Hatimaye mtangazaji wa Clouds Fm, Gardner G. Habash amemjibu aliyekuwa mkewe, Lady Jay Dee, aliyemtaka aombe radhi ndani ya sikusaba kwa kauli aliyoitoa iliyodaiwa kuwa imelenga kumdhalilisha. Katika majibu yake amekana madai hayo.Siku chache zilizopita, Gardner alionekana katika kipande cha Video akisherehesha tukio la kumsaka mrimbwende wa chuo cha Tanzania Institute of Accountancy (TIA) jijini Dar es Salaam, ambapo alisema kuwa “yule binti sina tatizo naye, nimeshamkojoza kwa miaka kama 15hivi…”, kisha wimbo wa ‘Ndindindi’ waJay Dee ukachezwa na DJ.Kama ilivyokuwa kwa Lady Jay Dee aliyetoa siku saba za kuombwa radhi kupitia kwa mwanasheria wake Amani Tenga, Gardner amejibu kupitia mwanasheria wake Stephen Axwesso.Katika barua yake kwa mwanasheria wa Lady Jay Dee, mwanasheria huyo wa Gardner amekiri kuwa ni kweli mteja wake alizungumza maneno hayo alipokuwa katika shughuli iliyotajwa, lakini alidai kuwa hakuna sehemu aliyomtaja mkewe huyo wa zamani.Alisema kuwa madai ya upande wa Lady Jay Dee hayana mashiko na alimshauri mwanasheria huyo kupitiaupya sheria inayozungumzia wanandoa waliotalakiana ili aweze kumshauri vizuri mteja wake kuhusu suala hilo.Nakala ya barua hiyo pia imetumwa Clouds Media Group na kwa Rais wa Wanafunzi wa Chuo cha TIA.
May 21, 2016
May 18, 2016
VANESA MDEE NA SHILOLE WALUSHIANA MATUSI INSTAGRAM
Ni juzi tu tuliona video ya msanii wa kimataifa vanessa mdee akimfundisha yai local artist Shishi baby salon cha ajabu ni leo ghafla wamenza kutupiana maneno uko instagram.
shilole alianza na ujumbe wa kwanza hapo chini Haikuchukua mda nae vanessa mdee amendika maneno hayo chini kupitia instagram account yake
"Nikupe KICKIII ujulikane au sio? Kila siku twanyamaza ndiyo mtugaragaze. Sit the f**k down.
Mimi sio wale uliowazoea. P.s: You ain't worth this post inashushwa sasa hivi"#MessageSent
May 16, 2016
MAKOSA YA MWANAUME YANAYOMFANYA MWANAMKE AMSALITI
Kuna sababu anuai zinazomfanya mwanamke amsaliti mumewe. Ni muhimu kutambua kuwa mwanamke ni kiumbe mwenye hisia kali na daima ahisi raha na amani. Baadhi ya nyakati hufanya usaliti ili kuziba pengo la upungufu unaotokea katika maisha yake. Zifuatazo ni sababu kubwa ambazo zinamfanya amsaliti mumewe:
1. KUTOMPA KIPAUMBELE NA KUTOMTHAMINI
Tunatambua kuwa mke anafanya kazikubwa sana ambayo lau kama ingekuwa ni kampuni basi pangehitajika watu zaidi ya 10 kuzifanya. Atamtunza mume, watoto, nyumba na familia kwa ujumla.Wakati fulani mume anaweza akampuuza na asimthamini, licha ya kujitoa kwa moyo wote kumtunza na kuihudumia familia. Hivyo, kutotoa kipaumble kwa mke ni kosa kubwa ambalo linaweza likamgharimu mume, mke akipata mtu anayempa kipaumbele na kumuonesha thamani hakika hataacha kuitumia hiyo fursa.
2. UKOSEFU WA MAHABA
Kwa asili mwanamke ana silika ya hitajio la kupendwa, mwanamke anahitaji kupendwa, mwanaume yeyeana silika ya kupenda ngono, ukimpa ngono tu basi anaridhika.Mwanamke anahitaji kupetiwapetiwa,anahitaji kudekezwa, anahitaji aambiwe maneno yenye ladha adimu yaliyochanganywa na vionjo vya ndimu, mwanamke anataka hivyo, anataka aone kama anapendwa, anataka aone mtu anamwambia vile alivyo, alivyo maridhawa, amueleze hisia zake, ampe lugha ya kimajnun, mwanamke anamtaka Majnun. Sasa akimpata mtu wa aina hiyo, tofauti namumewe, huwa ni balaa tupu, mnanipata hapo?
3.USALITI WA MUME
Miongoni mwa mambo ambayo huibadilisha roho ya mwanamke ni pale anapogundua kuwa mumewe kipenzi anamsaliti. Hapo mwanamke anaweza akabadilika kabisa. Wapo wanaosamehe, lakini wapo wanaolipiza kisasi.
4. KUTOJIAMINI
Mwanamke anahitaji mwanaume anayemfanya ajiamini iwapo mumewe hatekelezi jukumu hilo, akimpata mtu anayemfanya ajiamini, yanaweza kutokea mengine kabisa. Hivyo, nasaha zangu kwa kaka zangu kuyaangalia kwa makini mambo haya.
May 15, 2016
GIGY MONEY:NIPO KWENYE MAHUSIANO NA GARDNER MIEZI 6 SASA
MUUZA sura kwenye video za Kibongo, Gift Stanford ‘Giggy Money’ amefunguka kuwa mtangazaji maarufu Bongo wa Clouds FM, Gardner G. Habash hachomokikwake na hadi sasa wako kwenye uhusiano wa mapenzi kwa muda wa miezi sita.
Gigy mefunguka haya baada ya picha zinazomuonesha akiwa kwenye mapozi yakimahaba na Gardner kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Giggy alisema mtangazaji huyo amekuwa mtu wa muhimu kwake kwa sasa.“Kwani kuna tatizo nikiwa na Gardner?
Yule ni mtu muelewa na sahihi kwangu, ninafikiri kupitia yeye nitajifunza mambo mengi na kuzidi kufanikiwa kwa sababu yeye ni moja kati ya watu ambao wako kwenye tasnia ya burudani kwa muda mrefu,” alisema Giggy Money.Gardner alipotafutwa ili aweze kueleza kuhusu ishu hii alisema:“Nipo karibu na Giggy lakini hatuna uhusiano wa kimapenzi, kwa hiyo kama anasema hivyo si kweli lakini yeye ni shabiki wangu na mimi ni mshabiki wake, ninapenda pia kazi anazozifanya,”.
KABAANG: WEMA SEPETU NA OMMY DIMPOZ KWA MARA NYINGINE TENA WAONEKANA KWENYE PICHA HIZI TATA
LICHA ya tetesi kuzagaa kuwa amerudiana na
mpenzi wake, Idris Sultan, mtoto mzuri Bongo
Muvi, Wema Sepetu kwa mara nyingine
ametengeneza habari, amedaiwa bado
anaendeleza uhusiano wa siri na staa wa
Bongo Fleva, Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’,
Hiyo imedhihirika hivi karibuni baada ya
kuvuja kwa picha mpya za wawili hao wakiwa
chumbani katika mapozi ya kimahaba huku
1)Picha moja wapo ilimuonesha Dimpoz akiwa
amemwekea miguu Wema mgongoni huku
nyingine akiwa ameegesha mkono kwenye
kalio kitendo ambacho kinaleta tafsiri ya mtu
na mtu wake.
Dimpoz amekuwa akiendelea ‘kujiweka’ kwa
siri jambo ambalo watu wengi hawalitambui.
“Mbona kitambo tu, Dimpoz amejiweka kwake
kiulaini, sema wenyewe wanafanya mambo
hayo kwa siri. Si mnajua Dimpoz si mtu wa
kutangazatangaza mambo yake na ndiyo
maana hadi Nay wa Mitego (Emmanuel Elibariki) akafikia hatua ya kumhisi vibaya
hadi kumuimba kwenye wimbo wake,”
kilisema chanzo
MAZINGIRA YA TUKIO
Chanzo hicho kilimwaga ubuyu kuwa, picha
hizo walipiga wenyewe chumbani, nyumbani
kwa Dimpoz, Kinondoni jijini Dar hivyo zilibaki
katika simu ya Dimpoz ndipo chanzo hicho
kilipozikwapua na kuzituma kwa paparazi
wetu.
“Bwana nakupa lakini msinitaje huko, nyie
kamilisheni mambo yenu lakini habari ndiyo
hiyo; Dimpoz na Wema ni kapo ya kimyakimya
maana wenyewe hawataki kuanika mambo
yao,” kilisema chanzo hicho.
WEMA ASAKWA
Baada ya kupata ubuyu huo, Reporter wetu
‘alimvutia waya’ Wema ili kumsikia
anazungumziaje picha hizo na uhusiano huo
unaodaiwa ni wa siri, simu yake iliita bila
kupokelewa lakini baadaye rafiki yake mmoja
alisema huenda hakupokea kwa kuwa siku
hiyo alikuwa safarini kuelekea Dodoma.
“Jana (Jumatano) aliniaga ana safari ya
Dodoma so (hivyo) nafikiri yupo njiani na
wenzake na pengine kelele za wasanii ndani
ya gari si unajua tena na kaenda na wasanii
wenzake wengi tu,” alisema rafiki huyo
ambaye hakupenda jina lake lichorwe
gazetini.
DIMPOZ HUYU HAPA
Baada ya kumkosa Wema, Repoter wetu
alimtafuta Dimpoz ambaye alikiri kuwa picha
hizo zilikwapuliwa kutoka kwenye simu yake
lakini akadai hawana uhusiano wa kimapenzi.
“Hizo picha nazijua, nakumbuka tulipiga
hapahapa Dar. Ilikuwa ni hotelini na si
nyumbani kama huyo mtu alivyowaambia
lakini kitu cha msingi unachopaswa kujua,
Wema ni mshikaji wangu wa karibu na hakuna
kitu kingine zaidi ya ushikaji. Kuna mtu
itakuwa kanifanyia umafia kwenye simu lakini
nitadili naye lazima nitamjua tu,” alisema
Dimpoz.
KUMBUKUMBU
Wema na Dimpoz walidaiwa kuanzisha
uhusiano wa kimapenzi, Februari, mwaka jana
walipokuwa wakirekodi video ya Ommy,
Wanjera nchini Afrika Kusini.
Picha zao ‘tata’ wakiwa chumbani zilizagaa
kwenye mitandao ya kijamii na kuripotiwa
katika vyombo vya habari.
Baada ya hapo, Wema aliripotiwa kutembea
na wanaume tofauti akiwemo Idris Sultan,
mshindi wa Shindano la Big Brother Africa.
VIJANA WANAOVAA SURUALI CHINI YA KIUNO KUCHAPWA VIBOKO 70
Wakazi wa Kata ya Karansi, Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro wametoa uamuzi kuwa wanawake watakaovaa sketi fupi na vijana watakaovalia suruali chini ya kiuno, wataadhibiwa kwa kuchapwa viboko 60 hadi 70.
Uamuzi huo umefikiwa na wakazi zaidi ya 200 wakisema uvaaji huo ni kinyume na mila na desturi za Kiafrika.Vazi lingine lisilotakiwa kwa wanawake ni kuvaa suruali pamoja na vijana kunyoa ndevu mitindo isiyofaa.
Mkutano huo ulioandaliwa na wazee wa kimila jamii ya Meru (Wachili) na Wamasai (Malaigwani), uliwavutia wananchi wengi ambao walihudhuria.
Sambamba na uamuzi huo utakaokuwa unafanyika hadharani, pia adhabu hiyo itawahusu wezi wa mali na wanaopenda kucheza pool table wakati wa kazi.Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Wilbrod Mutafungwa alipinga uamuzi huo akisema kwa maazimio hayo ya kuwaadhibu watuhumiwa kwa kuwachapa viboko ni kujichukulia sheria mkononi na ni kinyume na sheria.
May 14, 2016
JE WAJUA WANAWAKE WANAVUTIWA NA NINI ZAIDI KWA WANAUME??
Kama mwanaume lazima upate wakati wa kujua unatakiwa kufanya nini kwa ajili ya kulifanya penzi lako lizidi kuchanua.
USAFI BINAFSI
Asilimia kubwa ya wanawake wanapenda sana usafi. Ni aghalabu sana kukutana na mwanamke asiyejipenda. Ndiyo maana wanaitwamapambo ya nyumba au la nyumba! Ni kwa sababu ya hulka yao ya kupenda sana usafi.Mwanamke anavutiwa sana na mwanaume mtanashati. Usafi wako unamfanya ajiamini kuwa na wewe. Hata nyumbani kwako, lazima uishi katika nyumba safi. Hata anapokuja kukutembelea, anakuta mazingira masafi kuanzia sebuleni hadi chumbani.Anapokukuta katika hali ya usafi, inakuwa rahisi zaidi yeye kuanzia hapo alipokukuta na kuendelea mbele.
KUJIAMINI
Mwanamke anajisikia salama zaidi akiwa na mwanaume ambaye anajiamini – mwenye uwezo wa kutetea hoja zake na kujieleza sawia.Siyo anayebabaika. Suala la msimamo binafsi, kwa mwanamke nikubwa kuliko hata kumnunulia manukato mapya!Mathalani unakuwa naye katika mtoko, angependa kukuona ukiwa katika hali halisi ya maisha yako, usiyeyumbishwa na mwenye kutoa maamuzi yasiyoyumba.Wakati mwingine, mwanamke anaweza kukupima hata katika jambo ambalo amekosea yeye, ataangalia unavyotoa maamuzi yako,lakini pia atafuatilia kuona kama utakuwa mwepesi wa kuyabadilisha.Anataka kuona msimamo wako muda wote. Mwenye kujiamini na mawazo yasiyo na matege wala makengeza!
KUJITETEA
Kipengele hiki hakina tofauti kubwa sana na kilichopita, lakini hapa ni kwenye upande wa kujitetea zaidi. Wakati unapodai haki yako mbele ya mwanamke wako, suala la kujitetea linapewa nafasi kubwa sana.Wanawake hawapendi kuwa na wanaume ambao wapo tayari kuonewa. Wanataka wenye uwezo wa kusimama kidete kuona haki zao hazichukuliwi kirahisi.Hili si suala la kutetea tu haki yako pekee kama mwanaume, bali inapobidi kusimamia haki ya mwanamke wako. Nisieleweke vibaya katika hili, lakini mwanaume imara ni yule ambaye ana nguvu – anafanya mazoezi na ambaye yupo tayari kwa lolote!Inapowezekana, uwe na uwezo wa ‘kuzichapa’ ikiwa mtakutana na vibaka au watu wabaya wenye lengo wa kukudhuru/kuwadhuru au kumdhuru mpenzi wako.Mwanaume aliye ‘fiti’ ni chaguo la wanawake wengi. Si mnyonge. Mpole kupitiliza na aliye tayari kuonewa! Huyu hana nafasi.
KUJALI
Wanawake wanapenda sana wanaume wanaojali. Wanawaona wao ni kila kitu na wanaotoa kipaumbele kwao. Kama huna tabia hiyo, ujue upo katika nafasi kubwa yakumkwaza mpenzi wako. Mjali mpenzi wako kwa kila hali.Kumjulia hali kila wakati na kutaka kujua maendeleo yake, kutakupa nafasi kubwa sana ya kuendelea kudumu katika uhusiano hai.
UKARIBU
Kati ya vitu vinavyowapa mshawasha mkubwa wanawake ni pamoja na kusogezwa karibu. Hapa ni kuwa naye katika mambo mengi unayoyafanya kila siku.Ni vizuri kuwasiliana naye mchana, ukitaka kujua aina ya chakula alichokula siku hiyo au ikiwezekana mchagulie. Ni mambo madogo sana lakini yanayoongeza nakshi katika mapenzi.Yapo mengi sana ambayo kwa kuyafanya utakuwa umemsogeza mpenzi wako karibu yako. Hebu tumia ubunifu wako ili uweze kuteka hisia za mwenzi wako kisawasawa!
KUMSIFIA
Wanaume wengi hupuuzia hili, huonakama ni jambo lisilo na maana sana kwao na wenzi wao. Hali ni tofauti sana kwa wanawake ambao hupenda kuwasifia wanaume zao. Nitakupa mifano miwili ya namna wanandoa wa jinsia mbili tofauti wanavyotambulishana kwa jamaa zao.MWANAUME: “Peter kutana na mke wangu, anaitwa mama Diana. Nipo naye mwaka wa tatu sasa, tuna watoto wawili, huyo Diana na mwingine anaitwa Cris. Mama Diana,huyu ni Peter nilisoma naye A – Level, Tosamaganga Sekondari.”MWANAMKE: “Suzan, huyu ndiye mume wangu mpenzi...anaitwa Elifaraja lakini mimi napenda zaidi kumuita Elly. Kiukweli nampenda sana mume wangu jamani, tuna mtoto wetu mmoja, anaitwa Agness. (Akimgeukia mumewe) Baby, huyu hapa ni rafiki yangu Suzan. Yaani tumekua naye mtaa mmoja huko Arusha.”ANGALIA TOFAUTIBila shaka kwa namna wawili hao walivyotambulishana unaweza kuona tofauti kubwa. Mwanaume amemtambulisha mkewe kawaida kabisa, hajaonesha manjonjo au namna anavyompenda na kumthamini mwenzake, lakini mwanamke amefanya hivyo.Sikia nikuambie,
KUMSIFIA mwanamke, kuna nafasi kubwa sana kwake. Chunguza kwa makini, hata kunapokuwa na mgongano katika familia, halafu wakatokea wageni, baada ya utambulisho na mazungumzo ya hapa na pale, wageni wakiondoka kunakuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kumaliza mpasuko katika familia.Jenga utamaduni wa kumsifia mpenzi wako, unamuweka katika kilele cha upendo. Anajiona kamili, peke yake na mwenye nguvu kwako. Anajiamini na unamfanya azidi kukupenda kwa kuwa anaamini yupo na mwanaume ambaye anajivunia kuwa naye.
MALENGO
Wanaume wengi wana ulemavu mmoja; hawapendi kuwashirikisha wanawake katika mambo yao. Wanapenda kufanya mambo yao kwasiri na wakati mwingine ikilazimika kumwambia mkewe basi kwa mshtukizo baada ya kukamilisha jambo husika.Hii si sahihi. Dunia ya leo imebadilikarafiki zangu. Inawezekana wazee wa zamani walikuwa sahihi, maana ilikuwa ni suala la kununua ng’ombe na kuwaweka katika zizi kwenye kijiji cha jirani, halafu wanapewa malisho mazuri, baada ya miaka miwili wanazaliana, hapo ndipo anamweleza mkewe.Siku hizi dunia imebadilika, kuna mambo mengi. Kuna suala la hasara katika biashara, utapeli n.k. Mkeo ndiye rafiki yako mkubwa kuliko wote, ndiye ndugu yako wa karibu zaidi kuliko yeyote. Yes! Mkeo ndiye ndugu yako maana umetengeneza naye familia. Mmeshirikiana kuzaa watoto na kujenga maisha pamoja.Yeye anapaswa kujua mambo yako, ndiye mtetezi wako nambari wani. Mweleze juu ya malengo yako, wakati mwingine anaweza kukusaidia sehemu ambayo hukutarajia.Hata hivyo, kumshirikisha katika malengo yako, kunampa nguvu na nafasi ya kujiona mama katika familia yenu. Msaidizi kamili wa nyumba yenu.
KIPAUMBELE
Kuna wakati wanawake huwa na mambo yao binafsi. Kazini au kifamilia. Inawezekana akatatizika katika eneo fulani ambalo kwa namna moja ama nyingine atahitaji usaidizi wako. Ikitokea mkeo akawa katika hali hiyo, msikilize.Mathalani ana tatizo la kifamilia, amekuambia mmoja wa wazazi wakeanaumwa, msaidie. Si lazima kifedha, lakini kuonesha kujali kwakotu, kutampa matumani kwamba anaishi na mtu sahihi. Acha kupuuzamambo yake; hata yale madogo, kama ya ‘mtoto wa dada amerudishwa ada shuleni’.Msikilize, mshauri panapofaa kufanya hivyo na ukiweza msaidie hata kifedha. Katika upande wa pili nihivyo hivyo. Labda una tatizo binafsi,kazini kwako au kifamilia, mshirikishe.Unaweza kushangaa jambo ambalo uliamini unaweza kulimaliza peke yako, kwa kumshirikisha likawa jepesi zaidi na mambo yakaendelea vyema. Kipaumbele kwa namna yoyote ile,kunaongeza mapenzi zaidikwa mwanamke.TENDO LA NDOAHiki ni kipengele nyeti, kinachohitaji lugha nzuri ya kirafiki kukifafanua. Hakuna siri,tendo la ndoa ni moja ya kiwakilishi cha ndoa. Maana hata maandiko yanasema: “Mwanamke ataacha wazazi wake na kwenda kwamumewe, nao watakuwa mwili mmoja.”Kimsingitendo la ndoalina nafasi yake. Ni muhimu likaheshimiwa na kutengewa muda maalum wa kufurahia. Si papara. Kwa bahati mbaya wanaume huwa si wafuatiliaji sana wa kujua namna ya kuwafurahisha zaidi wenzao. Wenyewe wanajiwazia wenyewe. Wanafikiria namna ya kuwakomoa wenzao.Si sahihi.Tendo la ndoahalina maana ya kukomoana. Jenga mazoea ya kufanya maandalizi kamili kabla ya tendo. Sikiliza hisia za mwenzako. Ukiweza kumjulia mke wako katika eneo hili, ni wazi kwamba utazidisha upendo wake kwako, lakini pia atakuwa katika kuta za uaminifu. Akatafute nini nje wakati wewe ndiyemganga wake unayeweza kumtibu barabara?Kuna kitu nimesahau kweli? Kama kipo nitafute pembeni, kwa hapa haya yatoshe kukufanya uelewe nilichotaka kukuelekeza. Nikuache na neno moja; uamuzi wakuijenga ndoa yakoupo mikononi mwako. Ukitaka iwe shaghalabaghala, pia ni wewe tu!CHANGIA MTAZAMO NA MAONI YAKO JUUYA HII MADA..
INDIA JOURNALIST ARRESTED OVER MUSLIM YOGA BAN REPORT
A journalist in India is facing charges over a report he wrote saying Muslims were banned from being yoga teachers under government policy.Pushp Sharma's report appeared in March in the Milli Gazette, a newspaper aimed at India's Muslim community.It quoted what was said to be a government document that banned Muslims from travelling abroad to teach yoga for last year's World Yoga Day.Mr Sharma faces charges of fabricating the document, which he denies.His reportwas based on what he said was an official reply from a government ministry that promotes yoga and ayurveda medicine.The report said that, after several queries to the ministry, it replied saying that none of the 3,841 Muslims who hadapplied to become yoga teachers had been hired up to October 2015.A letter printed alongside the article, purporting to be from the ministry, said that 711 Muslims had applied to travel abroad as instructors during the first World Yoga Day last June, but none was selected "as per government policy".The letter does not include a government letterhead and contains a number of spelling mistakes, including an incorrect spelling of the word "yoga".The Milli Gazette confirmed Mr Sharma was arrested on Saturday morning. Its editor Zafarul-Islam Khan said the charges were "clear attempts to stifle the freedom of the press".Police in Delhi told NDTV that Mr Sharma was facing charges of "cheating,forgery and promoting enmity between different groups on grounds of religion or race".India's Prime Minister Narendra Modi, a yoga enthusiast who says he daily practises the ancient Indian art, lobbied the United Nations to declare 21 June World Yoga Day. The first event was heldlast year.His support for yoga, and creation of the new yoga ministry, was criticised as "a campaign to enforce Hindu rituals on all non-Hindus," one Muslim officialtold Reuters last year.After opposition from Muslim groups, a series of Hindu practices were dropped from the first World Yoga Day events in India.In response, a Hindu priest and MP for Mr Modi's BJP party, Yogi Adityanath, said anyone who opposed taking part should "live in a closed room or must jump into the sea".
May 13, 2016
MHUDUMU WA TRUMP ATAKA OBAMA AUAWE
Huduma ya ujasusi ya Marekani imeanzisha uchunguzi baada ya aliyekuwa muhudumu mkuu wa nyumbani kwa Donald Trump kutaka raisBarrack Obama auawe.Anthony Senecal aliandika katika mtandao wake wa Facebook kwamba Obama angechukuliwa na jeshi na kupigwa risasi kwa kuwa adui katika muhula wake wa kwanza.Bwana Senecal alimfanyia kazi bwana Trump,mgombea wa urais kupitia chama cha Republican kwa takriban miaka 30.Kampeni ya Trump hatahivyo ilijiepusha na matamshi ya Senecal.''Hakuajiriwa na Trump na hajaajiriwa tangu mwezi Juni 2009'', alisema msemaji wa kampeni ya Trump Hope Hicks katika taarifa.''Tunashtumu matamshi haya machafu kutoka kwa Senecal.Chapisho hilo la Bwana Senecal halikuwa hadharani.Na baadaye siku ya Alhamisi, bwana Senecal mwenye umri wa miaka 84 alikiambia chombo cha habari cha CNN kwamba Obama anafaa kunyongwa nje ya Ikulu ya White House.Pia aliitaja Ikulu ya White House kuwa ''msikiti mweupe''.
BOKO HARAM LINKS TO (IS) ALARM (UN)
The UN Security Council has said it is alarmed by ties between Nigeria's Boko Haram Islamist militants and the Islamic State (IS) group.
In a statement, it said Boko Haram - which pledged allegiance to IS in 2015 - continued to "undermine the peace and stability" in West and Central Africa.
Meanwhile, a senior US official said there were reports of Boko Haram fighters joining IS in Libya.
Nigeria is to host a summit on Saturday on fighting Boko Haram.
President Muhammadu Buhari will welcome counterparts from Benin, Cameroon, Chad and Niger for the gathering in Abuja, along with French President Francois Hollande, UK Foreign Secretary Philip Hammond and US Deputy Secretary of State Antony Blinken.
'More contacts'
In the statement, the 15-member UN Security Council expressed "alarm at Boko Haram's linkages with the Islamic State".
It also voiced its support for Nigerian President Muhammadu Buhari's "crucial initiative" to hold the security summit in Abuja.
Meanwhile, Mr Blinken - who is already in Nigeria - said he was concerned by reports that Boko Haram militants were going to Libya, where IS influence has grown in recent months.
"We've seen that Boko Haram's ability to communicate has become more effective," he said.
"They seem to have benefited from assistance from Daesh [IS]."
Mr Blinken added: "So these are all elements that suggests that there are more contacts and more co-operation, and this is again something that we are looking at very carefully because we want to cut it off."
At the same time, he declined to comment on whether the US would agree to a Nigerian request to sell it American war planes to fight Boko Haram.
WATOTO WALIWA NA FUNZA BABA YAO ADAI NI DHAMBI KUUA KIUMBE CHOCHOTE
WAUMINI wa Kanisa la Holy Ghost Tebernacle katika Kaunti ya Murang’aAlhamisi walimvamia mshirika mwenzao waliyemshitumu kwa kuwatesa watoto wake na uvamizi wafunza kwa 'kukataa' kuwatafutia huduma za kimatibabu.Washirika hao kutoka eneo la Kiamaihwa katika Kaunti ndogo ya Kigumo walidai kuwa muumini huyo wa kiume alikuwa akitii itikadi kali ambazo hupinga mauaji ya kiumbe chochote kilicho hai, wakiitaja kama “iliyopitwa na wakati”.Pasta Joseph Mwaura wa Kanisa hiloaliambia Swahilihub kwa njia ya simu kuwa “watoto wawili wa muumini huyo wake walikuwa wamevamiwa nafunza kila sehemu ya mwili na wakitembea ungedhani walikuwa wakicheza mchezo wa kuigiza uliohitaji wahusika kutembea kana kwamba wanacheza densi na kujikunakuna!”“Baada ya kupata habari hizo, waumini wenzangu wakiwa zaidi ya 100 walimvamia muumini huyo alipowakataza kutekeleza uokoaji huo wa watoto wake na kisha wakamwamurisha awatoe watoto hao nje watolewe funza,” akasema.Alisema kuwa watoto hao wote wakiwa ni wa kiume wa kati ya miaka 10 na 13 walikuwa wamevamiwa na wadudu hao na ikabainika kuwa hata hawakuwa wakienda shule.“Waumini hao walikataa katakata kumsikiza baba watoto hao akisema kuwa walikuwa wakimtakia laana kutoka kwa Maulana ikiwa angewakubalia waue funza hao!"Aliongeza kuwa aliteta vikali kuwa imani yake haingemruhusu kuua kiumbe yeyote aliyeumbwa na Mungu, akiongeza kuwa funza hao walikuwa wametumwa kukaa katika 'hekalu' - yaani miili ya wanawe.Funza kutumwa“Alituambia kuwa wadudu hao wametumwa ndani ya miili ya watoto wake na hakuna vile angeweza kupingana na tukio la kiroho. Alishikilia kuwa Mungu angewaamrisha watoke kutoka miili ya wanake atakapoamua kufanya hivyo,” akasema Pasta Mwaura.Baba huyo alidaiwa kubishana kuwa imani ya waumini hao waliomvamia kwake ilifaa kuwa ya kulisha watu kiroho wala sio kutibu magonjwa au kutekeleza uokoaji wa watu kutoka naukarimu wao kwa viumbe wa Mungu.“Alitulaumu kwa kupotosha waumini kuwa madawa ya kizungu ni suluhu kwa magonjwa, akiyataja kama uchawi wa Kizungu!,” akateta Pasta Mwaura.Aidha, bwana huyo alisisitiza kuwa hakuna mahali ndani ya Biblia ambapo Yesu alionekana akitafuta matibabu hospitalini.Hata hivyo, ubishi wake haukumfaa kwa lolote kwa kuwa waumini hao walifanikiwa kuwaokoa watoto hao ambapo waliwatoa funza hao na hatimaye wakapakwa dawa ya kutibu vidonda.“Aidha, waokoaji hao waliwapeleka watoto hao hadi hospitalini kwa matibabu zaidi ambapo walipewa dawa zaidi ya kupulizia nyumba yaoili kuuwa wadudu wanaosababisha uvamizi wa funza,” akasema pasta Mwaura.Alisema kuwa kuanzia Jumatatu ijayowatoto hao watasajiliwa shuleni na ambapo wamemuomba chifu wa eneo hilo kumwandama baba huyo ili atimize hilo.“Wakati umefika kwa waumini wa Kikristo kutupilia mbali itikadi ambazo zimewasababishia ujinga, magonjwa na umasikini,” akasema.ULIMWENGU WA PILI BADO UNASUMBULIWA NA FUNZA KWELI!!!ONLY IN KENYA
May 12, 2016
MZIWANDA:NILIWAFUMANIA MADEE NA SHILOLE LIVE..
Aisee hii hata mimi nilipitwa nayo ama kweli mimi mapenzi basi nimeyavulia Shati.
akuu mapenzi sio ubondia bora nijitoeLeo akihojiwa na Diva clouds Fm Mziwanda amekiri kuwa Madee alitembea na Shilole kipindi wapo wote na Aliwafumania na kumkuta mmoja wao akiwa hana nguo,Diva anakiri kusikia hizo habari ila alitaka Nuh athibitishe Nuh anasema inauma sana ila ana muheshimu sana Madee ana Muheshimu pia Shilole japo Inauma sasa wali kwichi kwichi na kuwafumaniaOyo nitakupigia nitakupia baadae noma noma noma sanaaaaaHapa Miguu pande hapa Say my name Shishi hapa Jike shupa oyooooo
YANGA YAPEWA PONGEZI
Uongozi wa Klabu ya Soka Yanga umetoa pongezi kwa wachezaji wake kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacon Tanzania kwa mara ya pili mfululizo.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Habari wa Yanga Jerry Muro, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya Klabu hiyo na kusema uongozi wa klabu hiyo unawashukuru wachezaji hao kwa kujituma pamoja na mashabiki wa soka wa klabu hiyo kuwaunga mkono kwa kuwashangilia kila michezo.
Amesema Jumamosi ya wiki hii timu ya Yanga itakabidhiwa Kombe lake katika Uwanja wa Taifa mara baada ya kumalizika kwa mchezo wake wa Ligi Kuu dhidi ya Ndanda FC.
Katika hatua nyingine Muro amesema maandalizi ya kuelekea Angola kwa ajili ya mchezo wa marudiano na timu ya Esperanca utakaofanyika Jumatano majira ya saa nane mchana kwa saa za Afrika Mashariki yanaendelea.
UVCCM WAGOMBANIA NYUMBA YA NYERERE MWANZA
Eneo la mapumziko ya Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, limegubikwa na mgogoro kati ya wakazi wa Kata ya Igoma dhidi ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza kuhusu uhalali wa umiliki wa eneo hilo.
Ni mvutano wa miaka kadhaa sasa tangu mgogoro huo ulipoanza kurindima ambapo wakazi wa eneo hilo linalofahamika kama Mtaa wa Nyerere, wamedai kuwa mtaa huo upo chini ya umiliki wao tangu miaka ya 70, wakati wa harakati za Azimio la Arusha ingawa wakazi hao wamethibitisha kuwa wanao uhalali wa kuendelea kuishi katika eneo hilo, lakini Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Nyamagana mkoa wa Mwanza umeyapinga madai hayo.
Wakati mvutano huo ukiendelea, Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyerere Kata ya Igoma John Manoni, akatolea ufafanuzi juu ya mgogoro huo.
Tangu mgogoro huo ulipoanza kurindima miaka ya 70 hadi sasa, umesababisha wakazi wa mtaa huo kushindwa kuliendeleza eneo hilo, huku wakiiomba serikali kuingilia kati ili kutatua mgogoro huo.
SAKATA LA SUKARI:MAKONDA AAGIZA UPEKUZI WA MAKONTENA YA BILIONEA DEWJI
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza kuchunguzwa kwa sukari kontena 115 ambayo ni zaidi ya tani 3,000 iliyokutwa katika Bandari Kavu ya PMM iliyopo eneo la Vingunguti.
Makonda alitoa agizo hilo alipofanya ziara ya kushtukiza katika bandari hiyo na kubaini uwepo wa sukari hiyo ambayo ni mali ya Mohamed Enterprises, ambayo kwa taarifa zake aliambiwa zilikuwa kontena 165.
Makonda ameziagiza Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Shirika la Viwango (TBS) kuichunguza sukari hiyo kutokana na sababu mbalimbali zilizojitokeza katika uwepo wa sukari hiyo kama sukari kuagizwa kutoka Dubai lakini imetoka Brazil na imepakiwa Dubai na upangwaji wa kontena hizo katika bandari hiyo.
“Nashindwa kuelewa kwa nini sukari iagizwe kutoka Dubai lakini itoke Brazil na kufungashwa Dubai, inaonesha inaweza kuwa imeshawahi kuisha muda wake hivyo nataka ichunguzwe na tunataka tujue kama Mohamed Enterprises anaficha sukari ili ipelekwe kwa wananchi kwa matumizi,” alisema Makonda.
Mbali na kutoa maagizo hayo, Makonda pia amezuia kutumika kwa sukari mifuko 22,000 iliyokutwa katika ghala la Mohamed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) lililopo Barabara ya Nyerere na kutaka wapeleke vielelezo kuhusu sukari hiyo kwa mamlaka zinazohusika kama ya matumizi yoyote.
WATU 35 KUTOA USHAHIDI KESI YA KUPINGA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI
KISUTU: Baada ya Kesi namba 3/2015 ya kupinga Matokeo ya Uchaguzi ya Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Jijini Dar es Salaam Maulidi
iliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Iddi Azan (CCM) kuahirishwa kusikilizwa mara 3 mfululizo ndani ya wiki hii kwa sababu mbalimbali, Jaji Chocha kutoka Mahakama ya Mbeya ameahirisha tena kusikilizwa kwa shauri la kesi hiyo leo na kuipangia Mei 19 ya mwezi huu.
msingi
ya
Madai
kutoka nane, hivyo
kuahirishwa kwa kesi
baada ya Abubakari Salim Wakili wa upande wa Iddy
mahakama impe muda wa wiki moja wa kuandaa mashahidi
viapo, ambapo Jaji Choche alikubali.
Abubakari Salim
Upande wa Mshitakiwa
(Maulidi Mtulia Mb) umethibitisha kuwa na wenyewe watapeleka mashahidi 10, wakati upande wa mshitakiwa namba 2 na 3 (Mwanasheria Mkuu na Tume ya Taifa ya Uchaguzi), na wao watapeleka mashahidi 15.
Jimbo la Kinondoni waliojitokeza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
manne
Msingi
ya
Madai
katika kesi hiyo ni
Mbunge Mtulia haukuwa halali 2. Katika moja ya Kituo cha Uchaguzi, Mwangalizi wa CUF alipiga kura nyingi kwa ajili ya mbunge huyo, 3. Mawakala
Azani (CCM) walitolewa nje, 4. Unafuu kwa pande zote mbili.
DR.LIPUMBA:AWATETEA WAFANYABIASHARA
Rais Dk. Magufuli alipiga marufuku uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi bila ya kuwa na kibali cha serikali mapema mwaka huu ili kuondoa ushindani usio rafiki kwa viwanda vya ndani vya bidhaa hiyo, Prof. Ibrahim Lipumba, Mtaalam aliyebobea kwenye masuala ya Uchumi,amenukuliwa hivi karibuni akisema Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli anatumia cheo kuwanyanyasa wafanyabiashara.
Lipumba ameyasema hayo katika mahojiano ya moja kwa moja na Kituo kimoja cha Runinga hapa nchini wakati akichambua sakata la ufichwaji wa sukari nchini.
Amesema kuwa endapo angekua anakaa na Rais Magufuli angehakikisha kunakuwepo na utaratibu wa uagizaji wa sukari kwa watu ambao ni waaminifu ambao hawatakwepa kodi zilizowekwa na kuagiza sukari ili pamoja na gharama na faida iweze kuuzwa kwa bei ya Tsh 1,800 ili viwanda vya ndani vinavyozalisha sukari viweze kulindwa.
“Tuepukane na kufanya mambo mazito ya sera kwenye majukwaa ya siasa na kuwatisha wafanyabiashara katika hali ambayo haiendani na hali halisi iliyopo” amesema Prof. Lipumba.
Hayo yanakuja siku chache baada ya Rais Dk. John Magufuli kutangaza kutaifisha tani za sukari zitakazokamatwa zikiwa zimefichwa na wafanyabishara kwenye maghala na kisha kuzigawa kwa wananchi bure.
Hata hivyo imeripotiwa hivi karibuni kuwepo kwa malalamiko ya kupanda bei ya sukari kutoka kikomo cha bei elekezi ya shilingi 1800 kwa kilo hadi kati ya 2,500 na 2,800.
INSTAGRAM YAZINDUA NEMBO MPYAA
Instagram imezindua nembo mpya katika hatua ya kutaka kujiboresha na kutoonekana kuwa programu ya picha pekee.Nembo hiyo imetengezwa kuimarisha ujumbe unaotumwa.Nembo hiyo inaonyesha kamera ya kawaida na rangi za upinde wa mvua.Zaidi ya picha milioni 80 na video husambazwa kila siku katika Instagram.Mtandao huo una takriban wateja milioni400 na uliipiku Twitter mwaka 2014.Wakati Instagram ilipoanza ,ilikuwa eneola kukarabati na kusambaza picha,kampuni hiyo ilieleza.Miaka mitano baadaye,ni eneo linalopendwa na jamii kubwa ulimwenguni ambapo watu husambaza picha na video.Watumiaji pia watagundua kwamba eneo la bluu katika nembo ya mtandao huo limeanza kubadilika na kuwa jeupe.Mtindo huo mpya una lengo la kuimarisha picha na video zinazotumwa bila kubadilisha unavyoingia katika mtandao huo.Ubunifu wa nembo hiyo mpya ulianza mwaka mmoja uliopita ,instagram iliambia Newbeat.Tulitaka kutengeza nembo ambayo ingewakilisha mahitaji ya awali ya sasa na ya siku za baadaye.
May 11, 2016
MADHARA YA KUPENDA USIPOPENDWA
Mapenzi si kamari, ridhia kwa moyo! Ni sentesi ambayo kama mtu akitafakari kwa kina kuna kitu kitaingia kichwani kwake, kuna baadhi ya watu huwa wanabahatisha katika mapenzi, unakuta mtu anakuwa na mpenzi bila kujua kama anapendwa kweli.
Mapenzi ni ridhaa, yanatokea moyoni,
Unajua moyo wako ndiyo wenye uwezo wa kufanya uchaguzi sahihi na si uchaguzi bali uamuzi wa moja kwa moja, maana moyo ndiyo wenye uwezo wa kupenda na kuhifadhi pendo ndani yake, kabla hujaanzisha uhusiano jaribu kuzingatia yafuatayo kwani Mapenzi ya kulazimisha yana madhara kama ambavyo Mtembezi Mahaba inakudadavulia.
MOYO WAKO UMEMPENDA? Suala la mapenzi uhusisha moyo zaidi, moyo wako ndiyo mwamuzi wa mwisho katika hilo, hata siku moja usikubali kulazimisha moyo wako kwa mtu ambaye hujaridhia kuwa naye, hivyo achana na imani kwamba ukimkataa kijana fulani basi bahati inaweza kukupita; nani amekudanganya?
SI KAMARI
Utakuta msichana anaingia katika uhusiano na mwanaume ambaye hana mapenzi naye ya dhati lakini kwa kuwa mwanaume huyo ana mali na uwezo wa fedha, huamua kumkubali kwa misingi ya kuwa na tamaa ya mali zake, hufanya hivyo akijidanganya kuwa atajifunza kupenda akiwa ndani ya uhusiano na mwanaume huyo kwa maneno mengine, anajidanganya kwamba atacheza kamari ya mapenzi.
MADHARA YA KAMARI YA MAPENZI!
Yapo mengi, lakini kubwa ni lile la kutotosheka na mpenzi uliyenaye; anaweza akakupa kila kitu lakini ukakosa penzi la dhati, ambalo ndiyo msingi wa mapenzi.
Mapenzi ya kweli siku zote utajisikia mwepesi na huru kwa mwenzako, madhara makubwa zaidi ni pale utakapojikuta ukiingia katika uhusiano na mwanaume mwingine kwa ajili ya kusaka penzi la dhati! Unajua kitakachotokea?
Kama hutaleta magonjwa ndani basi siku moja utafumaniwa, kuna siku lazima utafukuzwa nyumbani kwa mwanaume huyo na kama ana hasira, anaweza kukufanyia kitu kibaya, hivyo ni vyema kufanya uamuzi wa busara kwa kuwa na mahusiano na yule akupendaye.
KASI YA MAGUFULI YAWAANDIKISHA BARUA ZA KUJIUZURU WATUMISHI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Simbachawene amesema kasi ya Rais Dkt John
tayari watumishi wameanza kuandika barua za kuomba kujiuzulu na kutafuta kazi sehemu nyingine.
Waziri Simbachawene ameyasema hayo ingawa hajataja majina ya watumishi hao na halmashauri wanazotoka, katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na ITV na
ameshapokea
kutoka
watatu
ambao hawana
kiutendaji
barua ya kuomba kuachia kazi hizo.
”Kasi ya Rais Dkt. Magufuli haitawaacha watumishi
kufanya kazi kwa maana mazoea kazini hayapo
nimeshapokea
watatu wakiomba kujiuzulu nyazifa zao na kweli kama kuna kiongozi anaona hataweza kwenda na kasi ya Rais na Wizara yangu ni bora aondoke mapema kabla
nitawatumbua
Chawene.
MSANII KINYAMBE AFARIKI DUNIA
Mchekeshaji aliyekuwa anakuja juu kwa kasi Mohammed Abdallah "KINYAMBE" amefariki dunia leo usiku huko nyumbani kwako Mbeya.
Mmoja wa wanandugu wa Kinyambe ameithibitishia saluti5 kuwa msanii huyo wa filamu ambaye pia alikuwa akijulikana kwa jina la James, amefariki baada ya kuugua kwa siku kadhaa.
"BWANA AMETOA BWANA AMETWAA JINA LA MUNGU LIHIMIDIWE".
MUIMBAJI SHILOLE ATAJA MPENZI WAKE WA SASA
Uking’atwa na nyoka ukiguswa na jani lazima utaruka.Baada ya kuvunjika kwa mahusiano na Nuh Mziwanda, taarifa za chini zimezidi kuenea kuwa Shilole ana mahusiano ya kimapenzi na msanii chipukizi wa Bongo Fleva, Nerd aliye chini ya label ya Ommy Dimpoz, PKP.Akiongea kwenye kipindi cha Busati, kinachoruka kupitia Magic FM, Shilole amesema hana mpenzi kwa sasa.“Mimi mpenzi wangu ni hela, Nerd ni rafiki yangu. Ukiwa kwenye mapenzi unakuwa kama kipofu unakuwa hauoni. Ukimkabidhi mtu moyo wako anakuwa anaufinyanga, kwa sasa moyo wangu umestawi tofauti na zamani,” aliongeza.Hata hivyo Shilole amesema hana namba ya Nuh Mziwanda na hajawahi kuwasiliana naye tangu walipoachana. Kwa sasa muimbaji huyo ana wimbo mpya uitwao Say MyName.
BINTI WA MIAKA 19 ANAEDAI KUA NA MIMBA YA PAPA WEMBA AJITOKEZA HADHARANI
Binti wa miaka 19 anadaiwa kuspend one night on the same bed na Hayati Papa Wemba amekua gumzo kwenyemitandao ya kijamii ndani na nje ya Congo(D.R.C) akidai kuwa na ujauzitowa Mfalme huyo wa Rhumba aliefarikiApril 24 mwaka huu baada ya kuanguka jukwaani jijini Abidjan nchini Ivory Coast.Picha zinazodaiwa kuwa copied kutoka kwenye akaunti za social media za binti huyo,zinamuonesha akiwa kwenye pozi tofauti za kimahaba na Papa Wemba,picha ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi ya picha hizo zikionesha tumbo lake na nyingine zikimuonesha akikiss na Hayati Papa Wemba.Mpaka sasa hakuna taarifa yeyote rasmi kutoka kwenye familia ya Papa Wemba juu ya madai ya binti huyo ambae baadhi ya mashabiki wa Mfalme huyo wa Rhumba wameahidi kumsaidia kwa lolote hadi atakapojifungua.
HARMONIZE:MIMI NA DIOMOND TUNATOFAUTI
Kwenye miaka ya 2000 staili ya kuchana ilishika hatamu ambapo msanii kama TID, Mangwea, Profesa J, Juma Nature, Fid Q, Afande Sele na wengine kibao walitikisa game ya muziki wa Bongo Fleva huku kila mmoja akiwa na staili yake inayomtambulisha na kufanya wajulikane na kupata umaarufu.
Hivi sasa game ya Bongo Fleva dizaini kama ladha unapotea siku hadi siku kutokana na kuwepo kwa baadhi ya wasanii kuigana sauti kama ambavyo imekuwa ikidaiwa na baadhi ya mashabiki wa muziki huo, Hit Maker wa wimbo wa Aiyola kuwa moja kati ya wasanii wanaomuiga sauti Star wa Bongo ambaye pia ni meneja wake DIAMOND PLATNUMZ kupitia 255 ya XXL Harmonize amesema
“Ukizungumzia Diamond unazungumzia mtu ambae anamelody ya malalamiko ambayo zimeganda kwenye vichwa vya watu wengi kwa hiyo ukiimba malalamiko lazima utafananishwa, lakini huu ni wakati mzuri wa kutambua huyu ni Harmonise huyu ni Diamond”
Baada ya kufanya kolabo ya ngoma ya Bado iliyobamba na kumuweka Harmonize katika nafasi nzuri kimuziki hivi karibuni amezawadiwa gari aina ya Mark X kutoka kwa uongozi wa WCB.
JE UNAJUA KAMA KUFLASH SIMU NIKOSA LA JINAI?
Kumekuwa na tabia kwa baadhi ya watu ‘kuflash’ simu kunakosababishwa na sababu kadha wa kadha; katika zama hizi za utandawazi vitendo vya watu kuporwa simu za mkononi vimeripotiwa kwa kiasi kikubwa na wengi wao waliona kuwa njia sahihi nikuziflash ili zitumiwe na mtu mwingine bila kujua kuwa ni kosa la jinai kutokana na sheria za mtandao.
Hayo yamebainika wakati zimesalia siku 36 pekee ili Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) kuzima simu zote ambazo hazijakidhi viwango huku Meneja Mawasiliano wa TCRA Innocent Mungy akisisitiza watu kuacha mara moja tabia hiyo kwani kwa kufanya hivyo kutapelekea simu zao kuzimwa ifikapo June mwaka huu kwa kuwa tayari zitakuwa zimetolewa ubora wake.
“Unapoflash simu lazima fundi atakubadilishia Software zilizokuwepo toka mwanzo alafu utakuwa umeharibu ubora wa kile alichotengeneza mwanzo hivyo kutokana na sheria za umiliki unakuwa umetenda kosa la jinai”. Alisema Mungy
Mamlaka ya Mawasiliano imetoa rai kwa wanaonunua simu za mkononi kwa wakati huu wa lala salama kuwa makini kwa kuangalia namba za IMEI kwa kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu wanapunguza bei za simu feki.
BAADA YA MIAKA 46 YA NDOA MWANAMKE MWENYE UMRI WA MIAKA 70 AJIFUNGUA
Baada ya miaka 46 ya ndoa, mwanamke mwenye miaka 70 amejifungua mtoto wa kwanza huko India..Daljinder Kaur amejifungua mtoto wa kiume baada ya kupata matibabu ya IVF kwenye kliniki za uzazi huko India.Kwenye picha akiwa na mume wake wa miaka 79, Kaur alisema yeye na mume wake walikuwa karibu kukata tamaa ya kupata mtoto kutokana na umri wao na kuona Kama Mungu amewalaani wasipate mtoto.Alisema hatimae Mungu amejibu maombi yao na wamepata mtoto na sasa wanajiona wamekamilika.Aliendelea kusema kuwa yeye na mume wake watamlea mtoto wao wenyewe kwasababu huyo mtoto amewapa nguvu mpya katika maisha.Pia anawasihii wote wenye changamoto za uzazi wamuombe Mungu bila kuchoka.... Aliongezea kusema....".....I can't wait to b a grandma!!
TP MZEMBE WAMLILIA SAMATTA
Jina la Mbwana Samatta limeacha historia kubwa nchini DR Congo hususani kwa mashabiki wa Klabu ya TP-Mazembe ambao wameshuhudia timu yao ikishindwa kufanya vizuri kwenye michuano ya Klabu Bingwa. Hapa ndio inaeleweka ni kwa nini Rais wa Timu hiyo Moise Katumbi alikuwa hataki kumwachia Mbwana Samatta.
Mazembe ilitolewa na Wydad Casablanca ya Morocco katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa na kuangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
Thomas Ulimwengu amesema kwamba kwa sasa pengo la Mtanzania mwenzake, Mbwana Ally Samatta linaonekana ndani ya TP Mazembe. Ulimwengu alisema TP Mazembe kwa sasa inamkosa mtu mjanja na mwepesi, mwenye uwezo wa kufunga kama Samatta.
Samatta aliondoka timu hiyo ya DRC Januari mwaka huu baada ya kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na kujiunga na KRC Genk ya Ubelgiji anakoendelea vizuri hivi sasa.
MAKONDA AFICHUA SUKARI ILIYO FICHWA GOROFANI
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda wamegundua Sukari iliyofichwa katika jengo la ghorofa tisa ambalo liko katika jengo linalojengwa katika eneo la Hananasifu -Kinondoni huku mmiliki wa sukari hiyo Bw,Bashir Ismail mwenye asili ya kiasia akitiwa mbaroni na jeshi la Polisi.
Sukari hilo inadaiwa kuingizwa usiku katika jengo hilo huku kikiwa katika mifuko ya viroba vya kilo 25,na ishiri lakini pia ikifungwa katika mifuko midogo ya Plastiki ya kilo moja moja.
Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari amesema baadhi ya wafanyabiashara wameendelea kukaidi agizo la serikali kwa kuficha sukari katika maghara na maeneo mbali mbali na kuahidi kuwa Oparesheni dhidi ya wafanyabiashara hao ni ya kudumu.
Bw, Bashir Ismail ambaye alikuwa chini ya Ulinzi wa jeshi la Polisi alihojiwa na kudai sukari hiyo iliyohifadhiwa katika jengo hilo inapelekwa katika vituo vya kijamii ingawa alishindwa kujieleza jinsi mazingira iliyowekwa huku ikifanyika kazi ya kuweka katika viroba kwa kuwa eneo hilo linafanyika ujenzi na sio kiwandani.
May 10, 2016
TRA YAFAFANUA JUU YA SAKATA LA UGAWAJI SUKARI
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetolea ufafanuzi wa sukari tani 6757 mali ya Kampuni ya El-Naeem Enterprises iliyokamatwa hivi karibuni katika Bohari ya Forodha ambapo imesema ilikuwa chini ya uangalizi ikisubiri vibali husika ili iweze kuruhusiwa kusambazwa nchini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania, Richard Kayombo, amesema sukari hiyo ilikuwa katika Bohari ya Forodha ya uangalizi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania ikiwa imehifadhiwa kusubiri kukamilishwa kwa utaratibu wa kodi, vibali vya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na vibali vya Bodi ya Sukari na hatimaye kuweza kuruhusiwa kutoka.
Sukari hiyo kwa sasa imeruhusiwa kutolewa ambapo mtembezi.com imefika katika bohari hiyo na kushuhudia ikipakuliwa tayari kusambazwa nchini.
RAIS MAGUFULI AGOMEA MUALIKO NCHINI UINGEREZA
Rais John Magufuli amepata heshima ya pekee kualikwa na waziri mkuu wa Uingereza katika mkutano utakaofanyika kuzungumzia mikakati ya mapambano ya rushwa ikiwa ni nchi mbili tu zimepata fursa hiyo kwa bara la Africa ikiwemo pia Nigeria.
Lakini Rais wetu amedai sasahivi amebanwa na majukumu kwahiyo atawakilishwa na Waziri mkuu mh. Kassim Majaliwa
RAIS MAGUFULI AWARUKA FUTI 100 MATAJIRI
Baada ya
sarakasi zilizokuwa zikipigwa na watia nia wa urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka jana na hatimaye kubaki na tano bora iliyopitishwa na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CC) na Mkutano
Mgombea Urais aliyepeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu Dk. John Pombe Magufuli lilipatikana.
kuzisaka
ya
Vita
katika uchaguzi
mbwembwe
kampeni kati ya aliyekuwa Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) chini ya mwavuli wa Ukawa,
aliyekuwa Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Magufuli
kupelekea
na
Uchaguzi
Magufuli kuwa mshindi Oktoba 29 na kuapishwa
kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hivi karibuni
amenukuliwa
vya Habari
itaendelea kutetea na kusimamia haki za wanyonge kwani anaamini wao ndio waliomchagua kwa kura nyingi kuliko matajiri katika kinyang’anyiro cha urais Oktoba mwaka jana
Mkuu.
Akasema
ilichaguliwa na masikini; kama matajiri walifikiri nitakuwa
wamenoa.
masikini na nitawatumikia masikini na si matajiri”.
JINAMIZI LA SELFIE NA MADHARA YAKE KWENYE MAISHA
Mwanamziki kutoka nchini DRC Congo “Koffie Olomide” hivi kaaribuni alirudi kwenye muziki baada ya kimya kikubwa na ujio wake ulikubalika kutokana na Nyimbo aliyorudi nayo kukubalika na mashabiki zake, wimbo huo unaojulikana kwa jina la “selfie” umekuwa gumzo karibu dunia nzima. Lakini tofauti na hiyo nyimbo neno hilo la selfie linamaana nyingine katika matumizi ya simu ambayo kwa sasa kwa asilimia kubwa yamekuwa yakisababisha ajali na kupoteza maisha.
Baadhi ya watu ambao asilimia kubwa ni vijana wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na matumizi maabaya ya simu wakati wakiwa wanatumia njia za uchukuzi na hii kupelekea vijana wengi kufariki kwasababu asilimia kubwa ya watumiaji wa simu ni vijana.
Nchini India mjini Pathakot imekuwa tofauti baada ya kijana wa miaka kumi na tano (15) kufariki dunia baada ya kujipiga risasi baada ya kutaka kupiga picha “selfie” akiwa amejielekezea bastora ambayo kwa Bahati mbaya alijifyatulia risasi, jitihada za kuokoa maisha yake ziligonga kwamba baada kufariki akiwa njiani akipelekwa hospitali.
Nchini India imewahi kutokea tena ajali ambayo kijana mmoja aligongwa na treni wakati alipokuwa anatumia simu akiwa kati kati ya reli na hali hiyo kupelekea kifo chake, kumekuwa na matokeo haya mara nyingi hapa nchini Tanzania iliwahi kutokea msichana kugongwa na treni kwa kutokuweza kusikia honi ya Treni alipokuwa akivuka kwenye reli huku ameweka hear phone zenye sauti ya juu
Tunashauriwa kuwa makini na matumizi ya simu zetu na haswa tukiwa sehemu za barabarani haswa watembea kwa miguu sio vizuri kusikiliza mziki wa sauti kubwa hiyo itatusaidia kusikia tahadhari yoyote tukiwa barabarani na sehemu yoyote inayotumiwa na vyombo vya moto.
NJIA MBILI PEKEE UTAKAZOTUMIA KUKATA TIKETI ZA MABASI YAENDAYO KASI
Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wanaonekana kurejesha matumaini yao kuhusu kumalizika kwa adha ya usafiri jijini humo, hii ni kutokana na kukamilika kwa mradi wa mabasi yaendayo haraka ambapo jana zilitangazwa nauli za mabasi hayo, na hii leo mabasi hayo yameanza majaribio kwa kubeba abiria kwa muda wa siku mbili bure wakati akisubiriwa Rais Magufuli kuuzindua mradi huo rasmi Alhamisi wiki hii.
JINSI YA KUKATA TIKETI ZA MABASI HAYO
Kutakuwa na mifumo miwili ya ukataji tiketi, mfumo wa kwanza ni ule uliozoeleka wa tiketi za karatasi ambazo unakata ukiwa katika kituo cha mabasi hayo, na wapili ni ule wa kutumia KADI MAALUMU, Huu ni mfumo ambao abiria atapatiwa kadi na kujaza salio kwenye kadi hiyo kupitia mawakala watakaotangazwa kwa kuweka kiwango cha nauli ambayo ataweza kuitumia ndani ya wiki au mwezi mzima.
Baada ya hapo abiria atakapofika kituoni atalizimika kuipitisha juu ya mashine maalumu zilizopo kituoni hapo, kwa ajili ya makato ya nauli na ndipo mlango utajifungua kumruhusu abiria kuingia kwenye sehemu ya kusubiria usafiri huo.
KINACHOENDELEA SAKATA LA KUONDOLEWA WAMACHINGA
Hatimaye mgogoro uliokuwepo katika ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Isaya Mnguruni na Baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo, kufuatia taarifa aliyoitoa Mkurugenzi huyo juu ya kuwataka Machinga wanaofanya biashara zao katika Soko la Kariakoo kwenda maeneo rasmi waliyopangiwa ikiwemo Ukonga, Kivule, Tabata Muslim na Kigogo Fresh umepatiwa ufumbuzi.
Hivyo mgogoro huo umefikia tamati baada ya madai waliyokuwa wanadai Baraza la Madiwani kuwa maeneo hayo yalikuwa hayana miundombinu stahiki hivyo Manispaa kupitia Mkurugenzi Mnguruni imeahidi kuyatafutia ufumbuzi na inaendelea na jitihada hizo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini hapa, Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko amesema madiwani kwa kauli moja wameridhia hatua ya Mkurugenzi huyo mara baada ya kuhaidi kutatua changamoto ambazo zilizowapelekea kupinga tamko la Mkurugugenzi, ikiwemo huduma ya choo na maji.
Pia ameongeza Machinga wanatakiwa kuondoka kwenye maeneo hayo haraka mpaka kufikia siku ya Jumamosi ili kupisha mradi wa Mabasi yaendayo Kasi (DART) ambao unatarijia kuanza hivi karibuni.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mnguruni amewapongeza madiwani hao kuungana kwa pamoja katika masuala ya maendeleo huku akiwahadi kutatua changomoto zilizobakia ambao zilikuwa tatizo kwa madiwani hao.
OMMY DIMPOZ ATOA YA MOYONI KUHUSU MAHUSIANO YAKE
Wakati mwingine unaweza kufunguka juu ya hisia zako kwa mtu fulani ingawa wakati mwingine zinaweza kuathiri jamii; pamoja na kwamba mtu hakatazwi kueleza juu ya hisia zake hata kama jamii itatafsiri kwa upande hasi ama chanya. Unataka kujua Star wa Achia Body Ommy Dimpozy amesemaje?
DIMPOZY AELEZA HISIA ZAKE
Ommy Dimpoz amesema kuwa hapendi ku “date” na wanawake maarufu kwa kuwa hakuna siri baina yenu hivyo anaepuka kuwa katika uhusiano na mtu maarufu, amesema kuwa kama asingekuwa maarufu angependa ‘ku-date’ na Star wa Bongo Movie Wema Sepetu.
“Ukidate na mtu maarufu there is no privacy maana unaishi kwa filling za kuridhisha marafiki wa girl friend wako, kama asingekuwa star ningetamani kudate na Wema” ameongeza Ommy Dimpozy
Ommy Dimpozy hivi karibuni amemtambulisha msanii kutoka katika Label ya PKP anayefahamika kwa jina la Nedy Music
SABABU ILIYO MFANYA DIAMOND PLUTNUMZ KUFANYA NGOMA YA MAKE ME SING
Kwa sasa ukitaja Bongo Fleva hutoacha kutaja jina la nyota wa muziki huo Diamond Platnumz kisha wengine wakafuata, hii ni kutokana na juhudi pamoja na kazi nzuri alizofanya Chibu Dangote kama anavyopenda kujiita Simbaaa. Platnumz ni Mtanzania wa kwanza kuwa na followers milioni moja pia Mwafrika wa kwanza kwa upande wa wasanii kuwa na followers wengi kwa sasa ana watu wanaomfuata katika mtandao wa Instagram milioni mbili na laki moja amemshinda hadi Ne – Yo mwenye “followers” milion 1.7; hili pia ni kipimo tosha cha kuangaliwa nani anafuatiliwa zaidi hapa Afrika.
KUHUSU NGOMA YA “MAKE ME SING”
Star huyo ambaye amedumu katika gemu ya muziki kwa miaka 7 hivi sasa amesema nyimbo yake ya Make Me Sing aliyoimba na msanii A.K.A kutoa Afrika Kusini ilifanyika pindi msanii huyo alipokuja katika “Zari White Party” iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City mwaka jana.
“Sababu ya kufanya nyimbo hii hatukuwahi kufanya nyimbo kali kati yangu na A.K.A, pia kipenzi changu Zari alipoisikia aliipenda sana na shemeji zangu kutoka Uganda wanapenda nyimbo zile ndio maana nimekaza sana katika nyimbo ile” amesema Diamond.
Diamond amezishukuru ‘media’ zote kwa kutoa ushirikiano katika ngoma hiyo kwani hakuisambaza lakini imefanya vizuri katika game ya Bongo Fleva na duniani kote
May 6, 2016
MWANAFUNZI ZIJUE MBINU ZA KUFAULU MTIHANI WAKO UKIZINGATIA HAYA.
Mwanafunzi ambaye anataka kupata alama za juu katika mtihani wake lazima awe mtu wa kujiandaa kila siku kwa kutumia dondoo zifuatazo ili kujihakikishia uwezo wa kufaulu na kuepukana na dhana ya kuishi kwa kutegemea bahati
KWANZA:
Kama nilivyosema hapo juu jambo la kwanza ni kuzingatia muda, si vema kukurupuka na kukimbizana nao na kujinyima usingizi wakati ratiba ya mtihani ilikuwa inafahamika na muhusika alikuwa na uwezo wa kujiandaa taratibu kuelekea kwenye siku ya kutahiniwa kwake.
PILI:
Jindae mwenyewe kwa kutafuta na kufanya mitihani iliyopita, huku ukinakili maswali ambayo watunzi wamekuwa wakiyarudia rudia kila mwaka. Njia hii itakuwezesha kujiandaa kwa kuzingatia shabaha na mahitaji halisi ya maswali yatokayo mara nyingi kwenye mitihani. Hakikisha unapata mitihani ya nyuma ya ngazi uliyopo isiyopungua kumi au zaidi na uifanye huku ukihakikisha hakuna swali hata moja ambalo linakushinda. Pamoja na ukweli kwamba ubahatishaji wa vitu si njia sahihi sana, lakini umeonekana kuwasaidia wale ambao ubahatishaji wao huambatana na umakini, hivyo mwanafunzi anatakiwa kuwa na tabia ya kubahatisha maswali ambayo anadhani mwalimu wake anaweza kuyatoa kutoka kwenye daftari lake na hivyo kujiandaa. Ubaharishaji huu, lazima uambane na kile nilichosema awali, yaani kuwa na kumbukumbu ya mitihani iliyopita. Wanasema watalaamu kuwa ulimwengu una tabia ya kurudia matukio, hivyo hata kwenye maswali kuna tabia hii ya kujirudia rudia.
TATU:
Orodhesha maeneo yote ambayo huyaelewi kwenye mtihani hiyo ya nyuma na uyafanyie mazoezi kwa kupata ushauri kwa waalimu wako. Kama kuna mada ambazo hujazielewa kwenye daftari lako hakikisha muda uliojiwekea utatosha kuzielewa.
NNE:
Hakikisha unajizoeza kufanya mitihani ya majaribio mara kwa mara, ambayo utaifanya kwa kuzingatia muda na masharti yote ambayo hutolewa siku ya kufanya mtihani halisi. Haifai mwanafunzi kukimbia majaribio yanayotolewa darasani na mwalimu wake, kwani hayo ndiyo yatamuwezesha kufahamu kama amekamilika kwa kutahiniwa au bado kuna eneo linamtatiza.
TANO:
Hakikisha kuwa kumbukumbu zako kichwani zinaongezeka kadiri unavyojifunza, usiwe mtu wa kusahau sahau uliyojifunza na ikiwezekana eneo ambalo unaonekana kulisahau ndilo ulipe kipaumbele cha kujikumbusha, ikibidi hata kila siku.
SITA:
Angalia kwa makini alama zako za mitihani ya majaribio, ikiwa unapata alama za chini ujue kuna mahali panahitaji nguvu za ziada, shauriana na mwalimu wako maeneo yote unayokosa au yanayokusumbua kabla ya siku ya mtihani.
SABA:
Ili mwanafunzi awe na uhakika wa kufanya vema mtihani wake anatakiwa kuzingatia dondoo zote zilizotolewa kwenye kipengele cha kuimarisha kumbukumbu kichwani, ambazo zimo ndani ya kitabu hiki.
NANE:
Wakati mwingine ni vema ukausikiliza mwili, si vema kuulazimisha kusoma hata kama unaona kuna udhaifu, baadhi ya wanafunzi hukesha wiki mbili mfululizo wakisoma, matokeo yake mwili na akili huchoka na kushindwa kupokea masomo vizuri. Muda wa kupumzika unahitajika.
TISA:
Kabla mwanafunzi hajaingia katika chumba cha mtihani anatakiwa kujiamini kwa kushinda hofu. Eneo hili ni muhimu sana kwani kuna wanafunzi hufeli si kwa sababu hawakujiandaa, bali hukumbwa na hofu muda mfupi kabla ya kuanza mtihani. Hivyo ni muhimu mwanafunzi akaandaliwa kisaikolojia na waalimu pamoja na wazazi wake jinsi atakavyoweza kufanya mtihani bila hofu.
KUMI:
Imani ni hitimisho la mafanikio ya mwanafunzi, haifai kuingia katika chumba cha mtihani ukiwa na mawazo hasi. Kinachotakiwa ni ari ya ushindi au kwa lugha nyingine ni mawazo chanya. “LAZIMA NIFAULU MTIHANI HUU” Imani hii inaweza kujengwa na mtu kupitia kujiamini mwenyewe au kuamini kwa msaada wa nguvu za imani yake ya dini.