Kumekuwa na tabia kwa baadhi ya watu ‘kuflash’ simu kunakosababishwa na sababu kadha wa kadha; katika zama hizi za utandawazi vitendo vya watu kuporwa simu za mkononi vimeripotiwa kwa kiasi kikubwa na wengi wao waliona kuwa njia sahihi nikuziflash ili zitumiwe na mtu mwingine bila kujua kuwa ni kosa la jinai kutokana na sheria za mtandao.
Hayo yamebainika wakati zimesalia siku 36 pekee ili Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) kuzima simu zote ambazo hazijakidhi viwango huku Meneja Mawasiliano wa TCRA Innocent Mungy akisisitiza watu kuacha mara moja tabia hiyo kwani kwa kufanya hivyo kutapelekea simu zao kuzimwa ifikapo June mwaka huu kwa kuwa tayari zitakuwa zimetolewa ubora wake.
“Unapoflash simu lazima fundi atakubadilishia Software zilizokuwepo toka mwanzo alafu utakuwa umeharibu ubora wa kile alichotengeneza mwanzo hivyo kutokana na sheria za umiliki unakuwa umetenda kosa la jinai”. Alisema Mungy
Mamlaka ya Mawasiliano imetoa rai kwa wanaonunua simu za mkononi kwa wakati huu wa lala salama kuwa makini kwa kuangalia namba za IMEI kwa kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu wanapunguza bei za simu feki.
No comments:
Post a Comment