Jun 15, 2016

BASI LA TAHMEED LATEKETEA KWA MOTO

Basi la abiria mali ya Kampuni ya Tahmeed, lililokuwa likitokea Jijini Tanga kuelekea Jijini Dar es salaam, likiteketea kwa moto mchana huu katika eneo la Komkonga.  Inaelezwa kuwa Ajali hiyo imetokea wakati Basi hilo likiwa limesimama baada ya Abiriammoja kuomba msaada tutani "WA KWENDA KUCHIMBA DAWA" ambapo baadhi ya Abiria wengine nao walishuka na kusikia harufu ya tairi linaloungua. muda mchache tu tairi hilo lilipasuka na moto kuanza kusambaa hadi kwenye tanki la Mafuta.Hakuna mtu yeyote aliepoteza Maishakwenye ajali hii na hakuna mali iliyoweza kuokolewa.

Jun 14, 2016

WAISLAMU WASAIDIA WAKRISTO KUJENGA KANISA

       Mji mmoja nchini Pakistan katika jimbo laPunjab, ambao ulipata umaarufu kutokana na vurugu zake dhidi ya makundi ya jamii ndogo umeleta watu pamoja kwa njia isiyo ya kawaida.Wakulima maskini wa Kiislamu katika kijijicha Gojra wanachanga fedha ili kusaidia katika ujenzi wa kanisa kwenye eneo lao.Lakini hali hii ya kuelewana na kuvumiliana kweli itawezekana katika eneo ambalo mara nyingi hutokea fujo zakidini

Jun 12, 2016

APATA KIPIGO BAADA YA KULA MCHANA HUKO PEMBA

Jana mchana, mtu mmoja kisiwani Pemba amejeruhiwa vibaya baada ya kupata kipigo kutoka kwa askari jamii. Mkasa huo umetokea katika kijiji cha Msingini Chake chake mkoa wa kusini pemba ambapo Polisi jamii wa Shehia hio waliamua kumpiga mtu huyo baada ya kuonekana akila mchana akiwa pamoja na wenzake watatu ambao walifanikiwa kukimbia na kutokomea kusiko julikana.

Jun 2, 2016

DIAMOND PLATNUMZ AMSAINI RASMI RICH MAVOKO

Mwanamuziki Diamond amemchukua rasmi mwanamuziki Rich Mavoko na sasa atakuwa chini ya lebo yake ya Wasafi ..Baada ya tetesi nyingi sasa leo rasmi amemtangaza mwanamuziki huyu kuwa chini ya lebo yakeAmeandika haya katika ukurasa wake wa Instagram