siku. Usiendeshe biashara kwa kula kila kipato unachopata, badala yake tenga sehemu ya akiba irudi kwenye biashara yako. Fanya hivi kwa nidhamu ya hali ya juu sana na unahakikisha kila unapopata faida sehemu inarudi kwenye biashara yako. Pia endelea kuangalia kwa mazingira uliyonayo na kwa biashara unayofanya ni kwa jinsi gani unaweza kukuza mtaji wako zaidi. Kama utafikiria hili kila siku, hutakosa majibu ambayo yatakusaidia.

3. Punguza gharama za biashara na za maisha pia

Kuwa kwenye biashara haimaanishi kwamba ndio una uhuru wa kufanya chochote unachotaka na fedha za biashara hiyo, kwa sababu tu ni zako. Wewe sasa upo kwenye wakati mgumu wa kukuza biashara yako huku ukiwa huna njia nyingi za kufanya hivyo. Hebu kwa sasa punguza kabisa gharama zako za kibiashara na za maisha pia. Kama kitu sio muhimu sana basi usikigharamie. Punguza matumizi yote ambayo ni ya anasa tu na sio kwa ukuaji wa biashara. Katika kupunguza gharama zako za biashara na maisha, jijengee nidhamu nzuri sana ya fedha. Usitumie fedha kiholela tu, kuwa na mahesabu na sababu kwa nini umetumia fedha fulani, hasa kwa matumizi ambayo sio ya kawaida.

4. Angalia watu ambao unaweza kushirikiana nao

Baada ya kuiendesha biashara yako vizuri na ukaona inaenda kwa faida, unaweza kuangalia watu ambao unaweza kushirikiana nao kwenye biashara hiyo. Kuna watu wengi ambao wanaweza kuwa na mtaji lakini hawana muda wa kufanya biashara. Lakini pia watu hawa wanataka mtu ambaye wanaweza kumwamini. Hivyo kama unaweza kuaminika angalia watu unaoweza kushirikiana nao kibiashara. Andaa mpango mzuri ambao utamshawishi mtu ni jinsi gani yeye atafaidika kama atawekeza kiasi kidogo kwenye biashara yako. Ikiwa unaendesha biashara yako kitaalamu itakuwa rahisi zaidi kushawishi watu kushirikiana na wewe.

5. Rasimisha biashara yako ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kupata mkopo

Hata kama biashara yako ni ndogo kiasi gani, irasimishe. Iendeshe kisheria kwa kuwa na namba ya mlipa kodi na hata leseni pia. Hivi vitakuwezesha wewe kutambulika na taasisi za kifedha pale utakapohitaji msaada zaidi wa kifedha. Mkopo kwenye taasisi za kifedha ni chanzo muhimu ila usikimbilie kama bado hujaweza kuiendesha biashara yako kwa faida. Hakikisha umeiweka biashara yako vizuri kwanza na inajiendesha kwa faida ili unapochukua mkopo unajua unauweka wapi na kuendelea kupata faida zaidi. Kuikuza biashara pale ambapo umeanza na mtaji kidogo ni kitu ambacho kinawezekana. Ila unahitaji kujitoa na kujenga nidhamu kubwa. Unahitaji kufanya kazi zaidi ya wafanyabiashara wengine, unahitaji kuwa mbunifu wa hali ya juu na pia unahitaji kujijengea uaminifu. Ukishajua wewe biashara yako ni ndogo na inahitaji kukua, basi hakikisha kila mara unaumiza akili yako ifikirie njia zaidi za kuikuza. Na kama utaweza kufanya hivi basi utaziona fursa nyingi zilizokuzunguka za kuikuza biashara yako.

Apr 22, 2016

JINSI YA KUJUA JINSIA YA MTOTO ALIYE TUMBONI

 Mwanamke anapokuwa mjamzito huwa na wasi wasi na kushindwa kugundua kama ujauzito aliobeba ni mtoto wa kike au wa kiume. Kuna njia mbalimbali ambazo wakunga, wataalamu wa afya na wanawaake wazoefu huzitumia kutambua jinsia ya mtoto aliyeko tumboni ambapo mara nyingi asilimia zaidi ya 50 huwa ni kweli. Zifuatazo ni dalili na njia zinazotumika kutambua jinsia:-

1. Tumbo, wazoefu wanaamini endapo utakuwa umebeba uzito mdogo tumboni na tumbo dogo mtoto atakuwa ni wa kume.

2. Haja ndogo, endapo mama mjamzito anatoa haja ndogo rangi nyeusi kuna uwezekano mkubwa amebeba mtoto wa kiume huku nyeupe au rangi ya mawimbi ikimaanisha jinsia ya kike.

3. Chunusi, uwepo wa chunusi nyingi na mara kwa mara ni ishara kuwa umebeba mtoto wa kiume wakati ngozi kuwa laini sana kupita awali ikimaanisha ni mimba ya mtoto wa kike.

4. Maziwa, pale ziwa la kulia linapokuwa kubwa kuliko ziwa la kushoto inamaanisha mimba ni mtoto wa kiume.

5. Miguu kuwaka moto na kuwa laini ina maanisha mimba ni ya mtoto wa kike wakati miguu kuwa na mikono kuwa ya baridi ni mtoto wa kiume.

6. Mapigo ya moyo, hii hutumiwa na wataalamu wa afya ambapo mapigo chini ya 140 ni mtoto wa kiume wakati zaidi ya 140 ikimaanisha mtoto wa kike. 

7. Kutamani vyakula, mjamzito anapotamani sana vyakula vya uchachu na chumvi nyingi kuna uwezekano wa kujifungua mtoto wa kiume wakati vitamu na sukari nyingi ni mtoto wa kike.

8. Mtindo wa kulalia ubavu wa kushoto mara nyingi ni jinsia ya kiume wakati ubavu wa kulia ni mtoto wa kike.

9. Kutapika, wengine wanaamini kichefuchefu na kutapika sana nyakati za asubuhi ni ishara ya kubeba mtoto wa kike.

10. Nyingine ni kuongezeka uzito kupita kiasi ikimaanisha mtoto wa kike huku kupungua, kubaki na uzito uleule au kuongezeka uzito kiasi ni ishara kuwa ni mtoto wa kiume

11. Nywele, mwanamke anapokuwa mjamzito na nywele zikaota au kukua kwa kasi inamaanisha mtoto wa kiume wakati kinyume chake ni jinsia ya kike.

Apr 21, 2016

MAFURIKO YATIKISA DAR

Mvua zinazo endelea kunyesha jijini dar es salaam zimesababisha madhara makubwa kwa wananchi waishio na wafanyao biashara maeneo ya kariakoo Baada ya mvua hiyo kusababisha hasara kwa wafanya biashara ambao walibaki kushuhudia mali zao zikisombwa na maji yaliyo sababishwa na mvua hizo zinazo endelea kunyesha kwa kasi.
Pia katika maeneo ya barabarani kulikua na msongamano mkubwa wa magari yaliyo zimika kutokana na maji yaliyo sababishwa na mvua hizo kubwa.
Kwa upande mwingine wafanya biashara walilazimika kufunga maduka ili kuepukana na janga hilo,
tatizo kubwa linalo onekana ni swala la miundo mbinu,Wananchi wameiomba Serikali kutenga fedha ili kurekebisha miundo mbinu hiyo ambayo inaonekana kuto kaa katika hali ambayo haijitoshelezi..

Apr 20, 2016

MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI ABAKWA NA WANAFUNZI WENZAKE

Matukio ya uvunjifu wa maadili kwenye shule mbalimbali hapa nchini yameendelea kushamiri baada ya wanafunzi wanne wa Shule ya Msingi Lulanzi wilayani Kibaha mkoani Pwani kutuhumiwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili na kumsababishia maumivu yaliyopelekea kulazwa Hospitali ya Tumbi kwa matibabu.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana babu wa mtoto huyo, Jacob Mrope alisema tukio hilo lilitokea Septemba 2 saa 6 mchana ambapo mjukuu wake ambaye ni yatima alikuwa akitoka shuleni huku akiwa na wenzake wawili wakike, walikimbizwa na watuhumiwa hao ambapo yeye alishindwa kukimbia kutokana na kuumia mguu na kujikuta akibakwa.

Mrope alisema kuwa wanafunzi wenzake aliokuwa nao walisema kuwa baada ya watuhumiwa hao kumkamata walimziba mdomo kisha wakaanza kumuingilia kwa zamu ambapo mwanafunzi huyo hakuweza kupata msaada wowote hadi watuhumiwa hao kutimiza haja zao.

"Wenzake waliokuwa nao walitoa taarifa nyumbani kwa mlezi wake ambaye ni dada yake ambapo alikwenda na kumkuta akitokwa na damu nyingi na alipomuuliza alisema kuwa wenzake wamembaka ndipo alimchukua na kumpeleka shuleni kutoa taarifa," alisema Mrope.

Kwa upande wake dada yake Lwiza alisema kuwa yeye alipata taarifa kupitia kwa wanafunzi hao ambao alikuwa nao wakati wanatoka shule na kukimbizwa na watuhumiwa hao, ambapo walisema kuwa ilibidi warudi na kumkuta mwenzao akitokwa damu, wamkokota mwenzao hadi nyumba iliyojirani na kumjulisha.

"Alikuwa kwenye hali mbaya kwani alikuwa akitokwa na damu nyingi na nilipomuuliza alisema kuwa amebakwa na mtuhumiwa ambaye alimtambua na kumtaja jina mwenye umri wa miaka 10 akiwa na wenzake watatu," alisema Lwiza.

Lwiza alisema kuwa baada ya kuona hali ile walimpeleka shule na uongozi wa shule ukamwelekeza kufuata taratibu za kisheria ambapo walikwenda Serikali ya mtaa kisha kwenda polisi na baadaye Hospitali ya Tumbi kwa matibabu zaidi ambapo hadi juzi mwanafunzi huyo alikuwa bado kalazwa na hali yake inasemekana kuwa ni mbaya.

Naye Mwalimu mkuu wa shule hiyo ya Lulanzi, Anna Bilali alisema kuwa wao kama uongozi wa shule hawawezi kusema lolote kwani suala hilo liko kwenye vyombo vya sheria pamoja na kitabibu na watakuwa tayari kusema mara taarifa zitakapokamilika.

"Ni kweli tukio hili limetokea lakini bado haijathibitishwa kama ni kweli au la na pia lilitokea nje ya shule na muda wa shule kwa wanafunzi wa madarasa ya chini walisharuhusiwa kurudi nyumbani mara baada ya masomo kwisha," alisema Bilali.

Akizungumzia tukio hilo mjumbe wa mtaa wa Lulanzi, Rasul Shaban alisema kuwa walipata taarifa hiyo na kushangazwa na kitendo hicho ambapo tukio hilo ni la mara ya kwanza kutokea katika shule hiyo ambayo iko kwenye mtaa huo na pia walitoa barua za kuwadhamini wanafunzi wanaotuhumiwa kufanya tukio hilo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Ulrich Matei alisema kuwa hadi sasa wanawashikilia wanafunzi wanne wenye umri kati ya miaka 10 na 13 kuhusiana na tukio hilo.

MTOTO WA MIAKA MIWILI AMPIGA RISASI MAMA YAKE.

Mwanamke mmoja katika jimbo la Idaho nchini Marekani ameuwawa na mtoto wake wa kiume wa miaka miwili kwa kumpiga risasi baada ya kuchukua bastola kwenye pochi yake.

Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Veronica J Rutledge, mwenye umri wa miaka 29, alipigwa risasi na mtoto wake huyo kwenye duka la Wal-Mart katika mji Hayden.

Msemaji wa duka hilo amesema mwanamke huyo alikuwa anafanya manunuzi akiwa na watoto kadhaa wakati wa tukio hilo. Maafisa wamesema marehemu kibali chake cha silaha kilikuwa kimefutwa.

Apr 18, 2016

MWANAMKE AFANYA NGONO NA WANAUME 1,500

MKAZI wa kitongoji cha Chelsea, jijini London,Mare Simone(54) amefanya ngono na wanaume 1,500 katika kipindi cha miaka 23 ili kuwatibu matatizo yanayohusiana na mapenzi.

Wateja ni miongoni mwa wanaume 10,000 waliokwenda ofisini kwake kupata tiba ya matatizo hayo.
Mjasiriamali huyo anatoa ushauri wa mambo ya kimapenzi kwa wanawake na wanaume na ametamba kuwa yeye ni mtaalamu wa masuala ya kitandani.

Baada ya kuachana na mumewe, Mare aliamua kuisomea rasmi taaluma hiyo ya mapenzi na kisha kufungua ofisi na hadi sasa ametoa somo la mapenzi kwa zaidi ya wateja 10,000 waliofika kwenye ofisi yake katika kipindi cha miaka 23.
Mare amebainisha kwamba, kati ya wateja hao,hadi sasa amefanya ngono na wanaume zaidi ya 1,500 wakiwemo waume au wapenzi wa wanawake wengine.

Amesema,hadhani kuwa anafanya kosa lolote kinyume cha sheria kutembea na waume za watu kwa sababu anaboresha maisha ya mapenzi ya watu wengine,anapata riziki yake kwa kutoa tiba hiyo, na kwamba, yeye si kahaba.
"Watu wananilipa kwa ushauri ninaowalipa na kwa kutibu matatizo yao hawanilipi kwasababu ya ngono".
"Najipatia kipato changu kwa kulala na waume au wapenzi wa wanawake wengine.
Lakini mimi sifanyi ukahaba kwa kuwa taaluma ya mapenzi inaruhusiwa kisheria na mapenzi yanafanyika katika mazingira ya tiba" alisema Mare.

"Nasaidia kuimarisha na kubadilisha maisha ya kimapenzi ya maelfu ya wanaume na hivyo nakuwa nimesaidia kuimarisha maisha ya kimapenzi ya wake zao au wapenzi wao"

"Wanawake wengine wanabeba mimba za wanawake wengine kwa sababu wanataka kuwasaidia wanawake wasio na uwezo wa kupata mimba.
Hali hiyo ni sawa na mimi kwani nawasaidia watu kuwa na maisha mazuri ya kimapenzi".

Mare anaifurahia kazi yake na huwa na furaha zaidi wateja wake wanapoondoka kurudi majumbani mwao wakiwa na matumaini mapya kwenye maisha yao ya kimapenzi.

Kwa siku anatoa vipindi vitano vya masuala ya mapenzi,wateja wake ni watu wa rika mbali mbali, jinsia zote, maumbile tofauti na wafanyakazi wa vitengo tofauti tofauti.

"Wanaume mara nyingi hunifuata kwa sababu ya matatizo ya kutosimama vyema kwa uume na kufika kileleni mapema kabla ya wapenzi wao wakati wengine huambiwa waje wanione na wake zao kwakuwa hawawaridhishi kitandani".

"Kabla hawajaniona huwa wote wanapimwa magonjwa ya zinaa na lazima watumie kondomu iwapo nitalala nao" alisema Mare.

"Kwa wanawake mara nyingi hunifuata wakiwa na matatizo ya kutofika kileleni au wanapoona wapenzi wao hawajui jinsi ya kuwaridhisha kitandani".
"Huwa nawafundisha jinsi ya kujipa raha wao wenyewe na kuipenda miili yao" amesema na kusisitiza kwamba hatarajii kuacha kutoa huduma hiyo katika miaka 10 ijayo.

hapo chini ni picha ya mwanamke huyo

BABA AUA WATOTO WATANO

Mwanamume mmoja raia wa Marekani anashukiwa kuwaua watoto wake watano na kuwatupa katika jimbo jingine, hii ni kwa muujibu wa polisi nchini humo.

Timothy Ray Jones anakabiliwa na mashtaka kadhaa katika jimbo ambalo ndio makazi yake la Carolina ya kusini,kufuatia shutuma hizo na alikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita huko Mississippi .

Watoto hao watano waliopoteza uhai kwa kuuawa na baba yao walikua na umri wa kuanzia mwaka mmoja hadi miaka nane inaelezwa watoto hao watano walipotea katika mazingira ya kutatanisha , mama wa watoto hao aliporipoti polisi baada ya mawasiliano kati yake na mzazi mwenziwe kukatika.

Maafisa hao wa polisi walipofanya uchunguzi wao waligundua miili ya watoto hao imezikwa karibu na mji wa Alabama karibu na barabara kuu baada ya kuwasaka watoto hao kwa siku nzima .

Jones alisimamishwa katika kizuizi cha barabarani na kushukiwa kua alikua akiendesha gari baada ya kutumia dawa za kulevya ,imethibitika kuwa katika gari yake kulikuwa na kemikali zinazoaminika kua dawa za kulevya, zaidi ya hapo polisi walikuta damu garini mwake na alikua akitafutwa huko Carolina ya kusini .

Kitengo kinachoshulikia usalama wa raia huko Alabama kimesema kupitia kwa msemaji wake sajenti Steve Jarrett kwamba baada ya msako huo Jones baba wa watoto hao aliwaongoza maafisa hao hadi eneo alikozika miili ya wanawe(picha hapo chini ni ya mtuhumiwa huyo)

mshirikishe na mwenzio

BIBI AZAA NA MJUKUU WAKE


    Bibi mwenye umri wa miaka 72 wa nchini Marekani amewashangaza marafiki zake na familia yake baada ya kutoboa siri kuwa anatarajia kuzaa mtoto na mjukuu wake mwenye umri wa miaka 26.
Bibi Pearl Carter, 72, anasema kuwa hajawahi kuwa mwenye furaha kama wakati ambao amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mjukuu wake Phil Bailey mwenye umri wa miaka 26.

Bibi huyo wa Indiana, Marekani anatumia pesa zake za pensheni kumlipa mwanamke atakayejitolea kuibeba mimba yake na mjukuu wake.

Bibi Pearl alisema kuwa hajali maneno ya watu kuhusiana na uhusiano wake wa kimapenzi na mjukuu wake na anasubiria kwa hamu kuzaa naye mtoto.

Phil ni mjukuu wa bibi Pearl kwa mtoto wake wa kike Lynette Bailey ambaye alipelekwa kwenye nyumba ya kulea yatima alipokuwa na umri wa miaka 18.

Wakati mama yake alipofariki, Phil alimtafuta bibi yake ambaye alikuwa hana mawasiliano naye kwa muda mrefu na ghafla walianza uhusiano wa kimapenzi.

"Ilikuwa ni wiki ya pili pamoja baada ya chakula na mvinyo nilipomuita Phil chumbani kwangu, nilimkalisha kitandani na kuanza kumbusu", alisema bibi Pearl.

"Nilitarajia angenikatalia lakini naye alianza kunibusu" Pearl alisema akielezea mwanzo wa uhusiano wa kimapenzi na mjukuu wake.

"Kwa mara ya kwanza nilijihisi kwenye msisimuko mkubwa wa kimapenzi", alisema bibi Pearl.

Phil naye kwa upande wake anasema kuwa anampenda sana bibi yake na kwakuwa tangia zamani alikuwa akiwapenda wanawake wazee anadhani bibi yake ni mrembo sana.

Phil na bibi yake wametumia dola 54,000 kumlipa mwanamke atakayebeba ujauzito wao.

"Ni kweli tunachekwa na kutukwana wakati tunapobusiana mbele za watu lakini hatujali kitu", alisema Phil.

"Sitamuomba radhi mtu yoyote kwani naamini Mungu amenipa nafasi ya pili", alimalizia kusema bibi Pearl.

Apr 16, 2016

SABABU 10 ZA UGOMVI KATI YA MME NA MKE KWENYE MAHUSIANO

Ugomvi baina ya wapenzi katika mahusiano ni kitu cha kawaida kutokana na watu hao wawili kutoka katika malezi na mazingira tofauti ya ukuaji toka wakiwa wadogo hadi watu wazima.

Wawili hao wanapoaanza kujenga mahusiano na kukaa pamoja kama familia,kuna vitu kadhaa ambavyo kila mmoja wao huvitazama tofauti na hivyo kuleta migongano. Migongano ambayo inaweza ikarekebishika kama wenza hao watamua kuifanyia kazi na kuelewana.

Kuna vitu vingi ambavyo husababisha ugomvi na migongano ndani ya mahusiano ya mke na mme na hapa tunaeleza sababu kuu ambazo kwa kawaida hutokea karibu katika kila mahususiano

1. Wivu Na Kukosa Kujiamini

Wivu unatokana na jinsi ambavyo mpenzi mmoja anavyohusiana na watu wengine wa jinsia tofauti. Inaweza ikawa marafiki,wafanyakazi wenza au wapenzi wa zamani. Vyovyote vile itakavyokuwa ni kwamba wivu unasababisha ugomvi katika mahusiano mengi.

Kunatakiwa kuweka mipaka ya kutosha na iliyo wazi ili kujenga uaminifu kwa mpenzi wako na kumpa kujiamini. Mpenzi ambaye hajiamini ni tatizo kubwa kwani uwezekano wa kuanzisha ugomvi ni mkubwa.Hivyo ni vizuri ukamjengea mweza wako katika mapenzi kujiamini kwa kuwa mwaminifu.

Uaminifu ni kitu kimoja kikubwa sana katika mapenzi. Kama mwenza wako akikuamini hakutakuwa na wivu wa kupita kiasi na pia atakuwa anajiamini kuwa yeye peke yake ndio chaguo lako na hakuna mwingine.

2. Mawasiliano Finyu

Mawasiliano yanapovunjika katika mahusiano ugomvi ni kitu cha kawaida kutokea.

Mawasiliano ya kawaida kati ya wapenzi husaidia sana kutoa wasiwasi wa nyendo za mwenza wako. Huleta amani na kujenga uaminifu kwa mpenzi kwako.

Kuzungumza juu ya mipango yako ya mendeleo kama ujenzi au biashara ni vitu ambavyo ni muhimu sana kuvifanya vinginevyo utajenga wasiwasi kwa mweza wako na itasababisha ugomvi wa mara kwa mara.

Kuwa muwazi kwa mipango ya maendeleo binafsi,ya familia yako na ndugu.

Utafiti unaonyesha kuwa wapenzi wanaoongea na kusikilizana mara kwa mara hawagombani mara nyingi kama wale wasio na mawasiliano ya kutosha.

3. Masuala Ya Fedha

Japokuwa fedha si msingi wa mapenzi,lakini ni kitu ambacho kinahitajika sana katika maisha ya kila siku ya kila mtu na ya familia. Na kimekuwa ni mojawapo ya vitu ambavyo wapenzi katika mahusiano au ndoa hugombana sana juu yake.

Mwenza mmoja anapokuwa mtumiaji mbaya wa fedha na mwingine siyo,huibua malalamiko na ugomvi. Baadhi ya wapenzi hasa wanawake hawataki kuchangia kwa kiasi kikubwa katika mahitaji ya msingi ya nyumbani na badala yake kuwaachia mzigo mkubwa wanaume.

Hili linaibua malalamiko mengi kwa baadhi ya wanaume,na wakati ungine toka kwa wanawake. Matumizi makubwa ya fedha kwaajili ya pombe na sharehe nyingine kwa wanaume na baadhi ya wanawake kumekuwa mojawapo ya sababu za ugomvi juu ya fedha katika mahusiano.

Ni muhimu kwa wenza wawili kupanga jinsi ambavyo fedha zao zitapatikana na kutumika. Vipaumbele vya kufanyika kwanza na kiasi cha kutumika kwajili ya starehe na urembo kwa wanawake kwa mfano.

4. Masuala Ya Familia

Familia ya nani ianze kwanza na ipi ifuate ni tatizo kubwa katika mahusiano. Upendeleo wa upande mmoja ambao kwa asili huwa unatokea tu ni chanzo cha ugomvi ndani ya nyumba.

Mitazamo tofauti kati ya mmojawapo katika wapenzi na familia ya mwenza wake husababisha kutoelewana kwa wapenzi hao ndani ya nyumba.

Mbaya sana inakuja pale wanandugu wanapoingilia mambo ya ndani ya nyumba yenu. Wazazi wa kike na mawifi mfano, wamejulikana kusababisha matatizo mengi kwenye familia za watoto na kaka zao.

Kuepukana na hili ni muhimu kwa wapenzi ndani ya nyumba kuweka mipaka kwa ndugu ambayo haitaathiri uhusiano nao kama ndugu.

Pia ni muhimu kwa wenza hao kuweka mikakati ya pamoja juu ya kuhusiana nakusaidia ndugu toka katika familia zao mbili.

5. Suala La Unyumba

Japo kuwa suala kufanya mapenzi si kila kitu kwa wapenzi ndani ya nyumba lakini linachangia sana katika kuleta ugomvi aina yao. Kufanya mapenzi kupita kiasi au mara chache kunaleta matatizo kwa wapenzi hasa ambao wana uhitaji tofauti.

Wengine wanaona kama mpenzi ambaye hahitaji kufanya mapenzi mara nyingi na mwenzake labda anauhusiano na mtu mwingine zaidi yake. Au hamvutii tena kama zamani na huenda akaanza kuangalia nje.

Hii inajenga kutojiamini na kupoteza uaminifu,ambalo ni tatizo jingine kubwa katika mahusiano kama tulivyoonesha mwanzoni.

6. Vipaumbele Katika Maisha

Wapenzi wawili wanapokuwa na mipango na malengo tofauti ni tatizo kubwa. Watu wanapokuwa katika uhusiano ambao ni wa kuishi daima,malengo na vipaumbele vyao ni lazima vioanishwe na juhudi za kila mmoja zilenge katika kufanikisha mipango hiyo ya pamoja.

Kunapotokea kuwa kila mmoja ana malengo tofauti basi hata vipaumbele vitakuwa tofauti na hapo ndipo shida zinapoanzia.

7. Uaminifu

Uaminifu katika mahusiaono ni jambo la muhimu sana. Bila uaminifu ni ngumu sana kwa mahusiano yoyote kudumu.

Uaminifu ni kitu ambacho hujengwa kwa muda mrefu na kikipotea ni ngumu sana kukirudisha. Japo inawezekana kujenga upya uaminifu lakini huchukua muda mrefu sana.

8. Wapenzi,Marafiki Na Maisha Ya Zamani

Mojawapo ya vyanzo vya ugomvi kati ya wapenzi ni wapenzi wa zamani. Mawasiliano ya aina yoyote na wapenzi wa zamani huleta wasiwasi mkubwa kwa mpenzi wa sasa. Ni kitu ambacho wapenzi wawili wanahitaji kuongea na kupanga jinsi ya kuepukana na matatizo ambayo yanaweza kusababishwa na historia zao za maisha.

Kuepukana na hii ni vyema kuvunya uhusiano wa aina yoyote na wapenzi wa zamani labda tu kama wapenzi hao ni wazazi wenza au mnafanya kazi pamoja na ni ngumu kutokuonana au kuwasiliana.

Suala linalofanana na hili ni uhusiano na baadhi ya marafiki wa jinsia moja ambao wanachukuliwa kuwa mfano mbaya na mpenzi wako. Kama haiwezekani kutowasiliana na kuonana na wapenzi wa zamani au marafiki, basi ni vyema wakawa marafiki wa familia nzima na mawasiliano yoyote kati yenu nao yawe wazi pasipo kificho.

9. Watoto

Suala la uleaji na ukuzaji wa watoto linasababisha ugomvi mara nyingi kati ya wazazi. Jinsi gani mtoto avae au shule ipi aende linapelekea wazazi wengi kugombana.

Ni jambo la muhimu sana kukubaliana juu ya mambo ya msingi juu ya malezi ya watoto. Tofauti za wazazi ziangaliwe kwanza vinginevyo zitaingilia malezi ya watoto na kusababisha ugomvi juu yao.

10. Kazi Za Nyumbani

Imekuwa kama utamaduni kwa waafrika kuacha kazi nyingi kama si zote za nyumbani kwa mke. Kwa Wanawake ambao wanafanya kazi pia inakuwa ngumu sana. Hili linasababisha pia ugomvi kwa wapenzi nyumbani. Kama nguo ambazo mume anazivaa na kuzichafua tu bila ya kujali kuwa mweza wake ataumia wakati wa usafi na ikiwa yeye mwenyewe hajishughulishi na kufanya baadhi ya kazi za nyumbani ni wazi itasababisha ugomvi.

Ni vyema wanaume kuchukua baadhi ya majukumu nyumbani hata kama kutengeneza bustani au kulisha chakula mifugo.

 

Faida Ya Ugomvi Kati Ya Mke Na Mme Katika Mahusiano

Japokuwa ugomvi ni kitu cha kuepuka,lakini kina uzuri wake katika mahusiaono kama kikichukuliwa vizuri na kutumika kama kioo.

Kama mtu anagombana na mpenzi wake kwa madhumuni ya kuboresha ni kitu kizuri. Hii inaonesha kuwa anahitaji kuwa na wewe na anahitaji amani.

Ugomvi na mifarakano pia inatoa nafasi kwako kujiangalia vizuri na kama kinacholalamikiwa na mwenzio kina ukweli basi ni nafasi ya kujirekebisha.

Ni mategemeo kuwa kuna kipindi ambapo ugomvi utakuwa mkubwa na baadae wapenzi hao wataelewana na kurekebisha mambo yao.

i.  Ugomvi Unatoa Nafasi ya Kuongea Mambo Magumu

Wakati mwingine mazungumzo ya kawaida hayatoi nafasi ya wapenzi wawili kusema yale ya ndani na yanayozizonga nafsi zao. Ugomvi hufungua milango ya hisia za ndani na huenda vyanzo vya matatizo vikawekwa wazi na hivyo kufanyiwa kazi.

ii. Ugomvi unaonyesha Kuwa Mnajali na Mnataka Maboresho

Katika uhusiano ambao wenza hawajali,au hawana malengo ya muda mrefu huwa hawatoi duku zao juu ya utofauti na wapenzi wao.Hivyo wapenzi wanaogombana wanaonesha kuwa wana nia ya dhati na mwenzao na sio tu kupitisha muda.

iii. Ugomvi Unaboresha Uhusiano

Kwa muwa ugomvi unaibua hisia zilizojificha toka kwa wapenzi,ni wakati mzuri kuona matatizo ya kila mmoja. Na kama wapenzi hao wana nia ya dhati ya kuwa pamoja basi watafanyia kazi tofauti na mataizo waliyonayo. Hivyo kuboresha mahusiano yao

Kuna sababu nyingine nyingi ambazo zinachangia ugomvi kati ya mke na mme katika mahusiano lakini haya ni yale yanayotokea katika mahusiano mengi.

Je wewe unasababu nyingine inayosababisha ugomvi na mwenza wako? Shiriki nasi na tuandikie katika sanduku la maoni.

Nawatakia mahusiano mema na wapenzi wenu

SIRI YA MAFANIKIO

Adui yetu mkubwa katika maisha ya leo, labda kuliko maadui wengine wote unaowafahamu ni hofu.

Tuna hofu ya kupoteza kazi, hofu ya kuugua, hofu ya kufa, hofu ya kupoteza mpenzi, hofu ya kuanzisha biashara yako au labda hata hofu ya kukuza biashara yako, hofu ya kukosa mitaji n.k, kwa ujumla tuna hofu za aina nyingi zinazotuzunguka kila siku.

Na ni ukweli tu kwamba ni hofu hizo zinazofanya tusiwe wabunifu, tushindwe kujaribu mambo mapya, na labda ya hatari kidogo na tuendelee kuwa masikini, ni kwa sababu ya hofu zetu tunapoteza fursa nyingi.

Katika aina zote za hofu ninazo zifahamu, ni aina moja ambayo kwangu naona ndio kikwazo zaidi katika maendeleo yetu. Hofu ya kushindwa.Tuna hofu kwamba nikianzisha biashara ikafa watanicheka, nikijaribu kuuza kipaji changu (labda cha kucheza mpira au uchekeshaji) labda wenzangu wataona mimi si bora kuliko walionitangulia.

Ni kwa sababu hiyo basi tunashindwa kabla hata ya kuanza,tunakosa ubunifu na jamii inakosa vionjo mbalimbali kutokana na vipaji mbalimbali tulivyonavyo.
Zaidi sana dunia inakosa ladha ya kipekee, inayotokana na upishi wako wa kipekee, kumbuka wewe ni wa kipekee, na hivyo hivyo fikra zako, kipaji chako, mtazamo wako na hata utendaji wako
Vilevile.
habari ambayo labda si njema sana kwako ni kwamba kushindwa/kufeli ni jambo unaloweza kuliepuka tu, kama alivyosema mwanafalsafa mmoja,kwa kutofanya chochote,kutojaribu chochote,kutosema chochote na kutokuwa chochote.

Lakini wanasaikolojia wanatuambia, tumezaliwa na aina mbili tu za hofu nazo kama zifuatazo; 

1) hofu ya kuanguka(fear of falling)
2) hofu ya kelele/sauti(fear of noise),

hofu zingine zote tumefundishwa na ama wazazi wetu au walimu wetu shuleni. Ushauri wangu ni kwamba huu ni wakati wa kufuta hofu hizi zingine zote ambazo si asili yetu, haswa ukizingatia kwamba sisi si wototo tena,na kwa kweli inafaa kujifunza kutoka kwa watoto(labda niseme kujikumbusha, labda tumesahau,siku moja tuliwahi kuwa watoto),wao wanaujasiri wa kujaribu chochote bila kujali wengine watawafikiriaje au watawaonaje,au matokeo yatakuwaje.

Leo ni wakati wa kuzika hofu zako, na kuishi kama ulivyo katika uhalisia wako (as a real you), jiulize tu kama usingekuwa na hofu yoyote ungefanya nini tofauti leo, halafu amka nenda kakifanye, haijalishi kama ni kuanza biashara ya kuuza mbogamboga, au kufungua kituo cha kulea watoto (day care), au kufungua biashara ya kuuza vitu kupitia intaneti, au kuandika vitabu n.k chochote unachoweza kufikiria,nenda kafanye,tutafurahi kusikia hadithi yako.Kitu pekee cha kuhofia ni hofu yenyewe.

Apr 15, 2016

(ISHINDE HASIRA) FAHAMU MBINU ZA KUISHINDA HASIRA

1.    Jaribu kuelewa ni kwanini umekasirika.

Ni muhimu ukaelewa kwamba umefikia hatua ya kuweza kukasirika.Kama hali au mtu fulani akikukasirisha, nenda kazungumze na mtu unaye muamini anaweza akawa rafiki wa karibu, daktari wako, wanasaikorojia au watoa ushauri  nasaha wanaweza kukusikiliza na kukusaidia nini cha kufanya.

2.    Jaribu kupumzika na kutuliza mawazo.

Kupumzika kunaweza kuweka mpangilio mzuri wa ufikiri kichwani.Kupumzika kunaweza kukawa ni matembezi mafupi au kujiweka katika mazingira tulivu yasiyo na kelele au bugudha ya aina yoyote ile.Ukiwa huko matembezini ama sehemu tulivu, unaweza ukaangalia filamu, ukasoma kitabu, ukasikiliza musiki, ukaoga au kuogelea.Ni muhimu kila siku ukatunza muda kwaajiri ya kupumzika. Chagua kitu chote ambacho utafurahia kukifanya ufikapo muda huo.

3.    Fujo sii njia nzuri ya kumaliza hasira.

Wakati mwingine mtu anaweza akakukasirisha sana, kitu ambacho kitakusababisha umvagae/ umvamie na kuanza kupigana.Mara nyingi kuchukua uamuzi wa haraka na kutamka au kumvagaa mtu, hujaribu kuonyesha kile kilichopo ndani ya moyo wako kwa wakati huo, kitu ambacho ni hatari sana!! na baada ya hapo utakuta ukijiuliza aaah!! ni kwanini nimefanya hivyo?

Kuwa tayari kuzuia hali ya ugomvi wakati ukiwa na hasira, andika chini list ya hali, Watu au vitu vinavyo kufanya ufanye fujo.Baada ya kuandika vitu vyote ambavyo mara nyingi hukusababisha kukasirika, angalia sasa njia ya kuepukana navyo.Pia kuna baadhi ya watu ambao wanaweza kukusaidia jinsi ya kuepukana na hisia za kuvamia watu wakati ukiwa na hasira.

1.    Unatakiwa kuelewa kuwa kila mtu maishani mwake ana matatizo yake.

Sababu za wewe kutokuelewana na mtu mwingine ni nyingi, kwamfano itakuwa ni vigumu kuelewa anachokiwaza mtu mwingine kuhusu jambo fulani.

Lakini unatakiwa kujaribu kufikiri je watu wengine wanafikiri vipi kuhusu jambo fulani kabla hujachukuwa hatua.Jaribu kusikiliza ushauri wa watu lakini baada ya hapo usiharakishe kuutumia ushauri huo, kaachini tafakari, chuja na chukuwa hatua.

Sii kila ushauri huwa ni mzuri, kwamfano mwingine huchochea ugomvi, mauwaji, taraka, kuvunja mahusiano na mwisho wa siku unakuta unaishia pagumu zaidi.

Niwachache wanaweza kufurahia mafanikio yako, hivyo utakapo hitaji ushauri tu kosa, wanakuwa wamepata nafasi ya kukusambaratisha “take care”!!.

2.    Suruhisha migogoro yoyote inapotokea.

Migogoro ambayo haijapatiwa ufumbuzi huweza kuleta mkanganyiko na challenge kubwa katika maisha.”Mzaha mzaha hutumbukia usaha” mbaya zaidi hali hiyo inaweza kusababisha mshituko, kukosa usingizi, magonjwa, kudolola kwa mahusiano, fujo na kuvunjika kwa familia. Mfano mzuri ni moja ya filamu ya kibongo ambayo kwa bahati mbaya siwezi kuikumbuka jina lake.

 Lakini ilikuwa ni mgogoro mkubwa sana kati ya mume na mke ndani ya nyumba, hadi kufikia hatua ya kutaka kugawana mali zilizomo ndani ya nyumba.

Lakini rafiki wa mume ndiye aliyeweza kuinusuru vyema ndoa hiyo iliyokuwa kati kati ya mikono ya shetani, alichofanya alitazama wapi uzito wa mgogoro ulipotokea alafu akadili nao huku akijaribu kutoa mifano mikubwa  ya matatizo aliyokwisha kabiliana nayo, nahiyo ilisaidia kumuonyesha yule bwana kuwa tatizo alilonalo ni dogo sana, hivyo jamaa akarudi kuwa mpole ndani ya nyumba na mambo yakasonga.

3.    Amua migogoro kadri ya unavyoweza.

Kama kuna mgogoro kwa mtu mwingine ni rahisi kuwapunguzia hasira wawili hao. Nirahisi kwa mtu kusuruhisha iwapo umekuwa ukitazama tukio zimima wkati linatokea.Nivyema ukiamua kusuruhisha  ukajitosa kiukweli, kwamfano unweza ukatumia simu kumpigia kila mmoja nakuzungumza naye na kuona kama wanania ya kupata mwafaka?

Unaweza kuwaambia jinsi ulivyo sikitishwa na mgogoro huo, na pia unaweza ukatafuta mtu mwingine mwenye busara ambaye ataweza kukupiga tafu huku akijaribu kutoa mifano harisi kwa mfano ting’a zozote zile alizowahi kukumbana nazo.

MADHARA YA UTUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA(Epuka utumiaji wa madawa ya kulevya ni hatari kwa afya yako)

Bangi

ni mmea ulio na asilimia kubwa ya watumiaji kulingana na takwimu za afya zinavyo onyesha.Mmea huu una rangi ya kijani ambao hutoa majani, maua na mbegu ambazo hutumika kama kilevi. Bangi hustawi karibu maeneo yote hapa nchini na hutumika zaidi kuliko dawa nyingine za kulevya.

Kulingana na matukio, takwimu za afya zinaonyesha kuwa bangi hupatikana kwa wingi katika mikoa ya Mara, Iringa, Arusha, Kilimanjaro, Shinyanga, Tabora, Kagera na Mbeya.

Pia bangi hujurikana kwa majina mbali mbali kama, msuba,ganja, daga, jani, stiki, ndumu, kaya, msokoto na kadharika.

Mvutaji wa bangi hubakiza moshi mwingi kwenye mapafu kwa muda mrefu,moshi wa bangi unapoingia kwenye mapafu hutengeneza kitu kama lami ambayo huganda na kuathiri utendaji kazi wa mapafu.

Madhara:

Bangi husababisha madhara mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuumwa koo, kupata kikohozi na saratani ya mapafu, kuathirika kwa mfumo wa uzazi ikiwa ni pamoja na kuzaa watoto wenye mtindio wa ubongo na mabadiliko ya hedhi kwa wanawake.

Bangi pia hupoteza kumbu kumbu, kuchanganyikiwa, ukatili, ukorofi, uhalifu na kadharika. Pia kuna aina nyingi za sura tofauti za bangi kwa mfano, kuna mafuta ya bangi, bangi kavu na bangi iliyo sindikwa.

Mirungi:

Pia kuna aina nyingine ya dawa ya kulevya ambayo huwa na majina mengi ya mtaani kama “Miraa, mbaga, mogoka, veve, mogoka, gomba, kashamba” n.k

“Mirungi ni aina ya mimea inayostawi kwenye hali ya unyevu nyevu na milima yenye urefu kati ya futi 4000 hadi 9000. Hapa nchini mimea hii hupatikana kwa wingi kama uoto wa asili katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro,Manyara na Tanga, hata hivo kulingana na uchunguzi mirngi mingi itumikayo nchini kwa kiasi kikubwa hutoka nchini Kenya.

Madhara:

Kuna madhara mengi ya kiafya na kisaikolojia pia ambayo huwakumba watumiaji wa mirungi, mojawapo ya madhara hayo ni matatizo ya kisaikolojia kama, ukatili, kukosa hamu ya kula, vidonda vya tumbo na vindonda vya mdomoni, kupungukiwa maji mwilini, shinikizo la damu, maumivu makali ya kichwa, kuharibika kwa Ini.
Mirungi husababisha mtumiaji kukosa usingizi kwa muda mrefu hivyo kuongeza uwezekano wa kupata ajali, wanafunzi kushindwa kuelewa masomo. n.k.

Heroin:

Heroin ni aina ya dawa ya kulevya itokanayo na mmea unaojulikana kama “Opium poppy”dawa hii hupumbaza mfumo wa fahamu.
Kwamujiu wa ripoti za taasisi za afya zinaonyesha kuwa Heroin huingizwa nchini ikitokea nchi za mashariki ya mbali kama Afghanistani, Pakistan, Thailand, India n.k.
Dawa hii pia ina majina mengi ya mitaani kama Unga, Brown sugar,Ngoma,Ubuyu,Mondo, Panda, Dume Farasi n.k.

Matumizi:
Heroin hutumika kwa kuvuta, kunusa unga, kunusa moshi na kujidunga sindano.Kuna madhara mengi sana yatokanayo na utumiaji wa dawa hii aina ya “heroin” ambayo asilimia 100 hutoka katika nchi za ughaibuni, madhara hayo hujitokeza katika mengi kama, mtumiaji mwenye ujauzito na madhara ya kijamii kawa ujumla.

Madhara:

Mdhara hayo ni pamoja na kuharibika kwa mfumo wa ubongo na fahamu, mabadiliko ya hedhi kwa wanawake, kushuka kawa mapigo ya moyo, kupata kizungu zungu, kichefu chefu na kutapika, dozi kuwa husababisha kifo, mchanganyiko wa heroin na pombe huleta madhara makubwa zaidi ikiwa ni pamoja na kifo cha ghafla.

Utumiaji wa heroin kwa njia ya kujidunga sindano husababisha maambukizi ya “Virusi vya Ukimwi” (VVU) na magonjwa mengine ya damu kutokana na kushirikiana sindano na vifaa vingine.

Madhara mengine ni kwa watumiaji wenye ujauzito, ambayo ni kupata matatizo ya moyo, upungufu wa damu, mamba kuharibika, kuzaliwa watoto njiti, watoto kupata matatizo ya kiafya ikiwemo kuchelewa kukuwa kiakili na kimwili pia kujifungua watoo ambao mara nyingi hufa wakiwa chini ya umri wa miaka mitano.

Tumbaku

Japo uvutaji wa tumbaku una madhara mabaya sana kwa afya ya mvutaji, haina athari za mihemuko au kubadilisha tabia ya mtumiaji ukilinganishwa na utumiaji vibaya wa vileo vingine vya kawaida. Kwa hivyo, siyo kileo cha msingi cha kushughulika na mshauri nasaha wa madawa. Mara kwa mara, unaweza kuwa na fursa ya kuwaeleza ama wanafunzi kuhusu madhara ya tumbaku.

Uvutaji wa tumbaku una uraibu mkubwa. katika nchi zilizostawi kiviwanda, ni muuaji namba moja na unaendelea kutishia afya ya binadamu ulimwenguni kota. Hii ndiyo bidhaa ya pekee inayopatikana kihalali kote duniani ambayo hudhuru afya ya binadamu ikitumiwa ilivyokusudiwa. Aidha, inajulikana kwa kusabibisha vifo vingi kuliko vileo vyote vinavyoamsha akili.

Ni tatizo la afya muhimu sana linalozuilika katika nchi zilizoendelea. kama tukiendelea na mtindo huu wa sasa, vifo kutokana na tumbaku duniani kote vinatarajiwa kufikia milioni kumi kila mwaka au zaidi ya asilimia kumi ya vifo vyote duniani itimiapo robo ya pili ya karne hii.

Utumiaji wa tumbaku na wanawake wajawazito waweza kuzua matatizo yanayohusiana na mimba, kupunguza ukuaji wa mimba yenyewe, uzani mwepesi wakati wa kuzaliwa, kuzaliwa kwa watoto kabla ya kufikisha muda wao, kuharibika kwa mimba, watoto kuzaliwa wakiwa wafu, watoto kufa wazaliwapo na vifo vya watoto wachanga. matokeo ya kudumu kwa mtoto mchanga ni kama kudumuza ukuaji wa mwili na akili wa mtoto. Ushahidi wa hivi majuzi pia ulithibitisha kuwa uvutaji hudhoofisha kinga mwilini na hivyo kutia hatarini zaidi kinga ya wavutaji tumbaku wenye virusi vya UKIMWI.

Kwa sasa uvutaji tumbaku unasababisha asilimia tisini ya saratani ya mapafu, ambayo ni asilimia thelathini ya saratani zote zikiwekwa pamoja. Zaidi ya asilimia themanini ya ugonjwa sugu wa kifua pamoja na asilimia ishirini hadi ishirini na tano ya magonjwa yote ya moyo na kupooza husababishwa na uvutaji tumbaku. Wasiovuta kama vile watoto, wanapovuta moshi wa sigara katika chumba kisichoingiza hewa safi wakiwa na mvutaji huweza kupatawa na magonjwa ya matatizo ya kupumua, hasa kwa watoto.

Kokein
Mmea wa koka (trythroxylon coca) ni gugu lisilokauka lipatikanalo kwa wingi katika maeneo ya Marekani kusini mwa Mlima wa Andes. Kiungo chake tendaji ni alkaloid cokeini, uvumbi mweupe utolewao katika majani yake kwa njia urahisi. Kokeini ni dawa yenye matokeo ya uchachawishi.

Utumiaji wa koka ulikuwa mazoea ya jadi katika baadhi ya maeneo ya tamaduni za kihindi katika Milima ya Andes. Hutumika kama chachawishi, ikiongeza nguvu stahimilivu za mwili na akili huku ikimaliza hamu ya kula na kunywa. Utafunaji wa matawi ya koka ulijulikana pia kuwa una sehemu muhimu katika shughuli za mila na sherehe za baadhi ya makabila asili ya Marekani kusini, ikichachawisha ukariri wa mkusanyo wa visasili na ufufuaji wa kumbukumbu za kihistoria kupitia usimulizi wa hadithi.

Ukuzaji haramu wa kokeini duniani umeongezeka maradufu kati ya miaka 1985 na 1994. Jambo hili limesababisha ongezeko la biashara ya mihadarati na hivyo kueneza dawa hiyo katika maeneo mapya ya kijiografia hata kufikia sehemu za Afrika.

Uvumbi wa kokeini hutumizwa kwa njia ya kunisisha puani. Aidha, uvumbi waweza kupashwa na kugandishwa kuwa dutu ngumu yanye nguvu zaidi iitwayo kokeini 'ceack', ambayo yaweza kuvutwa kwenye kiko au kuyeyushwa majini na kudungwa kwa sindano. majani ya koka yanaweza kutafunwa peke yake lakini zoezi hili halifanywi na watumiaji nje ya wakazi asili wa tamaduni za Marekani kusini.

Dawa hii nguvu kubwa ya kusababisha utegemezi wa kisaaikolojia na kimwili. Utegemezi wa kimwili utakuwepo, kama kokeini imettumiwa katika viwmango vikubwa kwa muda mrefu. Utumiaji wa mwanzo wa kokeini husababisha na 'utmamu usioelezeka' unaofuatwa na wingi wa raha, ambayo hudumu kati ya dakika 30 hadi masaa machache kulingana na kipimo kilichonisishwa.

Watumiaji huripoti hisia za hali ya juu ya nguvu stahimilivu za akili na mwili, utambuzi wa hali ya juu, hisia za kujionea fahari, mwenye uwezo na mara nyingine wasiwasi au wazimu wa kufikiria unaonewa kila wakati. Baada ya hisia hizi kupungua, mtumiaji wa kokeini huweza kupatwa na mahangaiko, wasiwasi, mfadhaiko, kuwa katika hali ya kukasirika, kutokulala na shauku ya kutaka kokeini zaidi. matukio ya uchokozi yameripotiwa kwa watu kama hawa. Watumiaji wabaya waliozoea hupatwa na njozi. Utumiaji vibaya sugu wa kokeini humfanya mtumiaji vibaya kujifikiria mwenyewe, na hujulikana katika utmaduni wa vileo kama dawa ya "kujipenda".

Hivi ndivyo dawa hizi hatari za kulevya yani Bangi, Mirungi, naHeroin zinavyo athiri Taifa letu linalo tumia motto “hali mpya nguvu mpa na kasi mpya”

Kila kitendo kinacho enda kinyume na jamii huwa kina kiuka sheria ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, hivyo utumiaji wa dawa za kulevya ni makosa kisheria na sheria hiyo huhusika kudhibiti utumiaji, uuzaji, usafirishaji, uhifadhi au utengenezaji wa dawa za kulevya ni kosa la jianai.Adhabu kwa mtumiaji, mtengenezaji au msafirishaji atakayebainika hufikia hadi kifungo cha maisha.
Watanzania wenzangu tushirikiane na taasisi mbali mbali nchini ili tuweze angalau kulinusuru Taifa letu na vizazi vijavyo kuto athirika na dawa hizi ambazo zimeenea dunia nzima.

Apr 14, 2016

FAHAMU MADHARA SITA (6) YA KUTOA MIMBA

Kutoa mimba ni nini?
Hii ni hali ya mwanamke kwa hiari yake mwenyewe kuharibu mimba iliyoingia ndani ya kizazi chake.

Kutokana kuongezeka kwa idadi ya mahusiano duniani na kutotumia njia za uzazi wa mpango kwa watu wengi walioko kwenye mahusiano, wasichana wengi kwa sasa wanatoa mimba.
Utafiti nilioufanya mwenyewe nimegundua kwamba zaidi ya asilimia tisini ya wasichana wanaokua kwenye mahusiano na wanaume zaidi ya mwaka mmoja kabla ya ndoa hutoa mimba na asilimia tano tu ya wote ndio wanaamua kuzaa. Sio ajabu kusikia mtu ameolewa akiwa ametoa mimba nne mpaka tano. Sasa unajiuliza bado kuna mtu humo au mfu?

Hata hivyo hao wanaozaa pia hujikuta wamebeba mimba zingine wakati watoto wao wakiwa wadogo na kulazimika kuzitoa. Najua watu wengi wanatoa mimba kukwepa aibu, kutokua tayari kisaikolojia na kadhalika lakini ni bora kutumia njia za uzazi wa mpango kama condomu kuzuia mimba na kama kondomu huiwezi basi tumia njia zingine kama sindano na vijiti kwasababu wengi wenu mkishalewa pombe au kondomu isipokuepo ndio basi tena.

Hebu tuyaangalie madhara ya kutoa mimba kama ifuatavyo…

Uwezekano mkubwa wa kufa:
Utafiti uliofanywa na madaktari wa finland mwaka 1997 umegundua kwamba wanawake wanaotoa mimba wanauwezekano wa kufa mara nne zaidi kuliko ambao hawatoi mimba. Vifo hivyo vimekua vikisababishwa na kujiua wenyewe kutokana na kujuta kwa maamuzi yao na madhara ya mda mrefu ya kimwili yatokanayo na kutoa mimba. Vifo ndani ya wiki moja baada ya kutoa mimba hutokana na kuvuja damu sana, madhara ya dawa za usingizi, mabonge ya damu kwenye mishipa ya damu na mimba iliyotunga nje ya uzazi. Utafiti pia uliongeza kutoa mimba moja uwezekano wa kufa unakua 45%, mimba mbili 114%, mimba tatu 192%.

Ugumba kwa wanawake wengi:
Miaka hii ya karibuni wanawake wengi ambao wanalia kutopata watoto wana historia za kutoa mimba miaka iliyopita, na wengi wao nilionana nao wanajuta sana kwa maamuzi yao. Hii inatokana na madhara makubwa waliyoyapata kwenye mfuko wa uzazi baada ya mimba kutoka.

Mimba kutunga nje ya kizazi:
Mfuko wa uzazi una utando maalumu amaboa hufanya mimba iliyotungwa kwenye mirija iitwayo fallopian kuwezesha yai kushuka hadi kwenye mifuko ya uzazi. Lakini utoaji wa mimba huambatana na magonjwa ya mirija hiyo na kupoteza utando huo na kusababisha mimba kukulia huko.matibabu ya tatizo hili ni kukata mrija husika tu hivyo kuongeza hatari ya ugumba..

Kuzaa watoto wasio na akili nzuri:
Utoaji wa mimba kuharibu mlango wa mfuko uzazi kushindwa kushika vizuri na matokeo yake mwanamke huyu hujikuta akizaa kabla ya mda husika akibeba mimba nyingine. Lakini pia watoto hawa wanaozaliwa kabla ya muda maalumu  na viungo ambavyo havijakomaa hupata shida ya ubongo na kua wagonjwa wa akili maisha yao yote.

kansa ya mlango wa uzazi
Wanawake wanaotoa mimba wana hatari kubwa ya kupata kansa ya mlango wa uzazi kuliko wengine ambao hawajatoa mimba. Hii ni kwasababu ya kusumbuliwa kwa mlango huo kwa dawa za kutoa mimba, vifaa vya kutoa mimba na mabadiliko ya ghafla ya homoni za uzazi.

Kuathirika kisaikolojia;
Hakuna mwanamke ambaye hatakaa ajutie maamuzi yake ya kutoa mimba siku za usoni hata kama hakupata madhara yeyote hii itamfanya aishi kama ana deni Fulani maisha yake yote na itakua inamuumiza usiku na mchana. Zingine ni kukosa hamu ya kula, kusikia sauti ya mtoto anayelia wakati hayupo, kua na hasira sana…

Mwisho
kumbuka kila mwaka wanawake 70000 wanakufa kwa kutoa mimba...maumivu ya kukosa mtoto ni makali sana kuliko aibu ya kuzaa nje ya ndoa. Hawa wanaozaa sasa hivi unawaona malaya ipo siku utawakumbuka utakapo ambiwa na daktari kwamba labda itokee miujiza ndo utazaa.Kama hutaki mimba tumia njia za uzazi wa mpango kwani kuendelea kutoa mimba kutakupa adhabu ya kukosa mtoto ambayo adhabu hiyo utaitumikia maisha yako yote..