May 11, 2016

TP MZEMBE WAMLILIA SAMATTA

Jina la Mbwana Samatta limeacha historia kubwa nchini DR Congo hususani kwa mashabiki wa Klabu ya TP-Mazembe ambao wameshuhudia timu yao ikishindwa kufanya vizuri kwenye michuano ya Klabu Bingwa. Hapa ndio inaeleweka ni kwa nini Rais wa Timu hiyo Moise Katumbi alikuwa hataki kumwachia Mbwana Samatta.

Mazembe ilitolewa na Wydad Casablanca ya Morocco katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa na kuangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.

Thomas Ulimwengu amesema kwamba kwa sasa pengo la Mtanzania mwenzake, Mbwana Ally Samatta linaonekana ndani ya TP Mazembe. Ulimwengu alisema TP Mazembe kwa sasa inamkosa mtu mjanja na mwepesi, mwenye uwezo wa kufunga kama Samatta.

Samatta aliondoka timu hiyo ya DRC Januari mwaka huu baada ya kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na kujiunga na KRC Genk ya Ubelgiji anakoendelea vizuri hivi sasa.

No comments: