May 15, 2016

KABAANG: WEMA SEPETU NA OMMY DIMPOZ KWA MARA NYINGINE TENA WAONEKANA KWENYE PICHA HIZI TATA

LICHA ya tetesi kuzagaa kuwa amerudiana na

mpenzi wake, Idris Sultan, mtoto mzuri Bongo

Muvi, Wema Sepetu kwa mara nyingine

ametengeneza habari, amedaiwa bado

anaendeleza uhusiano wa siri na staa wa

Bongo Fleva, Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’,

Hiyo imedhihirika hivi karibuni baada ya

kuvuja kwa picha mpya za wawili hao wakiwa

chumbani katika mapozi ya kimahaba huku

1)Picha moja wapo ilimuonesha Dimpoz akiwa

amemwekea miguu Wema mgongoni huku

nyingine akiwa ameegesha mkono kwenye

kalio kitendo ambacho kinaleta tafsiri ya mtu

na mtu wake.

Dimpoz amekuwa akiendelea ‘kujiweka’ kwa

siri jambo ambalo watu wengi hawalitambui.

“Mbona kitambo tu, Dimpoz amejiweka kwake

kiulaini, sema wenyewe wanafanya mambo

hayo kwa siri. Si mnajua Dimpoz si mtu wa

kutangazatangaza mambo yake na ndiyo

maana hadi Nay wa Mitego (Emmanuel Elibariki) akafikia hatua ya kumhisi vibaya

hadi kumuimba kwenye wimbo wake,”

kilisema chanzo

MAZINGIRA YA TUKIO

Chanzo hicho kilimwaga ubuyu kuwa, picha

hizo walipiga wenyewe chumbani, nyumbani

kwa Dimpoz, Kinondoni jijini Dar hivyo zilibaki

katika simu ya Dimpoz ndipo chanzo hicho

kilipozikwapua na kuzituma kwa paparazi

wetu.

“Bwana nakupa lakini msinitaje huko, nyie

kamilisheni mambo yenu lakini habari ndiyo

hiyo; Dimpoz na Wema ni kapo ya kimyakimya

maana wenyewe hawataki kuanika mambo

yao,” kilisema chanzo hicho.

WEMA ASAKWA

Baada ya kupata ubuyu huo, Reporter wetu

‘alimvutia waya’ Wema ili kumsikia

anazungumziaje picha hizo na uhusiano huo

unaodaiwa ni wa siri, simu yake iliita bila

kupokelewa lakini baadaye rafiki yake mmoja

alisema huenda hakupokea kwa kuwa siku

hiyo alikuwa safarini kuelekea Dodoma.

“Jana (Jumatano) aliniaga ana safari ya

Dodoma so (hivyo) nafikiri yupo njiani na

wenzake na pengine kelele za wasanii ndani

ya gari si unajua tena na kaenda na wasanii

wenzake wengi tu,” alisema rafiki huyo

ambaye hakupenda jina lake lichorwe

gazetini.

DIMPOZ HUYU HAPA

Baada ya kumkosa Wema, Repoter wetu

alimtafuta Dimpoz ambaye alikiri kuwa picha

hizo zilikwapuliwa kutoka kwenye simu yake

lakini akadai hawana uhusiano wa kimapenzi.

“Hizo picha nazijua, nakumbuka tulipiga

hapahapa Dar. Ilikuwa ni hotelini na si

nyumbani kama huyo mtu alivyowaambia

lakini kitu cha msingi unachopaswa kujua,

Wema ni mshikaji wangu wa karibu na hakuna

kitu kingine zaidi ya ushikaji. Kuna mtu

itakuwa kanifanyia umafia kwenye simu lakini

nitadili naye lazima nitamjua tu,” alisema

Dimpoz.

KUMBUKUMBU

Wema na Dimpoz walidaiwa kuanzisha

uhusiano wa kimapenzi, Februari, mwaka jana

walipokuwa wakirekodi video ya Ommy,

Wanjera nchini Afrika Kusini.

Picha zao ‘tata’ wakiwa chumbani zilizagaa

kwenye mitandao ya kijamii na kuripotiwa

katika vyombo vya habari.

Baada ya hapo, Wema aliripotiwa kutembea

na wanaume tofauti akiwemo Idris Sultan,

mshindi wa Shindano la Big Brother Africa.

No comments: