Apr 20, 2016

MTOTO WA MIAKA MIWILI AMPIGA RISASI MAMA YAKE.

Mwanamke mmoja katika jimbo la Idaho nchini Marekani ameuwawa na mtoto wake wa kiume wa miaka miwili kwa kumpiga risasi baada ya kuchukua bastola kwenye pochi yake.

Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Veronica J Rutledge, mwenye umri wa miaka 29, alipigwa risasi na mtoto wake huyo kwenye duka la Wal-Mart katika mji Hayden.

Msemaji wa duka hilo amesema mwanamke huyo alikuwa anafanya manunuzi akiwa na watoto kadhaa wakati wa tukio hilo. Maafisa wamesema marehemu kibali chake cha silaha kilikuwa kimefutwa.

No comments: